Wakimbiaji wenye ulemavu wa viungo, wakianza mbio za kujifurahisha za kilomita sita pamoja na wakimbiaji wengine wakati wa mashindano ya riadha kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘the Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa, Dar, leo.
Baadhi ya wakimbiaji wakianza mbio za kilomita 15 za kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘The Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa, Dar, leo. Rais wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania, Johnson Jason (kushoto) akitoa zawadi kwa mmoja wa wakimbiaji wenye ulemavu, Ernest Nabalale, mara baada ya kumalizika mbio hizo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar leo. Wa pili kushoto ni Makamu wa Rais wa Riadha Tanzania, Dk Issa Ndee. Mshindi wa kwanza wa wanaume wa mbio za kilomita 15 Damian Chopa akimaliza mbio hizo wakati wa mashindano ya riadha kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘the Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa jijini Dar leo. Wasanii wa kikundi cha Wakali Dancers wakitoa burudani wakati wa mashindano ya riadha kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘the Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa jijini Dar leo. Msanii wa muziki wa kizazi kipya AP akitoa burudani wakati wa mashindano ya riadha kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘the Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa jijini Dar leo. Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya Tigo, Elizabeth Amayo (kulia) akitoa zawadi kwa Husna Adam wa Arusha mmoja wa washindi wa mashindano ya riadha kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘the Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa jijini Dar leo. Mbio hizo zilidhaminiwa na Tigo, Exim Bank na wadhamini wengine. Wa pili kulia ni Meneja katika Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Tigo, Fatma Manji







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ankal mbona hukuweka muda waliotumia?

    ankal hii ni mara ya tatu nakukumbusha uwe unaweka muda katika mashindano.

    Mbona kwenye soka unaweka magoli lakini kwenye riadha huweki muda ankal?

    (US Blogger)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...