TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

“TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UGAWAJI WA MAJIMBO NA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU WA 2010”
1.Ugawaji wa Majimbo
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ,Kwa mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,inawatangazia wadau wa Uchaguzi na Wananchi kwa ujumla kuwa itagawa Majimbo ya Uchaguzi yafuatayo.
i.Nkasi
ii.Tunduru
iii.Maswa
iv.Kasulu Mashariki
v.Bukombe
vi.Singida Kusini
vii.Ukonga

Taarifa zaidi kuhusu Majimbo hayo mapya yatakayoanzishwa itatolewa baada ya Tume kukutana na wadau wa Majimbo husika.

2. Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa 2010
Kwa mujibu wa Vifungu vya 37(1)(a) na 46(1) vya Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Vifungu vya 41(1) na 48(1) vya Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ,Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia inawatangazia Wananchi wote kuwa Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 kwa Uchaguzi wa Rais, Bunge na Madiwani itakuwa kama ifuatavyo;



1. UTEUZI WA WAGOMBEA - 19 AGOSTI,2010
2, KAMPENI ZA UCHAGUZI -20 AGOSTI, HADI 30 OKTOBA,2010

3. UPIGAJI KURA 31 OKTOBA, 2010

Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi, Tume itawatangazia Wananchi rasmi, tarehe ya kutoa Fomu za Uteuzi kwa wagombea.

JAJI MSTAAFU LEWIS M.MAKAME
MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. NDO KWELI! NCHI MASIKINI MNAZIDI KUONGEZA MAJIMBO, MAANA YAKE MORE PUBLIC SPENDING, BADALA YA KU-INVEST KWENYE SECTOR ZINGINE ZA UMMA KAMA VILE AFYA, ELIMU, MAJI, BARABATA, SIMU, UMME, INTERNET. NYINYI MANAONGEA IDADI YA WATU WA KUWAPA MISHAHARA NA MAOFISI YAO. NI UVIVU, MWANZO WA HURU KULIKUWA NA WABUNGE WACHACHE SANA NA KAZI ILIKUWA SAFI KWA MFANO NAKUMBUKA WILAYA NZIMA ILIKUWA NA MBUNGE AMA MMOJA AU WAWILI TU NA WAKATI ULE HATA HALI YA KUWAFIKIA WANANCHI ILIKUWA NGUMI LAKINI WALIKUWA WANAENDA VIJIJI VYOTE KWA KARANDINGA/MWAROBAINI/LANDROVER NA WABUNGE WA SASA MARA BAADA YA UCHAGUZI TU HUWAI=ONI TENA WOTE WANAKAA DAR MBEZI BEACH. NINGEELEWA KAMA WANGEKUWA WANAKAA DODOMA NINGEJUWA NI OFISI ZA BUNGE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...