Dk. Ramadhani Dau
HABARI ZILIZOTUFIKIA ZINASEMA WATU WANAOSHUKIWA KUWA MAJAMBAZI YENYE SILAHA ALFAJIRI YA LEO WAMEVAMIA NYUMBA ANAYOISHI MKURUGENZI MKUU WA NSSF DK. RAMADHANI DAU NA KUPORA VITU NA NYARAKA KIBAO KWENYE SEFU KABLA YA KUTOKOMEA.
BAHATI NZURI DK. DAU MWENYEWE NA FAMILIA YAKE WAMENUSURIKA KWANI HAWAKUWEPO NYUMBANI MAJAMBAZI WALIPOVAMIA, ILA WALINZI WAKE WA NYUMBANI WAMEJERUHIWA VIBAYA SANA KUTOKANA NA VIPIGO WALIVYOPATA. INSPEKTA JENERALI WA POLISI IGP SAIDI MWEMA AMEFIKA NYUMBANI HAPO ASUBUHI HII NA UCHUNGUZI UNAENDELEA PAMOJA NA MSAKO MKALI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Duh!!!hali ya wananchi hinapo kuwa duni sana ndipo wanageuka kuwa wanyamba kumbukeni we are all mammals . ngoja niweke hivi mnyama anaweza kuwa pet hila anapo kosa chakula anarudi kuwa mnyama tu !!!
    when will our leaders understand that they need to do change to the society they are living. unaweza kuwa tajiri hila kama society yako ni masikini.one day watakuvamia tu !!!
    mungu ibariki tz

    ReplyDelete
  2. jamani inasikitisha na poleni sana. hapo sasa ndio serikali itambue kuwa hali ya watu ni mbaya. gap kati ya walionacho na wasionacho nayo ni kubwa. kinachofuata ni kuwa kila mwenye nacho akae chonjo kwani wananchi maskini inaelekea sasa wameamua kuchukua uamuzi mikononi kwa kuwanyanganya walio nacho. ni wazi kuwa huyu mkurugenzi wa NSSF mshahara wake haulingani na wa mwalimu au wa nesi na hata polisi. ni pesa hizo hizo tunazokatwa kwenye mishahara yetu ndio inayowalipa hao wakubwa mishahara. nimesikitika kwa kuvamiwa lakini pia ujambazi unaoshamiri hivi sasa jijini iwe changamoto kwa serikali yetu kutambua kuwa endapo njia ya amani ya kuleta usawa haitatumika basi nguvu itatumika

    ReplyDelete
  3. pole sana Dk. Dau.

    ReplyDelete
  4. Any where in the world kama society haitili mkaso swala la inequality matatizo ya wizi na ujambazi yatakuwepo na yatakuwa sana. Jamii inatakiwa itilie mkazo swala la ama kupunguza mwanya wa usawa unaondelea kukuwa kwa kasi au kujaribu kuunda sera zitakazo wafanya wananchi kwa namna moja ama nyingine wajione nao wamo katika mchakato wa maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla. Hili linawezekana kamisa kupitia kufanya mchakato juu ya utowaji wa ELIMU, AJIRA, MATIBABU, SIASA ZA INCLUSIVE, MIUNDO MBINU, KILIMO NA UVUVI, BIASHARA NDOGO NDOGO. Watu wanataka kujiona nao wamo katika mchakato mzima wa maendeleo ya nchi si wachache tu ndio wawe kwenye mchakato huo. sidhani mtu mwenye cha kufanya katika kuchangia maendeleo ya nci na ya jamii kwa ujumla anaweza kujihusisha na UJAMBAZI, kwa vile watu hawanacho na hakuna njia nyngine ya nkato ndo maana wanajihusisha katika ujambazi wapate kwa haraka na wana ile hisia kuwa hali yao ya kutokuwa nacho inasababishwa na few elites so ni vizuri wakachukuwe kwa nguvu. TUKIJALIANA NI RAHISI SANA KUPUNGUZA VITU KAMA HIVYO. TULIJADILI HILI WADAU.

    ReplyDelete
  5. Michuzi umenibania maoni yangu poa wangu kama blog ya jamii ndiyo hivi sawa!Sijatukana na wala sijasema ovyo, mzee umenitenga! nini zaidi unaogopa wakubwa au? Kweli jamaa apunguze matumizi aimarishe jeshi la polisi askari wamwagwe mitaani kama Njugu tuone hao majambazi watapitia wapi. Mfano WENZETU MSUMBIJI KILA KONA KUNA ASKARI,UHARIFU umedhibitiwa ile mbaya. Haya nibanie tena wangu!

    ReplyDelete
  6. NGUME MICHUZI UNATUBANIA WENGI YANI MIE KUSEMA TU KWAMBA HIII INAWEZEKANA WENYEWE KWA WENYEWE WANAFANYIANA TABIA CHAFU KWENYE UONGOZI IMEKUWA VIBAYA WAKATI TUNAJARIBU KUAMSHA WATU? LAZIMA ULINZI UWE MZURI KWA WATU KAMA HAWW NA MIE NIBANIE ILA INSHALLAH MWENYEZIMUNGU ATAJUWA NILICHOANDIKA.

    ReplyDelete
  7. Ni Kumbe nimekosea nimeandika Ngume ilikuwa tu machungu ya kubaniwa Comment ya mwanzo, ila hapo maskini walinzi watakuja kufungwa wao japo wamepigwa vibaya sana. lazima kuna kitu kinaendelea hapo.

    ReplyDelete
  8. Kwanini Dr. Ramadhan Dau?

    Pole sana Dr Dau na familia yako.
    Maggid

    ReplyDelete
  9. Sijawahi kusikia mtu kupatwa na tatizo wengine wanafurahia! Yaani kuibiwa kwa Dr Dau vyeti vyake vya shule na pasipoti ndio kunaambaatanishwa na hali ya umasikini wa nchi! huko mitaani tunapigwa kabali kila siku hata wakati wa miaka ya serikali ya awamu ya kwanza wakati kila kitu kilikuwa bure....Jamani ujambazi ni tabia sio shida....tusichanganye hoja.

    ReplyDelete
  10. ASSALAMU ALAYKUM,
    KWA BAHATI MBAYA TUMEFIKIA WAKATI KWAMBA WATZ WENGI HUPENDA KUIMBA NYIMBO ZA SIASA, HATA BILA TAFAKURI.
    KADHIA YA UJAMBAZI SI MATOKEO YA UMASKINI WA MAJAMBAZI, HASHA. UJAMBAZI NI MARADHI. HATA KATIKA NCHI AMBAZO RAIA KARIBU WOTE WANAWEZESHWA KUPATA MAHITAJI YAO YA LAZIMA, MFANO ULAYA, BADO UJAMBAZI WA AINA MBALI MBALI UNASHUHUDIWA.
    HUKO NYUMBANI, MAJAMBAZI WENGI SI MASKINI HIVYO WA KUSHINDWA HATA KUJIPATIA RIZKI YAO YA MKATE NA CHAI YA SIKU. WENGI WANA UWEZO WA KUMILIKI SILAHA, NA MITANDAO YAO INA GHARAMA NYINGI. ILA, KAMA WALIVYO BINADAMU WENGI, MAJAMBAZI NA UJAMBAZI NI MATOKEO YA KUTOTOSHEKA PAMOJA NA TAMAA!!
    TUKUBALI, HAYA PIA NI MATOKEO YA NYOYO KUKOSA IMANI, NA KUPOROMOKA KWA MAADILI. KUMILIKI SILAHA SI RAHISI KWA MTU MASKINI, SASA NI VIPI HAWA MAJAMBAZI WAWEZE KUMILIKI SILAHA NYINGI, TENA ZA KISASA?
    WAMEZIPATAJE? NANI AMESHIRIKIANA NAO?
    JE JESHI LA [POLISI LINAFANYA KAZI GANI KUMLINDA RAIA, HASA MWENYE MCHANGO MKUBWA KATIKA UJENZI WA TAIFA KAMA DR. DAU?
    KWA UJUMLA MFUMO MZIMA WA ULINZI NCHINI TZ NI MBOVU WENYE UVUNDO.
    MARA NYINGI TU TUMESIKIA MAJAMBAZI WAKISHIRIKIANA NA POLISI KATIKA UHALIFU, AMA KWA KUPATIWA SILAHA AU KUSHIRIKIANA BEGA KWA BEGA KATIKA MATUKIO. JE HAYA NI MATOKEO YA UMASKINI?
    JE HIVI NI KWELI KWAMBA MTANZANIA MWENYE NJAA ASIYEMUDU HATA KULA YAKE ANA UWEZO WA KUTENGENEZA NETWORK YA UJAMBAZI WA SILAHA KUBWA? HUO KAMA SI UONGO NI NINI?
    LAKINI WADAU WENGI WANAPENDA TU KUIMBA NYIMBO ZA WANASIASA, KUWA ETI UJAMBAZI NI MATOKEO YA UMASKINI. INABIDI WAKATI MWENGINE KUTUMIA AKILI YAKO KUANALYSE MAMBO, SIO TU KUIMBA IMBA KAMA KASUKU BILA KUJIULIZA KAMA MAONI YAKO YANA MAKE SENSE.
    POLE SANA DK DAU, INSHAALLAH MWENYEZI MUNGU ATAKUBADILISHIA KWA YALIYO BORA ZAIDI. SOTE TULIO KARIBU NAWE TUKO PAMOJA NAWE KWA DUA, ENDELEA KUWA NA SUBRA.
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  11. issue hii naamini imesukwa huko huko juuu... majambazi na nyaraka zinawahusu nini?

    Dr Dau anajulikana ni mtu wa watu, na naamini kwamtu mwenye akili hii itampelekea ni mchezo umechezwa hapa...mheshimiwa michuzi usiwe kama unaishi karne ya 19..wacha blog yako ishamiri kwa maoni ya kutanua akili..maswala ya kubania maoni ya watu simwenendo mzuri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...