Chef Issa katika libeneke lake la
http://activechef.blogspot.com/
leo anakuja na ratiba ya wiki nzima kwa ajili ya watoto wa miezi 9 mpaka miaka 10 ili angalau kusaidia wazazi kuandaa chakula bora kwa watoto wao.
Chef Issa anasema kama umeipenda ratiba hii ya chakula kwa ajili ya mwanao tuma email kwa:
ili nikutumie ratiba maalumu ikiwa kwenye ms word uweze kuprint pia nikutumie na maelekezo jinsi ya kuandaa vyakula vyote hivyo kwa urahisi zaidi maelekezo ni mengi hayatatosha hapa katika blog yatachukua ukurasa wote.

Naimani mtaipenda sana na
familia zenu watafurahia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Asante sana ndugu yetu CHEF ISSA kwa mawazo yako haya mazuri.
    Tatizo lilopo hapa sio kuandaa chakula bali ni utamaduni wa magahribi uliotumika hapaa. Lakini unasahau kuwa ratiba hii haita saidia sana ambapo bado tupo karibu na Ulezii, Mahindi
    Sio siri umefanya kazi kubwa ya COPY na PASTE ila je mlo hii inaweza kupambana na magonjwa kama malaria kali, maji yasiyo salama na mengineyo mengi? Hauoni kuwa UJI wenye nafaka nyingi bado ni muhimu? Maana hizo B'FAST zote zina nafaka? Japo inakuja kupitia pancakes, cereals, toast or sandwich? Ningeomba sana upatapo muda japo jaribu kutafsiri kila kitu ili iwe imekaa vizuri(badala ya kichwa cha habari tu)!

    ReplyDelete
  2. mbona hamna wali maharage? watoto wanaotumia hiyo watakuwa vibonge hao mpaka utashangaa

    ReplyDelete
  3. we mdau acha maneno ya kejeli soma vizuri kisha uelewe chef katoa ratiba na anasema atatufahamisha zaidi jinsi ya kuandaa inamaana hata majina hayo yote atatueleza zaidi nilimuandikia mail asubuhi kanieleza kua anaweka ratiba mbilimoja itakua ya nyinyi wa ugaibuni na nyingine itatufaa sisi wa huku umatumbini kwa vyakula ambavyo mtanznia yeyote yule ataweza kununua. soma uelewe ndio uongee.

    Mdau Mbezi

    ReplyDelete
  4. AME COPY NA KUPEST WAPI? TUPE USHAHIDI KABLA HUJA PONDA TOA MAELEZO YA BUSARA TUELEWE HOJA YAKO ACHENI UKIRITIMBA WA KUKATISHA TAMAA WATU WANAOJITOLEA KATIKA JAMII KIJANA UKO JUU KAZA BUTI.

    MDAU ITALY

    ReplyDelete
  5. Ankal huyu kijan yuko fiti bwana mi kila siku napitia blog yake duh full maakuli kazi kwetu

    ReplyDelete
  6. TUNASUBIRI HAYO MAELEKEZO NA EMAIL TUMESHATUMA OLE WAKO IWE MIYEYUSHO UTATUTAMBUA ANKAL UWIIIIIIIII ILA KIJANA BAAANGU FANYA KAZI USIOGOPE

    MAKONO KOREA

    ReplyDelete
  7. Chef Issa pole na kazi! unajitaidi sana ila mi nakuomba unajitolea kwajili ya watnzania wenzako na blog yako kweli imesimama sana jitaidi kulenga chakua ambacho kila mtu ataweza kunua ili watanzania wote wafaidike.

    mama Jane

    ReplyDelete
  8. MENU NA RATIBA IMETULIA TUNASUBIRI MAELEKEZO YATAELEWEKA?

    ReplyDelete
  9. Sasa utaitafsiri hivyo chakula kwa kiswhili au ndio imetoka? maana sisi wengine kina maimuna bwana duh!

    mama Tgt

    ReplyDelete
  10. CHEF ISSA ACHANA NA MANENO YA WATU YAKUKATISHA TAMAA SASA SI HAWAWEZI HAYO MACERAIL WE BADILISHA MENU HIYO HIYO WEKA UGALI NA UJI ILI UWAONYESHE HUJA COPY KAMA HAO WENYE FIKIRA FINYU WANAVYOFIKIRI MI NAKUAMINIA NA KILA SIKU NAFATILIA MAFUNZO KATIKA BLOG YAKO KWELI KIJANA UMEIVA KATIKA FANI YAKO NA UNAIFAHAMU WENGI WAKIKAA ULAYA WANAJIFANYA KUSAHAU KISWAHILI WE UNASHUSHA SOMO KWA ULGHA YAKO YA NYUMBANI NA WATU WANAELEWA NAONA KATIKA MAONI MENGI SANA KINA MAMA WANASHUKURU KWELI UMEOKOA NDOA ZAO SASA WANAPIKA NA FAMILIA ZINAFURAHI KWELI MUNGU AKUZIDISHIE NA UENDELEE NA MOYA HUO ILA KIJANA MWANO DUH ULISCAN AU ULIZAA MAANA NAONA COPY HASAAA!!

    MDAU BELGIUM

    ReplyDelete
  11. sasa menu hii mbona inaonekana ghali sana jamani sisi kina mama chanja tutaiweza? chef? mhhh?

    mama chanja!

    ReplyDelete
  12. Chef Issa mbona utawakomesha wabongo mwaka huu...Hiyo ranch dressing, cottage cheese, Fish fillet (ukizingatia kule kwetu ni samaki wa kukaushwa) watatoa wapi hivi????.. mmweeee ungejaribu kuwabadilishia vyakula kulingana na mazingira ya kwetu....
    eg cottage cheese ungebadili iwe maziwa ya mtindi (yogart) etc

    ReplyDelete
  13. naona vizuri ukatia ya kule korogwe kama vile uji,viazi vya kuchemsha,mihogo, n.k

    ReplyDelete
  14. Msimle Chef Issa hebu tumsaidie basi kubadilisha kwa kikwetu varieties zinaweza kuwa nyingi cha muhimu ni ujue protein, carbs na vitamis souces. Mengine yote ni ubatili tu...

    Kwa mlo wa Monday kubadilisha kwa kikwetu...

    Uji wa mtama weka butter, maziwa ya mgando au mabichi, na machungwa... kama unataka pancake basi ni chapati za maji weka baking powder na badala ya cottage cheese tumia yogurt(maziwa ya mtindi)

    Badala ya English muffin pizza....chukua kipande cha mkate uutosti chemsha mchicha kidogo kamua maji changanya na nyanya..weka juu ya mkate na nyunyuzia mafuta ya olive kama unatengeneza (bruchetta) vile na maziwa mabichi

    Veggie platter ....chukua carrot mbichi...ranch sijui itakua nini lakini watoto wetu wanaweza kula carrot bila hii kitu. Kama sio carot basi mpe mwanao pilipili hoho au mkatie nyanya, matango etc

    Then the last meal of the day....Wali changanya na njegere, kuku wa mchuzi kama kawa...kucover mushroom kunywa maziwa na matunda siku imepita...

    Cha muhimu jitahidi mtoto wako ale vyakula whole meal au unprocessed foods...Uji wa dona una afya kuliko uji wa sembe.....

    Chapati za unga wa atta ni nzurikuliko za ule nga mweupeeee.

    Mchicha wa kuchemsha una afya kuliko wakukaanga.

    Matunda ni muhimu sana kwenye diet ya mtoto.......

    My 2 cents


    NB pumpkins na maparachichi ni muhimu sana kwa watoto pia ukiwa unampa mtoto hivi mara kwa mara vitamsaidia pia

    ReplyDelete
  15. Chef Issa tunashukuru kwa juhudi zako, ila mimi nafikiri ungetusaidia zaidi kuimega zaidi kiumri. Manake mtoto wangu ana miezi 9 na nusu lakini sioni hizo french fries na toast zitakatizia wapi.

    ReplyDelete
  16. JAMANI MBONA MWENZENU SIJUI CHAKULA HATA KIMOJA HAPO? lABDA EGGS TU... HEHE HEEE

    ReplyDelete
  17. Anon wa April 115, 05:36
    Kweli umenifurahisha SANA. Yaani watu tungekuwa na moyo wa uzalendo kama huo. Tanzania ingekuwa mbali. Yaani umeona kabisa kwamba something is wrong au lugha haieleweki. Ulichokifanya umetafsiri! Hukuungana na wale waliomtolea maneno huyu mungwana. What a good thing to know, we still have some honorouble people in our society?

    Umenifurahisha sana kweli.

    Watu tuige huu mfano, when something is wrong..play your part tusianze kulaumu tuuu. Hata kama wengine hatuwezi kuafford lakini tumepata mwanga. Infact kwa haya maelezo vyakula vingi alivyoorodhesha Issa..hata kwetu usukumumani vipo...

    Mtoto wa mkulima

    ReplyDelete
  18. Kama unataka kumuuza mnadani akiwa amenenepa (kama wamarekani) basi hiyo ndiyo menyu yake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...