Rais wa chama cha gofu nchini Dionzi Sebugwayo Malinzi amesimikwa rasmi kuwa kamanda wa vijana wa CCM mkoani Kagera katika shughuli iliyofanyika jana mjini Bukoba.Pichani juu nanchini ni Bw. Malinzi akisimikwa Ukamanda na Mwenyekiti wa CCM mkoani Kagera Constansia Nyamwiza Buhiye ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa ya CCM, NEC.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. kwanini hiyo nafasi wasingepewa vijana wenyewe au munaangalia vigezo gani hela au

    ReplyDelete
  2. kaka leo tunakuona kwenye picha ukiwa na mwili wako wa kawaida kabisa lakini ngoja mwaka upinduke utamshinda huyo mama hapo CCM mnavyojuwa kula nguvu zetu sijuwi lini tutapata haki sisi wanyonge

    ReplyDelete
  3. Simba oyeee

    ReplyDelete
  4. We anonymous comment namba 2 hapo.Huyo Dioniz Malinzi ni Rais wa Gofu nchini na amedhamini gofu tangu mwaka 1994 mpaka leo kwa pesa yake ya mfukoni,Huyo hategemei pesa ya CCM ,bali ni mapenzi yake kwa nchi ndiyo maana amekubali hiyo nafasi ya ukamanda wa vijana .SIMBA OYEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  5. hallooo huyo jamaa anaela ndefu sio kawaida!!Huwezi kutaja matajiri kumi hapa Tanzania bila kumtaja Malinzi, anamiliki Cargo stars na vitu vingine kibao!!Multi million dollar companies!!Napinga vikali kusema atakula ela mbuzi ya CCm kwasababu hao ccm wenyewe(JK) kampeni yake ilitumia vijisenti vya huyo bwana. Ishu ni kwanini awe kamanda wa CCM sasa hivi na sio huko nyuma???Analenga nini haswa??

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  6. Jamani msiwe kama vipofu.. Malinzi ni mfanya biashara.. na mara zote wafanya biashara hutaka faida.. kama kweli ni mapenzi kwa nchi yake si achangie ujenzi wa hospitali, shule, watoto walemavu nk, kwani lazima mpaka awe kamanda wa chama cha siasa.. tunajua wafanya biashara walipoingia katika siasa ndiyo waliharibu.. wao hutumia pesa tu..

    ReplyDelete
  7. Hii yote inadhihirisha utata uliopo katika sera ya JK ya kutenganisha biashara na siasa. Ni ukweli uliowazi kwamba sera hii haitekelezeki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...