
Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh.Dk. Emanuel John Nchimbi usiku wa kuamkia leo ametembelea mji wa Kusoma (Reading), Uingereza na kukutana na viongozi wa umoja wa Tanzania UK katika hafla fupi iliyofanyika katika Break Point ya Ukerewe a.k.a The New Vincent Restaurant mjini humo. Shoto ni Mwenyekiti wa CCM tawi la UK Mh. Maina Owino akifuatiwa na Katibu wake Mh. Suzan Mzee

Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Emmanuel Nchimbi akiwa na Mwenyekiti wa TA UK, John Lusingu (kuume) na kushoto kwake ni katibu wa CCM UK, Mh. Susan Mzee akifuatiwa na mjumbe wa TA UK, Bw. Allan Kalinga.

Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Emmanuel Nchimbi akiwa na Mwenyekiti wa TA UK, John Lusingu (pili toka kuume) na mwakilishi wa
http://www.nifahamishe.com/ UK, Mohamed Kindindi (kuume kabisa) na kushoto kwake ni katibu wa CCM UK, Susan Mzee na mwenyekiti wa CCM UK, Maina Owino.
PICHA ZAIDI NENDA
http://www.nifahamishe.com/photos_news.aspx?topic=229&&NewsId=1001
Hang on!!! umoja wa watanzania uk? are you sure? toka lini makao makuu ya umoja wa watanzania uk uko reading?
ReplyDeletemheshimiwa tueleze sababu hasa zilizokufikisha reading, lakini uongozi wa watanzania haupo reading.
by the way, nini jina official la umoja wa watanzania uk? maana kila siku naona unaandikwa vyenginevyo, au kuna jumuia nyingi kila moja ikijinasibu kuwa muwakilishi wa watanzania uk?
Michuzi asante kwa kutupa habari.
ReplyDeleteWewe ni mwelewa tafadhali sana nipe nafasi niseme yafuatayo:
Naipenda sana CCM na ni mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, lakini hao viongozi wa matawi ya chama ughaibuni ndio wanaleta utatanishi na kichefuchefu.
Hili jambo jamani, halina mchango wowote chanya zaidi ya kutupunguzia heshima. Si la lazima na linatushushia heshima. Sisi si wapigania uhuru kama ilivyokuwa ANC pale Mazimbu na vyama vinginevyo ughaibuni.
Na hata kama ingekuwa lazima kwa kuangalia wingi wa watu na ambao wana yumkini kubwa ya kuwa Tanzania kupiga kura mbona hatukuanzisha matawi haya Kenya au Uganda?
Tungángáne kufungua matawi mengi vijijini nchini kwetu na siyo huko Ughaibuni.
CCM tuko juu lakini mambo kama haya ndiyo wengine HATUTAKI.
Leta ajenda hii katika Mkutano Mkuu wa Taifa uone tutakavyopiga kwa kura zaidi ya 80% !!!
Michuzi huwezi kuibana hii maana haya ndiyo mawazo yangu na nitasema hadi naingia kaburini kama hili litaendelea.
Na kwa nakala ya comments zangu hizi kupitia blogu ya jamii ya MIchuzi namsogezea Mwenyekiti wetu na Katibu wetu Mkuu wa CCM Taifa ili walitazame jambo hili na kulipa uzito wake.
Hatuna haja ya kulazimisha mambo hambayo hakika hayana Tija wa faida Kichama.
Tukumbuke Mh. Moi alivyolazimisha 'project yake' ikaki-cost chama cha KANU mpaka leo huko kenya.
Tafadhali michuzi usinibanie hii.
UBALOZI USIPOCHUKUA HATUA MADHUBUTI BASI HAWA WATU WA READING WATAWAGAWA WATANZANIA WALIOPO ULAYA hasa hawa CCM READING ni watu ambao wako so selfish,badala ya kuwaunganisha watanzania wanawagawa.sijui kama viongozi wa TA walialikwa kwenye hili.
ReplyDeleteJamani jaribuni kukwa wastaarabu na kutengeneza sehemu za kukutania isiwe kama sehemu ya mkakati wa sima moto tu. Meza hiyo iliyofunikwa kwa plastic sheet na pembeni imefungwa vifungo kuizuia isipeperushwe na upepo wa fan. Labda kwa vile kikao ni cha
ReplyDeleteCCM na kama kingekuwa kilichoandaliwa na mwenyekiti wa watanzania bila itikadi za chama kimoja natumaini mandhari ya chumba hicho yangebadilika. Mkazi wa kijijini hawazi amini meza aliyokaa mheshimiwa Mbunge ni huko kwa ajuza bibi yetu
Michuzi kwa nini unaniminyia.
ReplyDeleteNilichosema ni kuwa mimi kama mwana CCM sikubaliani na haya matawi ya CCM- Ughaibuni. Wanaotaka washuke vijijini hapa TZ wafungue matawi hayo.
Pili nikatoa maoni yangu kuwa hili suala kama unafikiri kuwa lina mshiko basi liletwe katika Mkutano Mkuu wa CCM Taifa uone jinsi tutakavyolitupilia mbali.
Michuzi wewe una nini sasa mpaka ukatae kutoa hizi comments zangu maana hapa sijatusi mtu naeleza ukweli halafu baadaye unalalamika kuwa watu tunachafua hali ya hewa au kwamba hatujui tuposti vipi maoni yetu.
Umekwenda mpaka huko 'Kusoma' ukazungunga huko lakini hukujifunza kitu bado Michuzi kuhusu hili jambo.
UK na kwingineko watu waendeleze hizo jumuia za watanzania na si vyama vya siasa.
Ukipenda na hii iminye tu lakini tutakuandika na kueleza juu ya hili na jinsi ambavyo hutaki sauti hizi zisikike.