Barabara itokayo katikati ya jiji la Mbeya kuelekea eneo la Soko Matola ambako Halmashauri ya Jiji hilo linataka kuliendeleza kwa kuondoa mbavu za mbwa na kujenga maghorofa.
Na Ripota wetu, Mbeya
Globu ya Jamii ilibahatika kuoneshwa barua hii inayompa mhusika notisi ya kujenga nyumba ya ghorofa kuanzia moja hadi sita, kama hana ubavu aondoke apishe wenye uwezo.
Uchunguzi wetu umebaini kuna manung'uniko mengi toka kwa wadau wahusika, kwani si wote wenye uwezo wa kujenga nyumba ya ghorofa, na kwamba hata wakilipwa fidia haitosaidia sana kwani itabidi wahamie nje kabisa ya jiji maana viwanja sio tu haba bali ghali mno jijiniMbeya.

Wengine wameeleza wasiwasi wao kuhusu hatua hiyo, wakihoji endapo Serikali kuu inajua na nani na lini azimio hilo limepitishwa, wakidai kuwa wengine wamepewa barua hii katika siku ya mwisho na sio miezi mitatu kabla.
Globu ya Jamii inafuatilia sakata hili kwa ukaribu na itatoa maelezokilayatapotatikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hivi baadhi ya viongozi wa hizi Halmashauri wana matatizo gani hasa na nini dhamira yao kwani wasichokielewa katika mazingira halisi ya hapo Bongo ni nini.
    Wadau wezangu wa blog hii kaeni mkielewa ya kwamba hakuna Banki yeyote itakayomkopesha mlala hoi kama huyu-Pia masharti ni magumu sana.Tunawaomba viongozi muingilie kati hili jambo

    ReplyDelete
  2. JAMANI HUU SIO UHUNI KWELI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...