Taasisi ya tzNIC imezindua rasmi kampeni ya kuhuisha (ku-renew) majina ya vikoa vya .tz (.tz domain names). tzNIC pia imeanza promosheni ya miezi mitatu (Mei – Julai 2010) ya kusajili majina mapya ya vikoa vya .tz kwa kulipia gharama ya matengezo TU ambayo ni kati ya Sh. 5,000 (kwa shule za chekechea, msingi na sekondari) na Sh. 20,000 kwa ajili ya makampuni, vyuo na asasi nyinginezo.
Gharama zilizofutwa kwa kipindi husika ni zile za usajili ambazo zilikuwa Sh. 5,000 (kwa shule za chekechea, msingi na sekondari) na Sh. 25,000 kwa makundi mengine.
Taarifa zaidi zapatikana katika tovuti yao
na jarida lenye habari zaidi juu ya zoezi zima zinapatikana hapa http://www.tznic.or.tz/docs/domain_renewal_steps.pdf.
Pia press releases zapatikana hapa
au hapa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...