Meneja wa bia ya Kilimanjaro (TBL) George Kavishe akifafanua jambo mbele ya wasanii waliochaguliwa kuwania tuzo za Kili Music Awards 2010 katika nyanja mbalimbali za sanaa,kwenye semina ya mwisho kwa washiriki hao iliofanyika kwenye hotel ya Paradise,jijini Dar jana jioni.
Mkurugenzi wa kampuni ya One Plus Commonication ambayo pia ni moja ya waratibu wa tuzo za Kili Music Awards 2010,Fina Mango akifafanua jambo na pia kumkaribisha muwakilishi kutoka baraza la sanaa la Taifa,kufafanua baadhi ya mambo kwenye semina ya wasanii waliochaguliwa kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hizo,ambazo safari hii zimekuwa na muonekano mpya na wenye msisimko mkubwa kwa wanamuziki wenyewe na hata wapenzi/washabiki wa muziki hapa nchini.
Muwakilishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Mzee Angelo Luhala akiwaonyesha wasanii nembo ya Baraza la Sanaa la Taifa na pia aliongelea kuhusu baadhi ya wanamuziki ambao waliamua kujitoa kwenye tuzo hizo kwa sababu wanazozijua wao,aidha aliongeza kwa kuwashauri wanamuziki kuwaheshimu mashabiki na wapenzi wao waliowachagua,"hawapaswi kuwaangusha kwa namna moja ama nyingine,kikubwa ni kuonesha na kukubali thamani yao kwako,Wanamuziki tusikubali kujiangusha wenyewe kwa mambo ambayo wakati mwingine yanakuwa hayana maana"" alisema Mzee Luhala.
Mtaalam wa kutengeneza Steji akiwaonyesha wasanii namna itakavyokuwa siku hiyo
Mkurugenzi wa kampuni ya One Plus Communication,Fina Mango na Meneja mkuu wa bia ya Kilimanjaro (TBL) George Kavishe wakiwa katika furaha baada ya kufurahishwa na Mzee Luhala.
Msanii Mrisho Mpoto akitoa hoja.
Prezidaa Nyoshi El Sadaat akiimba moja ya nyimbo zake.
AY akiuliza swali
Deo Mwanambilimbi akiuliza swali la kuhusu usafiri wa bendi iwapo yeye atakuwa ameshinda tuzo hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya One Plus wakiwa katika pozz
Wasanii wakiwa wametulia kwa umakini mkubwa kufuatilia Semina hiyo iliyofanyika jana jioni katika hoteli ya Paradise,iliyopo Benjamin Mkapa Tower,jijini Dar
Wasanii mbambali wanaoshiriki kinyang'anyiro cha tuzo za Kili Music Awardsa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kwa semina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. suleiman salehApril 29, 2010

    Hongera kwa AY kwa maendeleo unayoyapata. Inasikitisha sana kuona vilabu vya Simba na Yanga vikishindwa ama kukataa kuendesha vilabu vyao kibiashara ili kuweza kujitegemea. Anatoyafanya AY ndio ulikuwa mkakati wa wadhamini waliokuwa wakiidhamini Simba METL,NBC na Tanga Cement kuweza kutoa bidhaa kamaambazo AY anatoa bages,Tshirts ,jezi,kanga.key holders nk .Lakini wapi ikawa ndoto na wadhamini wakaamua kuachana na Simba, Inasikitisha wachache waliopinga azma hii nzuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...