Hebu angalia hilo bango la ofisi za kusimamia sheria za jiji/serikali za mitaa na mipango miji. Ukiwa na gari dogo kama Honda CRV RAV 4 etc, huwezi kuona upande mwingine mpaka uchungulie kwa chini, na kama unalo lililo juu kama Toyota landcruiser, ni lazima utoe pua ya gari kwanza, ukigongwa utajua mwenyewe. Je wa-bongo tulio maofisini tunatimiza wajibu kweli?
-Mdau
mdau ulietuma hii picha,natumaini hapo ni karibu sana na hio ofisi ya mtendaji wa kata,whatever,kwa nini usiende na kumweleza hii kero?kuleta hii issue hapa hakusaidii kitu,mambo mengi sana yameletwa hapa ni porojo tu,watz tupeleke kero zetu kunakohusika sio kila kitu mnapost kwa michuzi.mnahakika wahusika wanasoma hayo malalamiko humu kwa michuzi??
ReplyDeleteMimi binafsi huwa nayang'oa hayo mabango ya kizushi na mda ambao ninayafanyia unyama hayo mambango mtu ukirogwa kuingilia kati nakupa nakozi tu!! na wewe sasa naenda kulihukumu hili la msasani leo usiku
ReplyDeleteMdau BAUNSA WA MABANGO
Hii ofisi imefanikiwa sana. Kwa mfano, imeweza kurundika taka taka kwa kuvunja rekodi. Halikadhalika, imeanzisah madampo karibu kila mtaa na hasa zile sehemu zilizo wazi kama Namanag, Magunia na kwa Mister Bolt.
ReplyDeleteChimi ya Mwenye Meza na kigoda, a.k.a mchungaji, ofisi inaweza kukusanya elfu mbili kila unapoingiza pua yako katika ofisi hiyo.
Mafanikio mengine, ni hamasa yao ya kuchangisha kila nyumba shiilingi 5000/ au elfu 10 kwa ajili ya mazingira!!
Mwisho, wamefanikiwa kutengeneza bajeti ya millioni 32 za kuusafisha mfereji wa maji ya mvua (ambao ni msafi).
LOL! HAWAKUWAZA KAMA WEWE, waliwaza watembea kwa miguu tu!kwani ndio wenye dhiki za kutafuta ofisi za serikali!
ReplyDeletewatu kweli hawajitumi maofisini, haihitaji degree kujua hivyo, hawawazi globaly!, nduo hasa sababu ya kutufanya tuwe hivi tulivyo!
Huwa napata shida mwanaume na kende mbili kuamka asubuhi na kuaga familia yake anaenda kazini, wakifika makazini issue ndio kama hivi!
hapa si kosa la idara ya mabango tu, ofisi nzima they should be held accountable for problems like these
NCHI AMBAYO HAIWAJALI RAIA WAKE HATA UHAI WAO UTAIJUA TUU KWENYE VITU VIDOGO VIDOGO VYA USALAMA NA USISITIZAJI MBOVU WA SHERIA ZENYE MANUFAA KWA WOTE. HAPO NI KIBAO CHA SERIKALI NDIO KIWEKWA KIHATARI NAMNA HIYO HALAFU HAKUNA HATA ANAYESHTUKA SASA WATU BINAFSI ITAKUWAJE?! HEBU ANGALIA TRAFIKI WANASISITIZA KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI WAKATI HATA KULAZIMISHA KILA GARI IWE NA INDIKETA NA TAA ZOTE ZINAZOFANYA KAZI WAMESHINDWA... KAZI YAO KUANGALI INSURANCE TUU. NI AIBU SANA! WENZETU WAMEFANIKIWA SANA KUDHIBITI AJALI KWA HILO NA PIA KWENYE KUFUATA SPEED LIMIT. HILI LA SPEED LIMIT NI TATIZO SUGU KABISA TANZANIA NADHANI LINAMSHINDA KILA MTU NCHI NZIMA.. TOTAL SHAME! KAMA TUNASHINDWA VITU VYA MSINGI HIVI NDIO TUTAWEZA MAENDELEO YA MAAN KWELI?
ReplyDeletemZOZAJI
<
Ndio Maana Ukijua Kuendesha Gari Dar Utaendesha Popote Duniani
ReplyDeletemi naona hii blog ni kwa ajili ya habari na mambo ya maendeleo sio habari ya kufuatilia au kujulishana habari za kiumbea.
ReplyDeletewadau tujitahidi
kakudanganya nani ukijua kuendesha gari dar utaendesha popote duniani?? yaelekea hujatoka TZ ndo maana unaongea hivyo. njoo UK ukutane na practical driving test ndo utatuambia kuwa ulipass kwa vile uliendesha gari Dar..lol
ReplyDeleteanony namba 2 kanikuna sana nafsi yangu. ukifanya research ya ajali nyingi zinazotokea kwenye makutano zinatokana na kutokuona vizuri. kumekuwa na tabia mbovu sana ya kulundika mabango mengi kwenye junction na yote yanakuwa chini sana kiasi cha kufanya madereva wasione chochote wanapotaka kuingia barabara kubwa. wawekaji mabango zingatieni hilo vinginevyo tutatafuta vijana mabaunsa wayang'oe na kuyatupilia mbali!
ReplyDelete