Salaam ndugu wote,
Idhaa ya Kiswahili ya BBC leo, Jumatano 28/04/2010 imezindua upya tovuti yake, bbcswahili.com baada ya kuifanyia marekebisho makubwa ya kiuhariri na kiufundi. Tovuti imepata mwonekano mpana zaidi (fomati ya 1024 pixel wide), vile vile sasa ina hadhi ya medianwai (multimedia).

Kuanzia sasa itakuwa na taarifa nyingi za habari na michezo, uchambuzi na makala; lakini kikubwa zaidi ni kwamba utaweza kutazama video na kusikiliza makala kwa nafasi nzuri.
Mapya yatakayokuja hivi karibuni ni kurasa maalum za kombe la dunia na uchaguzi mkuu wa Tanzania.
Kazi ya marekebisho bado inaendelea, tunakaribisha maoni ya wasomaji na wasikilizaji wetu, tuweze kunogesha tovuti iliyosanifiwa kukidhi matakwa ya watumiaji.
Hassan Mhelela
Mratibu
Idhaa ya Kiswahili ya BBC
http://vijanafm.blogspot.com/2010/04/bibi-nitakuja-vikindu-wiki-ijayo.html
ReplyDeleteMbona matangazo ya dira ya dunia hayapatikani live? Rekebisheni bwana!!
ReplyDeletekama alivyosema mdau mmoja hapo juu,ilikuwa vigumu sana jana kupata matangazo yenu live,je kuna uwezekano mkaweka link ndani ya web pia? badala ya hivi sasa ambapo media player imebaki nje ya web.
ReplyDeletemdau birmingham
Ofcoz mwonekano mzuri, ila no Live broadcasting sasa ndio nn?
ReplyDeleteHopefully mna/mtalifanyia kazi.
Mdau, Honolulu Hawaii