Ankal na wadau naomba msaada tutani wa kufahamishwa sababu ya vioo vya sehemu ya kupokea wanaosafiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere kupigwa tinted kama inavyoonekana pichani...
Yaani nimeenda pale na kushangaa kukuta vioo hivyo vimezibwa kuzuia abiria wanaowasili wasionekane na wenyeji wao. wengi niliowauliza sababu walipandisha mabega juu kusema hawajui sababu.
Baadhi ya wafanyakazi nilioongea nao wakanambia ati sababu za kiusalama. Jamani! usalama wa mwenyeji kumuona anayempokea hadi atoe pua nje ndio nini? Sijapata kuona adha namna hii mahali popote duniani. Hivyo naomba kufahamishwa sababu kwani maeapoti ya wenzetu hakuna maajabu kama hayo. ama kuna namna huko nyuma ya pazia??
Mdau wa Ukonga Sitakishari



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Kwa Mdau mleta habari hii:

    Nakubaliana na wewe kuwa hivyo vioo kuwekwa tinted vinaharibu muonekano na pengine kuharibu shauku ya kumpokea mgeni.

    Ila nashindwa kuelewa unaposema nchi za wenzetu hawafanyi hivyo, sijui una maanisha nchi gani hasa...kwa hapa UK Uwanja wa Heathrow (Terminal Zote 5) na Gatwick (South na North) humuoni mgeni mpaka anapotokea kwenye Milango Mikubwa ya abiria Wanaowasili. Humuoni mgeni kabisa akiwa anahojiwa na Uhamiaji, anachukua Mabegi yake au anakaguliwa na Ofisa wa Kodi (Custom).

    Huenda TAA wameiga UK, ila kwa uwanja wetu wa Dar kunahitajika mabadiliko makubwa sana kuliko kuweka tintedi kwenye vioo.

    I wish wangeanza na vile vyumba vya msalani (walau viwa na maji muda wote)!!

    NE, Reading
    UK.

    ReplyDelete
  2. KWANI HAPO NYUMA YA VIOO NDO WANAPOCHUKULIA MIZIGO YAO AU NDO WANAPOHOJIWA NA IMMIGRATION OFFICERS AND CUSTOMS, KAMA NI HIVYO BASI HUO SI UWANJA NI CHOO, GATWICK NA HEATHROW UNAOUZUNGUMZIA NI VIWANJA VUKUBWA MIZIGO NA MAHOJIANO HUFANYIKA MILES AWAY LAKINI ANAPOKARIBIA MLANGONI HAMNA KIZUWIZI CHA KUMZUWIA KUTO MUONA MGENI WAKO ALAFU KU-TINT VYOO OFISINI NI ISHARA YA RUSHWA OFISI SI SEHEMU YA SIRI NI SEHEMU YA UWAZI, UKWELI NA HAKI. WAKUBWA WANALIONA HILI LAKINI HAWALISEMEI KWA VILE WAO HAWASHUKII HAPO NA WALA HAWAHOJIWA NA WALA HAWALIPII KODI VIJIZAWADI VYAO HAPO UWANJANI KINACHOFANYIKA NI UONEZI MTUPU TU

    ReplyDelete
  3. Annoy Hapo Juu

    Umeshawahi kumpokea Mgeni wako Heathrow au Gatwick Airport??

    Usipotoshe watu hapa jamvini hivyo viwanja vyote humuoni mgeni wako mpaka automatic doors zinapofunguka. Kuna milango tena mizito na mikubwa inayokuzuia kuona kitu labda pale inapofunguka wageni wakiwa wanapita ndio unaweza kuona kwa kuchungulia. Hakuko wazi au kuna vioo kama unavyosema wewe.

    Wewe utakuwa hujafika kupokea mgeni Heathrow wala Gatwick; vinginevyo usingekuja hapa kubisha kitu wazi kama hiki.

    ReplyDelete
  4. Wewe mdau unayelalamika na tinted hapo bongo, njoo Beijing International Airport ndo utajua maanake. ni mambo ya kawaida kabisa hayo. kwani hofu yako nini wewe kama ni mgeni wako atafika tu na utampokea, kwani mpaka umuone kwa mbali ndo uamini kwamba kafika? tubadilike wabongo.

    ReplyDelete
  5. Uchizi mtupu; airport escalators hazifanyi kazi, hamna elevators, vyoo maji hamna, eneo la kutoa viza na kujaza forms ni dogo na halina mpangilio, harufu mbaya ya wafanyakazi na eneo lote kwa ujumla. Sasa wanajali usalama wa nani hapo na hivyo vioo?

    Tangu Wafaransa wajenge hiyo airport ni rangi tu ndio imekuwa imekuwa updated.

    Wizi mtupu!!

    Mday NY.

    ReplyDelete
  6. Mtu kashachua tender hapo, japo si la ulazima kama mambo mengine hapo uwanjani. Ndio mambo ya bongo, sasa uliza iyo tint imegaribu kiasi gani nbio utachoka kabisa

    ReplyDelete
  7. SASA BILA KUWEKA TINTED UTAPOKEAJE RUSHWA ??

    ReplyDelete
  8. Sasa si afadhali wangejenga ukuta kabisa kupisha hivyo vioo?
    Kuna maana gani ya kuwa na vioo kama vioo vyenyewe vimwekewa tint?
    Hata hivyo mazingira ya uwazi yamepokwa.

    ReplyDelete
  9. Mi nadhani kuweka vioo watakuwa wanaiga labda vwanja vya huku,lakini si mbaya,hata hapa frankfurt international airport,moja ya vwanja vkubwa kabisa duniani,humuoni mgeni mpaka anatoka nje kabisa,yaani kama hapo,kwa maneno mengine,vioo vina tinted

    ReplyDelete
  10. hini hizo ,kuingia ilikua bureeeeeeeeeeeee, na mtu unapanda mpka juu kabisa kujionea Midege inavyo tua, sasa tunasikia mirio tu hata midege hatuioni tena, na wageni nao, akapum, ghfla bin vu mtu huyu hapa,
    teh teh teh teh.
    Tenda hiyo mtu kasha lamba mamiliani.

    ReplyDelete
  11. dunia nzima mgeni anapotoka haonekani jamani,tofauti kidogo kwa vile bongo mgeni anapokelewa nje ya uwanja,afadhali ya hao huko zanziba utafikiri ni jela hasa hiyo airpot maana sijui hata abiria wanaingilia wapi na kutokea wapi,ila cha kushangaza kuwa Kwa nini Raia wa Tanzania akisafiri na kurudi agongewe muhuri wakati ni raia?basi haina maana kugawa sehemu za raia na wageni.Pia ukisafiri na ndege kutoka zanzibar kwenda arusha au kinyume chake pia unagongewa exit haya si maajabu?

    ReplyDelete
  12. Naungana na Anonymous #5 hapo juu..hao watu hawako serious.sijawahi kuona airport mbaya kama hiyo duniani haina hata hadhi ya kuitwa International Airport,kwanza ni aibu tupu..ukiachana na escalators,elevators,maji chooni.kuna siku mimi nilishuhudia na macho yangu..na umeme unakatika ..yani international gani wanakatiwa umeme hawana hata standby generators jamani..wat a shame!!yani hata huwezi kuona unachoandika kwenye immigration forms, and the blackout lasted for an hour or so mana nilikaa muda mrefu mana flight yangu ilichelewa kuja..ni aibu tupu..utadhani uko uwanja wa mtwara au mwanza bwana..haya na kuweka madustbin kuzuia maji ndo nini..
    hivi hii eapoti yetu haina wahusika au wao wakikinga mkono end of month ndo wanasahau?
    hawajui kuwa the first impression lasts?
    akija mgeni akiona jinsi pasivyo organised meaning na watu wa nchi hawako organised as well.

    ReplyDelete
  13. MIE NAONA WALIOLIFANYA VIZURI MZUNGU AKIKOSA VISA AGEUZWE JUU KWA JUU ASIONE KUKOJE NJE NDIO INAVYOTAKIWA AIRPORT. AIRPORT NYINGI NJE NDIO ZIPO HIVYO TATIZO LA UWANJA WETU WA NDEGE NI SEHEMU MOJA TU INAUZI KUPITA ALAFU UNAFIKA HAPO MLANGONI UNAULIZWA TENA PASSPORT YAKO WAKALALE MBELE. JAMES.

    ReplyDelete
  14. wewe anony unayeshupalia kuwa heathrow terminal 5 humuoni mgeni wako hadi atoke nje acha uongo!! nimetumia heathrow terminal karibu zote na Gatwick pia. kuna sehemu ya kungojea wageni wanaowasili na sio nje..yani unasisitiza kuwa hadi milango ya automatic ifunguke..hehehe. yaani unachekesha sio kidogo. rudi tena heathrow terminal 5 uone wageni wanapokelewa wapi halafu urudi hapa na hizo story zako za uongo..

    ReplyDelete
  15. mimi kwa maoni yangu kabla ya kutia tinted wangeliondowa lile pipa la taka linalovujiwa na maji ya ac ama vipi wadau?

    ReplyDelete
  16. tanzanians they got a bigger hearts but everything else is stinks!not working,out of order,come tommorow and alot of blah blah.SHAME ON YOU LEADERS!!!!!.

    ReplyDelete
  17. Yeah! kwa Tanzania hizo hela wangeziallocate kwenye mambo ya muhimu lakini viwanja ving i hata hapa USA humuoni mgeni wako mpaka atokeze mlango wa Nje...Lakini AC zao hazimwagi maji na kuwekewa mabin ya taka....

    ReplyDelete
  18. makubwa,ukishangaa ya musa utayaona ya filauni

    hatuna viongozi siku nyingi,asa kipindi hiki ndo upupu kabisa

    nyambaf

    ReplyDelete
  19. Mmmeshaanza kulalamika Upuuzi sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...