Mwenyekiti wa Simba Mzee Hassan Dalali akilia kwa furaha
Nahodha wa Simba, Nico Nyagawa akipokea Kombe la Ubingwa wa Ligi kuu ya Vodaconeshno jipya jijini Dar leo kutoka kwa mgeni rasmi, Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana Profesa Kapuya ambaye hafichagi kuwa yeye ni Simba damu.
Kocha Msaidizi wa Simba, Amri Saidi, akibebwa na mashabiki wa timu yake baada ya mchezo kumalizika. Amiri Saidi ndiye aliyeshika mikoba leo kwani kocha mkuu wa simba Phiri yuko kwao Zambia akiuguza
Beki wa kushoto wa Yanga, Amiri Maftah akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Simba, Nico Nyagawa.
Wachezaji wa Yanga wakiwasalimia mashabiki wao kabla ya kuanza kwa mchezo wa ligi ya Vodacom dhidi ya Simba.
Hilary Echessa, akishangilia bao la nne aliloifungia timu yake ya Simba wakati wa mchezo wa Ligi ya Vodacom dhidi ya Yanga uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kulia ni Emmanuel Okwi. Simba ilishinda 4-3.
Mchezaji wa Simba, Uhuri Selemani (kulia) akibadilishana jezi na Abdi kassim wa Yanga









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AUNGURUMAPO SIMBA MCHEZA NANI?

    ReplyDelete
  2. "Mwenyekiti wa Simba Mzee Hassan Dalali akilia kwa furaha" MIMI NI SIMBA DAMU ILA JAMANI NAOMBA MNISAIDIE MWENZENU, HIVI KULIA KISAIKOLOJIA KWA MTU MZIMA IMEKAAJE? MAANA MIMI NIKIONA MTU MZIMA ANALIA HUWA NAMUONA KAMA ANA UDHAIFU FULANI HASA UKUCHUKILIA UNA WATOTO WANAMUONA ANALIA KWASABABU YA MICHEZO.

    ReplyDelete
  3. Picha ya tatu washabiki waliombeba kocha ni kama wanaimba "kimanumanu...kina manuamanua" Sijui kama hizi nyimbo zinaimbwa siku hizi viwanjani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...