
msafara unakaribia mji kasoro bahari
anakoishi mshindi wa Tuzo milionea Benard John

Mshindi wa Tuzo Milionea Benard John akiwaonyesha waandishi wa habari alikolala siku alipopigiwa simu na kuambiwa kuwa amejishindia kitita cha shilingi milioni 100.

Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Nector Foya (kushoto)akimfafanulia jambo Mshindi wa Tuzo Milionea Benard John wakati walipomtembelea Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya kumkabidhi kitita chake cha Milioni 100 hivi punde.

Mshindi wa Tuzo Milionea Benard John(27)kulia akifurahia jambo na Meneja wa Vodacom Tanzania Nector Foya mara walipomtembelea kwenye makazi yake Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya kumkabidhi kitita chake cha shilingi Milioni 100.

Mshindi wa Tuzo Milionea Benard John(27)(katika)akibadilishana mawazo na Mtaalamu wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kushoto)na Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Nector Foya (kulia)wakati walipomtembelea Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya kumkabidhi kitita chake cha Milioni 100 siku za usoni

Mshindi wa Tuzo Milionea Benard John akiwa kwenye picha ya pamoja na ndugu zake huku wakifurahia ngekewa hiyo iliyomwangukia bila kutarajia.
Tunafurahi kuona umasikini unapunguzwa kwa kila aina ya njia, lakini jewapo washauri wowote wa mambo ya Kiuchumi, au Biashara na kumfanyia huyu kaka wepesi wa maisha ili pesa zisije kuisha kwa kupanga wasichana na warembo kama ....au zikawa sababu ya kumporomosha kimaisha?Afanyiwe ukarabati wa kifikra jinsi ya ku-invest hiyo pesa
ReplyDeleteJamaa ndio keshauchinja kama wanavyosema wenyewe. Hapo sasa ndugu wote watahamia kwake. Inaonesha jamaa ni msukuma, kwa maana kaamua kuisogeza redio kitandani aweke nayo pozi. Mwaveja sana.
ReplyDeleteKwakumtangaza hivi hata marafiki zake wa darasa la pili watamtembelea. Kazi unayo kijana.
ReplyDeleteAnkal Michuzi, hivi Tanzania inatoa tax au mshindi anapata ela zote millioni mia moja?
ReplyDelete"Inaonesha jamaa ni msukuma, kwa maana kaamua kuisogeza redio kitandani aweke nayo pozi. Mwabeja sana"
ReplyDeleteKwani Wasukuma ndiyo tunasogeza redio kitandani? Aisee umenichekesha sana. Wewe ni lazima utakuwa mtani wetu tu. Safi sana!
Mie ni mtani ndio samahani nauliza swali la kizushi hivi ni kweli wanaume wa kisukuma hawakatwi ile Nanihiiiiiiii? Swali tu kama maswali mengine please msinielewe vibaya wajameni.
ReplyDeleteNaomba kujibiwa
Muna
Unaamaanisha sweta? yah hawakatwi kaka
ReplyDeleteMtani anony - kimila ni kweli Wasukuma tulikuwa hatutahiriwi. Kuna tatizo?
ReplyDeleteInasemekana kwamba asilimia 82 ya wanaume wote duniani hawajatahiriwa!
http://www.mothersagainstcirc.org/
hahahahaaaa uwiiii yaani nimecheka kwisha khabari duh wasukuma!!!
ReplyDeletedah kweli wasukuma inawezekana?
eti 82% ya wanaume hawajatailiwa + wasukuma
mbavu zangu