MKAZI WA MOROGORO ALAMBA MILIONI 100!
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Leo imechezesha Droo kubwa ya Tuzo Milionea ambapo mteja mmoja wa Vodacom amejinyakulia shilingi Milioni 100.
Katika droo hiyo ya moja kwa moja kwenye iliyochezeshwa kwenye Luninga ya ITV, mteja aliyebahatika kushinda ni Benard John mkazi wa Morogoro na ameshinda kitita hicho ambacho kitabadilisha maisha yake.
Droo hiyo kubwa kuliko zote ya Vodacom Tanzania ilisimamiwa na bodi ya michezo ya kubahatisha nchini (Tanzania Gaming Board).
“Kwa kweli naishukuru sana Vodacom Tanzania kwa kubadili maisha yangu …. Nimefurahi sana,” alisema mshindi kwa njia ya simu.
Huyo ni mshindi wa pili kutajirishwa na Vodacom kupitia promosheni hiyo ya Tuzo milionea, mshindi wa kwanza alikuwa ni Bw. Renatus Mkinga mkazi wa Ukonga Jijini Dar es Salaam aliyenyakua kitita cha shilingi milioni 100 mwezi Aprili mwaka jana.
Mkinga alizitumia fedha hizo kuboresha maisha yake---alinunua gari na kujenga nyumba za kisasa.
liishukuru Vodacom Tanzania kwa kuanzisha promosheni hiyo ambayo alisema hakika inasaidia kubadili maisha ya Watanzania kama ilivyosaidia kubadili maisha yake ambayo sasa yameboreka.
Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, alisema kupitia droo hiyo kubwa ambayo ni mara ya pili kufanyika, mteja mmoja wa Vodacom amekuwa akiuaga umasikini kujishidia shilingi milioni 100 taslim.
Alisema kupitia promesheni hiyo, wateja saba wa Vodacom pia wamekuwa wakijishindia muda wa maongezi wenye thamani ya sh. 100,000 kupitia droo za kila wiki.
Droo hizo zimefanyika kwa wiki 12 na hivyo wateja kujipatia muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni tisa, alifafanua.
Mtingwa alisema promosheni hiyo ni mwendelezo wa promosheni ya Tuzo milionea iliyoendeshwa na kampuni hiyo mwaka jana, na kuchezeshwa kwenye TV moja kwa moja.
“Tuache imani hizo potofu, mimi nimeshiriki mara nyingi katika promsheni hii na hatimaye Mungu akanisaidia nikawa mshindi, hivyo tushiriki kwa wingi ili tupate nafasi ya kushinda,” alisema Mkinga.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...