Habari za kazi Ankal!

Asante kwa kazi ya kutuhabarisha wanajamii. Sisi ni wananchi tuliobahatika kupata viwanja katika mradi wa viwanja 20,000 vilivyopimwa huko kibada (kigamboni). Tumejitahidi kujenga na hata wengine wamekwisha kuhamia.
Tatizo tulilonalo ni kwamba mpaka leo hakuna barabara zilichochongwa kiasi kwamba watu wanakatisha katika viwanja ambavyo bado havijajengwa.pia hakuna maji wala umeme watu wanatumia maji ya visima na wanaishi giza. Tunaomba wahusika walikumbuke hilo eneo.
Asante kwa msaada wako.

Wakazi kibada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Asante sana Mdau,

    Hata mimi nilinunua March 2007 mpaka leo hakuna barabara na tumeambiwa tujenge baada ya miezi 36 ambayo imepita tayari sijui sisi wa block 9 materials tutapitisha wapi? wizara inakatisha tamaa kwa kweli.

    Mpenzi wa blog hii.

    ReplyDelete
  2. Nia na madhumuni ya mradi wa Viwanja 20000, ulikuwa ni pamoja na kupima, kugawia, na kuweka miundo mbinu kama barabara za changarawe, kuvuta maji karibu na viwanja na Umeme. Ndio maana bei pia ilikuwa kubwa kuanzia laki5 na kuendelea. Wajanja wamekula pesa hakuna chochote, Mbweni kwa wakubwa kunasuasua itakuwa huko Kibada ??

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kabisa ndugu yangu. Kwanza kabisa ukiangalia kwamba viwanja hivyo viliuzwa kwa bei nzuri tu kwa serikali. Mwenzio nilishawahi sikia kuwa kuna watu wamekuwa wajanja wakatia ndani baadhi ya hela za mradi ndiyo maana ni upande mmoja tu umechongwa barabara na si wote. Kuna mtu aliniambia yawezekana ni kutokana na kwamba viwanja vingi walijiuzia watu wa Ardhi na mpaka sasa wanaviuza kwa wananchi kimoja baada ya kingine kwa bei ya juu sana. Nchi hiii!!! Acha tu!

    ReplyDelete
  4. YANAYOSEMWA NI KWELI, MIMI NILINUNUA KIWANJA KIBADA KWA MTU AMBAYE ALIKUWA AMESHINDWA KULIPIA KIWANJA CHAKE ARDHI, ALIKUWA ANADAIWA TZS 3,551,456.15, TULIKUBALIANA ANIUZIE KIWANJA JUMLA YA TZS 3,500,000/- HIVYO JUMLA IKAWA MILLIONI SITA NA NUSU YENYE USHEHE. PESA HIYO SI TATITI ILA JUZI TU ILIBIDI KUFYEKA MSITU NA VICHAKA VYA MIIBA HADI KWENYE KIWANJA CHANGU, NAFIKIRI NITAWASILIANA NA MICHUZI ILI NITOE PICHA KWENYE BLOGU HII WAKATI NATENGENEZA BARABARA KWA GARAMA ZANGU, ILA NIMEKWAMA KWENYE KORONGO MAANA PANAHITAJI DARAJA. HIVI HAYA MAMILIONI TUNAYOLIPIA WANAYAPELEKA WAPI? KWA NINI WAZIRI WA ARDHI ASITOE TAMKO JUU YA HATIMA YA BABABARA MAANA NDO INAWAHUSU ZAIDI? HIVI WATANZANIA TUTATESEKA HADI LINI KATIKA MIGONGO YA WATU WASIOPENDA KUHESHIMU MAJUKUMU YAO?
    NAFIKIRI HII NI KERO ILIYO KATIKA CHANGAMOTO INAHITAJI UTATUZI WA MAPEMA.

    NKYABO - BONGO

    ReplyDelete
  5. waheshimiwa kwa watu waliozoea kujza matumbo yao, ni vigumu kufikiria maendeleo. kwanza hii kigamboni imefikia vipi hatima yake na mradi uliokuwa unapigiwa debe na serekali??? maaana hakuna kinachoelewa kila kitu ni kupigana changa la macho...najuwa kuna sehemu kama walivosema wadau kabla yangu kuwa vilipimwa na kuuziwa. Je sehemu ingine waliopropose serekali watakuja kujenga mji wakisasa imefikiaje?????

    kusema ukweli inasikitisha sana kwa serekali yetu ya tz, lakini navojuwa mimi chamtu hakiliki katu. ndio mwanzo wakuanza kujiletea majanga na maafa tusiotegemea. Dhulma ni kitu kibaya sana. Na njaa isiomalizika mwishowe mbaya.

    ReplyDelete
  6. umebana coments yangu ya kithungu michu.poa

    ReplyDelete
  7. mdau aliyotowa lalamiko ili nampa pongezi sana mimi mwenywe nimenunua viwanja uko kibada block 12 na 16 tena kwa bei ya juu kwani niliuziwa na mtu wa ardi cha kusikitisha ni kwamba hakuna lolote hadi sasa hadi unakata tamaaya kujenga kwani utajenga nyumba halafu ulale giza hata kuchonga barabara bado halafu wanajifanya kusema watawapokonya wale watu ambawo hawajajenga kitu kwenye viwanja vyao .viongozi tumieni akili acheni kujifikiria nyinyi tuu mnatia hasira

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...