Pole na kazi ankali,
na habari kwa wana globu ya jamii,
Sasa Ankali mimi nimepata zawadi kutoka kwa jamaa zangu huko Ughaibuni ni Gari aina ya Ploton sasa gari hii haitumii mafuta inatumia Gas sasa nifanyaje na mwezi mzima iko ndani tuu,naomba nisaidiwe kama kuna fundi yoyote anaeweza kubadili system ya Gas kwenda kwa mafuta. ama mtaalam yeyote
chonde chonde
asante
Mdau HP

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Hahahaha!! Mbavu sina!

    ReplyDelete
  2. ploton or proton?

    ReplyDelete
  3. Sasa ni hivi, kuna huyu dada mmoja Engeneer safi sana, a.k.a kiuno hakina spring, yuko fiti sana kwenye hayo masuala. Anafanyia nadhani Kwenye kampuni fulani ya mambo ya gesi, sijui ni kampuni gani, niliona tu kwenye TV, kile kipindi cha Sayansi na Teknolojia.

    ReplyDelete
  4. weka all the detail like proton model gani na nk

    ReplyDelete
  5. Station kwa ajili ya Gas ipo pale ubungo mataa no need of changing

    Dee

    ReplyDelete
  6. Wataalamu wa chuo cha DIT waliwahi kusema wana uwezo wa kubadilisha gari za petroli ili zitumie gesi. Ulizia kama watakuwa na utaalamu wa kufanya kinyume chake.
    Lakini kama upo Dar ingependeza ungeendelea kupeta na gesi mdau. Bei ya gesi iko chini kuliko ya wese.

    ReplyDelete
  7. Mume Wangu, Mikanjuni TangaApril 14, 2010

    Nenda kanunue gesi kule TANZANIA OXYGEN uweke na uanze kupeta mitaani. Ha ha haaaaa

    ReplyDelete
  8. angalia kwenye website ya proton upate maelezo yao mara nyingi gari za gas huwa ni dual fuel labda inatumia petroli pia au dizeli wabillahi tawfiq

    ReplyDelete
  9. Samahani bwana "Mikatapera", mimi ni mshamba kiasi/ niseme sijui chochote kuhusiana na magari yanayotumia gesi kama hilo hapo juu, naomba wanajamii mnisaidie, Hiyo gesi inawekwa kwenye hicho kifuniko hapo ubavuni kulia kama yale yatumiao wese? kama sivyo jee hiyo gesi inawekwa wapi? Aksante Bwana "Mikatapera", kabisa,

    ReplyDelete
  10. Hiyo Gari sidhani kama jamaa anaelea vizuri anachokisema, na hao ndg zake walomtumia gali sidhani kama hawajali kiasi hicho na kumtumia gari ya kutumia gesi ila ninachojua kwa mfan kwa WaMarekani mafuta ya ya gari yaani petroli wao wanaita GAS kwa wadau angalieni isijekuwa kuw aile kitu wanaita LOST IN TRANSLATION!

    ReplyDelete
  11. kaka samahani hiyo gari inatumia petrol ya kawaida tatizo wenzetu wanita jina tofauti tumia wese la kawaida yahaani regu/super ilo kaka ni jina tu tofauti wenyewe wamezoea kuita gas kwa sababu uku vituo vya wese vinaitwa gas station sio kua vinauza gas vinauza wese ka la bongo

    ReplyDelete
  12. mohamed kiswagaraApril 14, 2010

    Kuuliza si ujinga , anyway There is no car in this world that use gas. But they used gasoline which in usa the call it gas in short . There is no difference between gasoline and petrol , which in swahile is mafuta. Go and enjoy ur nice car bro .

    ReplyDelete
  13. Mzee, huhitaji kubadili chochote kwa kuwa GAS ndo MAFUTA. Sisi huku mamtoni hatusemi petrol tunaita GAS, umeelewa?

    Proton ni gari imeundwa na Mitsubish hivyo spea zikianza sumbua waweza tumia za mitsubishi. Ishu ya wese ndo kama hivyo nilivyokwambia GAS = MAFUTA.

    Ukitaka kuhakikisha fungua hicho kifuniko cha tank la mafuta na utasikia harufu ya petrol.

    Sema unachotakiwa kuwauliza ndugu zako ni kuwa inatumia mafuta yepi, legular au premium au disel?

    ReplyDelete
  14. Kaka Trio nakubaliana na wewe. Huyo jamaa hajui kuwa gas ni kifupi cha gasoline(petroleum product/fuel). Ni kama vile ukienda Mbeya wana avocado wanaita katapera, na ukienda Moshi wanaita parachichi. Mwenye gari usipate pressure, hiyo ni gasoline/petrol.

    ReplyDelete
  15. Mbavu sina...lakini labda najicheka mwenyewe hivi gas si ndio hiyo hiyo petrol kweli?

    Kama wamemtumia gari inayotumia natural gas basi kazi. Huwezi toka nje ya jiji ukiishiwa CNG huko basi tena...nani ataibeba na vigaloni kukuletea huko?

    ReplyDelete
  16. wewe uliyotumiwa hiyo gari wenzio wanasema "Gas" wakimaanisha "Gasoline" aka Petrol hebu peleka gari ikawekewe wese na itembee usianze kupulizia gas kwenye gari italipuka, shauri yako.

    ReplyDelete
  17. Duu. Kweli isije ikawa inatumia gasoline ikawa mambo ya lost in translation.
    Kampuni inayotengeneza magari ya Proton ina historia ya kufurahisha...

    http://en.wikipedia.org/wiki/Proton_%28carmaker%29

    ReplyDelete
  18. iyo gari inaitwa proton persona inatengenezwa malaysia ina dual system inaweza ikatumia petrol ya kawaida na gas( natural gas maalumu kwa gari)

    ReplyDelete
  19. Mdau nenda ofisi za TPDC pale Mafuta House aka Benjamin Mkapa Tower. Uliza kitengo cha Utafiti wa matumizi ya gesi kwenye magari, majumbani na viwandani kuna wahandisi kibao watakuelekeza kwa ufasaha kama gari yako inaweza kutumia NGV (Natural Gas) au kurekebishwa mfumo kuweza kutumia NGV lakini kama inatumia LPG (Liquified Petroleum Gas)ujue imekula kwako.

    ReplyDelete
  20. Nenda Chuo Kikuu Mlimani, Kitivo cha Engineering, Department inaitwa Mechanical and Industrial Engineering, Muulizie Dr. Rajabu. Nimeona magari kadhaa wameweka system ya kutumia gas(kama inaendana na gari yako), unaweza kupata lead au reference ya kuweka gas. Nasikia ni Ubungo..! Nadhan nitakuwa nimekusaidia

    ReplyDelete
  21. Hiyo ni Proton Persona na si Ploton
    imetengenezwa Malaysia na kule inafanya vizuri sana. Kwa kawaida inatumia mifumo miwili wa Mafuta na Gas ya NGV ambayo na sisi tunatumia hapa. TPDC walikuja kuchukua utaalamu huo na wao ndio wameanzisha hapa sasa nenda kwao watakwambia cha kufanya ingawa Ubungo pale ni kituo cha kwanza kuuza Gas.

    Ila angalia ina Tank la mafuta kama kawaida na Gas inajaziwa Mbele kwe Engine kwa Pembeni.

    ReplyDelete
  22. Jamani watu wanaomwambia mdau kuwa hakuna gari zinazotumia gas si kweli zipo, na hapa Tanzania mchakato huo unaendelea sina uhakika kama wameshaanza kuitumia. Ila gari yoyote ya Petrol inaweza kubadilishwa mfumo tu ikatumia "GAS". Mdau fanya utafiti kwanza kama ile Gas imeshaanza kutumika maana nasikia bei yake itakuwa chini usije ukabadili wakati mambo tayari. Nadhani ukienda EWURA wanaweza kujua vizuri kuhusu mchakato wa hio Gas ulipo fikia.

    ReplyDelete
  23. HONGERA SANA KWA KULETEWA ZAWADI, MAANA HATA HAPA BONGO SASA WATU WENGI WANAPELEKA GARI ZAO KUWEKEWA CHOMBO MAALUM WATUMIE GAS, CHUO KIKUUU DAR WANA KITENGO KAWAONE WATAKUHAKIKISHIA KAMA NI GAS PEKEE AU WAWEZA KUTUMIA NA WESE PIA, DIT/TRIANGLE WAMESHIRIKIANA WAPIGIE SIMU NAMBA 0784 167000 WATAKUPA MAELEZO WAKO WAPI. MPELEKEE SALAM JAMAA YAKO TENA ZA SHUKRANI =KIGMB

    ReplyDelete
  24. hana lolote anaajionyesha tu!!!!!!! dar sehemu kibao wanajaza gesi

    ReplyDelete
  25. Jaribu kufika Chuo kikuu mlimani -College of engineering and technology - Department of energy huwa wanayo project ya kuongeza system ya gas au petrol, ila itabidi gari yako iwe na system mbili, ya gas na ya petrol, gharama yake ni kama shilingi millioni moja na nusu hivi

    ReplyDelete
  26. NENDA DIT WANABADILISHA NA ACTUALLY WANAUWEZO WA KUBADILI TOKA MAFUTA KWENDA GAS.

    ReplyDelete
  27. Dogo, nenda facult of engineering chuo kikuu cha DSM watakupa ushauri wote na wao wanatengeneza hata magari yenye mfupo wa petrol kuongezea huo mfumo wa GAS na mara nyingi huwa njia zote 2 usihofu au wapigie 0784 464435 kwa ushauri zaidi.

    ReplyDelete
  28. Naomba unipigie no.0783161987 ili nikupe taratibu za kupeleka gari yako ikawekewe hiyo gas na gas yenyewe ni hii ya Songas wana mpaka filling station na kikaratasi cha advert. nimekiacha nyumbani ndo maana nasema tuwasiliane nikujulishe.
    Watanzania majibu mengine ambayo ni ya matusi na utani usioisha yanaturudisha nyuma kimaendeleo wewe unayemjibu hovyo utastaarabika lini?

    ReplyDelete
  29. Usiharibu gari yako bure kwa kuibadili. Hapa Dar kuna kituo cha kuweka GESI. Kiko Ubungo nyuma ya kiwanda cha kutengeneza Kibuku. Kwa nyuma utaona bango au uliza jirani watakuelekeza. Kama sikosei unapita barabara iliyo kati ya Kiwanda cha Kibuku na godown ya Twiga cemet. Utawekewa gesi na kuendesaha gari yako raha mustarehe.

    ReplyDelete
  30. Kuna mtu hapo juu kasema hakuna gari duniani inayotumia Gas. Huo sio ukweli, magari yanayotumia Gas yapu na hiyo gas inaitwa LPG ( Liquefied Petroleum Gas) http://en.wikipedia.org/wiki/Liquefied_petroleum_gas. Unaweza kuconvert gari yeyote ile ikatumia use LPG.

    ReplyDelete
  31. Ninyi msemao eti GAS = GASOLINE kalaghabaho!! Kama hujui kitu kaa kimya kaka/dada.

    Kwa taarifa na faida yenu kuanzia hivi sasa ufahamu kuwa kuna injinui za gari na mitambo mingine hutimia gesi (gas). Inashangaza pamoja na umarekani wenu wote huo bado mnaikweti gas na gasoline?

    Kwa jinsi ambavyo nimeona na ninaendelea kuona hapa nilipo ni kuwa, gari huwa na tanki la kawaida la 'petroli' na mtungi wa 'gesi' ambao hufungwa katika buti ya nyuma ya gari.

    Gari huhitaji petroli kwa 'starting', na kama dereva 'kaswitch on' gas mode basi itaendelea kutumia gesi katika kujiendesha. Na kama kaweka 'petrol' mode, basi itatumia petroli.

    Joooob true true, bado watu hawajatoka tongotongo halafu kelele nyingiii kujifanya wao ndio wajuaji wa majuuu!

    ReplyDelete
  32. UKIANGALIA HIYO PIC YA GARI. HICHO KIFUNIKO PEMBENI NI CHA NINI?, KWA UELEWA WANGU MDOGO NAONA KAMA NI CHA MAFUTA. WACHANGIAJI WENGINE WANASEMA GAS INAWEKWA KWA MBELE HUKO KWENYE ENGINE. SIMPLE, MDAU WAULIZE WALIOKULETEA. HAPA UTACHANGANYWA TU MAANA WENGINE HAWAKO SIRIASI MTU ANPOULIZA.

    ReplyDelete
  33. Hapa German kuna BMW za mwaka kuanzia 1999 zina tumia Petrol na Gas....wala sio gasoline kama wadau wengi wanavyo comment ala natural Gas....watu hapa hawatumii Gas ila zimetengenezwa just in case.

    ReplyDelete
  34. gari imetengenezwa malaysia na inatumia petrol and gas, ambapo kuna button unapress ili kutumia gas or petrol. angalia wasikuingize mjini wewe.

    ReplyDelete
  35. Kaka michuzi me nashauri uwe unaangalia comments nyingine usiziruhusu huku, mtu mpaka kuuliza huku ni kwamba hajui na ameshatafuta njia kaona ajaribu kuuliza huku watu wamsaidie matokeo yake watu wanamkebehi, kwani kuuliza ni ujinga??? watanzania tubadilike, kama we unajua kitu hukuzaliwa unajua ulijifunza na mwenzetu anauliza ili ajifunze, sasa mtu eti "mbavu huna", that crazy, tutabaki kuwa masikini hivi hivi kwa uchoyo wa ku-share maendeleo kisa unajua zaidi au?? ndg yangu me sijui ningekushauri na ninawashukuru waliokushauri maana na mimi wamenifumbua macho. by tha way to live abroad doesnt mean u knw everythin, TUBADILIKE WABONGO KHAAA....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...