Mhe. Ali Mzee (kulia) akijadili jambo na Seneta Rowland Burris wa jimbo la Illinois(Chicago)ambalo kabla ya hapo lilikuwa linashikiliwa na Rais Obama kabla ya kuwa Rais wa Marekani.
Mhe. Ali Mzee, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar alikuwa ziarani Washington DC, Marekani, hivi karibuni ambapo alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Marekani, kutembelea Bunge na Baraza la Wawakilishi la Marekani, na kutembelea makazi ya Rais wa Marekani ya White House katika ziara ambayo aliandaliwa mahususi na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Mazungumzo yake yalikuwa ni elimu kubwa kwa viongozi wa Marekani kuelewa historia ya Zanzibar na Tanzania pamoja na maridhiano ya vyama vya CCM na CUF.
Mhe. Ali Mzee (kulia), Seneta Burris (kati) na Bw.Suleiman Saleh (shoto) afisa katika Ubalozi wa Tanzania jijini Washington DC.
Mhe. Ali Mzee (pili kulia) akiwa White House na Bw. Suleiman Saleh (kulia) na Bw. Mkama (pili shoto) pamoja na ofisa wa Ikulu hiyo ya Marekani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Me love this country so much, ha ha ha ha! Obama kweli mume mtu!

    ReplyDelete
  2. UNADHANI KILA MTU AKIJIPELEKA ATAONANA NA OBAMA!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Bongo kweli ni vichaa. roland Burris ana scandals kibao za corruption kwa kununua kiti. Lakini anapelekwa juu na wabong na kupiga picha na viongozi wetu. Lini umewahi kumwona Roland Burris na kiongozi wa nchi nyingine. Obama is nothing but a socialist and a liar. Obama is the dumbest president ever ruled America. Hana lolote wala chochote. Wabongo amkeni muanze kusoma mambo kwa undani. Acheni kukumbatia wasoshalisti

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...