Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Mama Juliana Yasoda akiongea na vijana leo. Shoto ni Rais wa TFF Sir Leodegar Chilla Tenga
Mama Yasoda akikabidhi bendera ya Taifa kwa timu hiyo
TIMU Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes leo imekadhiwa bendera ya taifa pamoja na vifaa mbalimbali vya michezo na wadhamini wa timu hiyo kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jijini Dar.

Timu hiyo inatarajiwa kuondoka kesho na msafara wa wachezaji 20 pamoja na viongozi watano kuelekea Malawi katika mpambano wake dhidi ya timu ya taifa ya vijana ya huko.

Timu hiyo inajiwinda kwa ajili ya mchezo wa kufuvu katika fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana zinazotarajiwa kufanyika Libya mwaka 2011.

Mbali ya vifaa vya michezo kampuni hiyo imekabidhi hundi yenye thamani ya sh. milioni 83 kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo katika kampeni zake za kucheza fainali hizo.

Meneja uhusiano wa kampuni ya Seregeti ambayo pia ni wadhamini wakuu wa timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda alisema kuwa kampuni yake haina ubaguzi katika masuala ya michezo na ndio maana imejiita katika kudhamini timu ya vijana na kuyataka makampuni mengine ujitokeza katika kuidhamini timu hiyo ambayo ni ya atanzaia wote.

Katika mchezo wake wa kwanza timu hiyolianza vizuri kwa kuibanjua timu ya vijana ya Kenya kwa mabao 4-3 katika mchezo uliofanyika Aprili 10 katika Uwanja wa Uhuru "Shamba la Bibi", Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Yaani ushikaji wa bendera ya taifa watu hawajui ukizingatia ni kiongozi wa juu wa serikali. Kuwa makini

    ReplyDelete
  2. Huu u "Sir" Bongo unagawiwa au kuuzwa kama karanga barabarani???

    ReplyDelete
  3. U-sir wa utani kidogo na wewe mbona una-mind vitu vidogo vidogo. Wewe unataka usikie mzungu anaitwa sir ndiyo umweshiiiimu!! Jiamini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...