askari wa faya wakiwasili jengo la PPF House jijini Dar jioni hii baada ya kutokea dharura ya moto katika ghorofa za saba na 11 katika jengo hilo lililo kona ya barabara ya Morogoro road na Samora avenue
askari wa faya wakipanda ngazi na mitungi yao
kila mtu, hata wale walinzi wa mlangoni, alikimbia
mmoja wa kinamama waliopata mstuko kwa ving'ora vya moto
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Mh. William Erio (suti ya kijivu) akiongoza zoezi hilo lililofana
mdau martin JP anayepiga boxi hapo PPF alitoka mkuku na soda yake mkononi
umati kama kawa ukishuhudia
umati ukiangalia
wafanyakazi wa PPF na makampuni mengine wakirejea maofisini baada ya kuambiwa kuwa hiyo ilikuwa ni rihezo ya dharura ya moto











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. ...Kwa kawaida..nchi za wezetu..kama kuna tukio kama hilo...hutolewa taarifa mapema kwa wafanyakazi wa office na jengo kwa ujumla...I never seen the worst decision like that...other people got pressure..

    ReplyDelete
  2. ovyo sana kwa nini hamkuwataarifu hao watu wanaofanyakazi wenye ofisi zao kwenye hilo jengo? mnakurupuka tuu hamjui kuwa watu wengine wanamagonjwa ya BP tumieni akili ovyooooo kufanya tu mambo alimradi watu wangevunja miguu yao sijui mngewasaidia vipi , wapuuzi sana

    ReplyDelete
  3. Ngoja itokee moto wa kikwelikweli, halafu hao watu watajua ni yaleyale tu ya RIHESO

    Na bongo palivyo siku hizi kama vichochoro vya Itali tgu au Zenji, sijui Faya zitapita WHERE??

    ReplyDelete
  4. sisemi mengi nikaambiwa ni muosha kinywa, lakini jamani moto wa kweli halafu zima moto anapanda na fire extinguisher? jamani jamani huko sio kuuwana lakini? kwa nini hawapewi vifaa vya kuweza kupambana na moto?

    tuseme kama ni moto wa haja unafikiri vitangi hivyo ndio vitazima moto?

    Hivi tanzania hakuna magari ya zima moto?

    ReplyDelete
  5. MICHUZI,michuzi,michuzi,unakosea mdau jp martin anakula vumbi hapo PPF na sio kula boxi- boxi ni la wana wa mtoni

    ReplyDelete
  6. Tanzania inabidi twende na wakati,watu huwa wana-post flyers kuwaeleza watu nini kitakachotokea saa ngapi na lini,mnaweza kuuwa watu hivihiviHalafu nani wa kulaumiwa?.

    ReplyDelete
  7. THIS IS WRONG!FIKIRIA UKIKURUPUSHA WATU HIVI NEW YORK, LONDON, TOKYO, PRETORIA AU GABORONE BILA KUTOA TAHADHARI ITAKUWAJE? MPAKA SIKU ATAKAPOKUFA "KIGOGO" KWA MSHTUKO KWENYE ZOEZI KAMA HILI NDIYO MTATAMBUA KUWA MNAWATREAT BINADAMU KAMA WANYAMA.WAKATI UMEFIKA KUACHANA NA MAMBO YA UJIMA. KWANI SHERIA ZINASEMAJE?

    ReplyDelete
  8. Baada ya watu kuiba pesa za wafanyakazi waliostaafu wanachoma moto ili kuondoa ushahidi, kweli Bongo tambarare!

    ReplyDelete
  9. MAKUBWA MOTO WA KWENYE JENGO KUZIMWA KWA FIRE EXTINGISHA

    ReplyDelete
  10. Kwa bongo ingetoka taarifa ya fire drill asingeshuka mtu..ustaarabu wa watu kuheshimu fire drills ni kwa nchi zilizoendela tu

    ReplyDelete
  11. Faya TingishaApril 17, 2010

    Mdau wa Sat Apr 17, 12:54:00 AM una akili sana. Umeongea point kuliko wote. Wabongo asingeshuka hata mmoja, ndio kwanza watu wangejikorogea chai zao wanywe na zoezi lisingekuwa na mafanikio yaliyokusudiwa, after all kama ingetangazwa isingekuwa na maana kwani watu wa fire wangejiandaa, inabidi nao kuwastukiza kuona wata-respond namna gani... Angetokea mtu kufa ni ajali kazini, kwa kuwa hilo ni shirika la bima lingelipa haraka.
    Kudoz kwa Resesoz

    ReplyDelete
  12. nyie mnacheza na wabongo, uwaambie tutakuwa na fire drill, unafikiri kuna mtu atashtuka, wala hawatajigusa. hivyo walivyofanya ni sawa kabisa

    ReplyDelete
  13. katelephoneApril 17, 2010

    sasa kwani mazowezi ni ya watu kutoka jengoni au fire brigades kupambana na moto? kama ni real fire watu wanaweza kutoka jengoni na kama fire brigades wazembe jengo linateketea! kwa hiyo hapo mtu hafanyiwi practice kukimbia hatari hiyo ni involuntary action utakimbia tu ikitokea ila wanafanyiwa practice jinsi ya kujikinga na kukabiliana na hatari kwa hiyo fire brigades ndio waliokuwa wanafanyiwa mazowezi so still point ya kuwaambia wafanyakazi ipo pale pale that was unfair kwao.

    ReplyDelete
  14. Hebu sikizeni! Faya wa bongo hukinga kila mwezi bilakufanya kazi yoyote. Riheso ni moja kati ya kazi za kubwa ambazo huzifanya kza ufanisi. Lakini lkifumukafaya la ki-true true, thubutuu!

    1. Zana hafifu, eksitinguishaa? Wanastahili medali hawa hata kwa kudhania tu kwamba wataweza kufifisha faya kwa kifaa hicho ambach hakitoshelezi hata kuzima moto wa sevanti kwota!

    2. Kuna mdau hapo juu kasema pwenti. Ivi fikiria, ni saa mbili asbuhi (au muda wowote mbapo barabara zawa na msongamano wa motokaa) alafu kafaya kanaanza taratiiibu pale tunapopaita sitesenta. Hawa faya watafikaje pale? Watapita wapi?

    3. Hizo riheso ni hadaa iliyo uchi kujaribu kuonesha kuwa kuna vitengo au vivuli vya vitengo vinavyoshughulikia usalama wa wanadamu wa Tanzania (sio wananchi, kwani wenye au wananchi ni wachache). Zimamoto za mabua!

    4. Mungu ibariki Tanzania

    Dayasipora

    ReplyDelete
  15. Oyaa hii ni kawaida tu mbona hata huko mnakosema Ulaya mambo ni hivyo hivyo tu. Hakuna cha flyers au hata matangazo.Haya ni mazoezi ya kawaida tu kwa ajili ya kuangalia uelewa wa watu kujikinga na majanga ya moto.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...