wa

Hii si mara ya kwanza kuona jina la asili ya Tanzania likitumiwa na jirani zetu bila kificho, pengine linalozoeleka sana ni lile la matumizi ya Mlima Kilimanjaro.

Mwezi Januari niliandika kuhusu suala la jirani zetu hao kuhamisha sanaa ya michoro ya Tingatinga toka kwenye makaratasi na vitambaa hadi kwenye motion pictures (video) kwa kuteneneza video za katuni.

Nakumbuka kujilaumu mimi na Watanzania wenzangu kushindwa kutumia vilivyo vyetu hadi wengine wanapoviona mali na kuvitumia. Siyo siri kuwa Tinga Tinga asili yake ni Tanzania, hilo linajithibitisha kwa kusoma vitabu mbalimbali na hata kwenye mitandao kama vile dokumenti la www.worldbank.org,
pamoja na
www.tingatinga.info

Habari iliyoandikwa kwenye tovuti ya http://www.slybeaver.com/ inafahamisha kuwa kikundi cha Tingatinga Arts Co operative Society (TACS) toka nchini Tanzania tayari kimeanza mchakato wa kutaka kampuni ya Kenya ya Tiger Aspect Production (TAP) kuacha kutumia jina hilo.

Pia TACS kinataka mashirika yote yaliyoingia ubia na kutiliana saini kwa ajili ya usambazaji wa kazi ya TAP kama vile Walt Disney, BBC, Penguin na Banda, wote wasitishe mara moja utumiaji wa jina hilo ambao unafanyika bila idhini ya TACS.

Watanzania wengi wamekuwa wakilalamika kutokana na aidha uzembe ama uvivu wa Wizara husika na maofisa wake kiasi cha kushindwa kuthibiti rasimili za nchi yetu dhidi ya watu, vikundi na hata mataifa kunufaika navyo huku wenyewe tukiwa tumelala fofofo.

Mfano ni Mlima Kilimanjaro ambao umekuwa ukunufaisha mataifa mengine badala ya sisi kwa uzembe/uvivu pamoja na mtindio wa ubunifu katika kuutangaza. Pia kuna mabaki ya wanyama wa kale ambayo haijulikani yatarudi lini nchini. Hapo hujasema sanaa kibao za kale zilizo katika makumbusho ya hizo nchi zingine.

Utakuta hapo anangojewa Rais Jakaya Kikwete aingilie kati ndipo wanaolipwa mishahara na kula allowance za masemina na mnakongamano yasiyo tija kila kukicha wazinduke na kuanza kazi kwa nidhamu ya woga badala ya kuwa na nidhamu ya ubunifu na kupenda nchi.

Utakuta wahusika wakuu wa kusimamia mambo hayo wanawaachia TACS peke yao wahangaike nalo, badala ya kulivalia njuga kiserikali na kula nao hao jamaa sahani moja. Pia wala hawajui kwamba hii kesi peke yake ni publicity tosha kwa TINGATINGA na TANZANIA yetu.

Watanzania sijui tumelogwa na mchawi wetu kafa...
Inatia uchungu wallahi!



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. inatia uchungu sana...
    kuna watu wamekaa huko serikalini wanalipwa mishahara ya bure na hawafuatilii kitu chochote...
    na inashangaza wanaamka asubuhi kwenda kazini kama watu wengine while hakuna wanalolifanya zaidi ya kulipwa bure sijui wao haiwaumi haya masuala nyeti?
    tunabaki kutizama majirani zetu wakinufaika kwa resources zetu....na bajeti za kufanya kazi wanapewa,wanaishia kukimbilia semina na vikao visivyo na tija,wakirudi yote waliyo discuss vikaoni wamesahau au wanafungia kwenye makabati wizarani...
    TUMELAANIWA............

    ReplyDelete
  2. NAWAPONGEZA SAANA TACS KWA JITIHADA ZA KUFUNGUA KESI,,,KINACHOSIKITISHA IDARA YA UTAMADUNI WAPO NA HIZI TAARIFA WANAZO WAMETULIA TU,,,KUNAWAKATI NAJIULIZA HIVI SEREKALI INAFANYA NINI,,,, NATUSIPOKUWA MAKINI KENYA LAZIMA ITATUTAWALA KWA KILA KITU,,NI JUZI TU WAKENYA WANATAKA KUJENGA UWANJA WAKIMATAIFA WA NDEGE TAVETA LENGOLAO KUBWA NI KULETA WAGENI WAJE WAPANDE MLIMA KILIMANJARO,,,, WATAWALA WAPO KIMYA KAMA VILE HAWAKUSIKIA ,,,,,KUNA UWANJA WA KIMATAIFA WA KILIMANJARO SEREKALI BAADA YA KUWAPA WAWEKEZAJI UCHWARA SASA INATAKA KUMUUZIA AGAKNAN,,, MAUWA KARIBIA YOTE YANAYOLIMWA ARUSHA YANASAFIRISHWA KUPITIA KENYA NA SIO KIA SEREKALI IMEKAA KIMYA,,,WATANZANIA TUAMKE,,,MUDA SI MREFU TUTAKUWA WATUMWA NDANI YA TAIFA LETU,HAKUNA ANAYEJALI WANASIASA WANAJALI MASLAHI YAO NA FAMILIA ZAO TU RASILIMALI ZA NCHI WANAPEWA WATU OVYO OVYO NA BILA GARAMA NCHI IMEKUWA KAMA SEHEMU WAHINDI, WAARABU WAZUNGU WANAKUJA KUNEEMEKEA HAKUNA ANAYEMTETE MYONGE WALA MASLAHI YA NCHI INAKERA SAANA

    ReplyDelete
  3. idara ya utamaduni ipo, watu wanakula mishahara tu, watu wamekuwa wavivu kufikiria, mbona nyerere alipambana nao hata akafunga mpaka na hawa manyangau????????????????????wakenya na washenzi ni juzi tu wametuzuia tusiuze pembe zetu za ndovu,,,hii mijitu haifai hata hii jumuiya ya africa mashariki tuwakatalie in afadhali twende kusini SADEC,,,,,

    ReplyDelete
  4. subira, we can't blame kenyans kwa kuwa washapu kwa sababu sisi tumekaa tunasubiri miujiza.

    ReplyDelete
  5. Watendaji wa Wizara/idara/kurugenzi ya Utamaduni akili zao zimajaa MATOPE.

    ReplyDelete
  6. Tukumbuke kuwa viongozi tumewachaghua wenyewe. Mpaka tutakapoamka na kubadilisha uongozi wetu tuwaweke wenye uchungu na nchi yetu hali itaendelea kuwa mbaya zaidi. Mwaka huu ni wa uchaguzi, tuamue kusuka ama kunyoa.

    ReplyDelete
  7. Ahhh, eehhhh!
    MAAJABU HAYA!
    Kumbe Tinga-tinga, inatumika kupitia kwa majirani zetu!!!

    Nimeshangazwa sana na mamlaka inayohusika,sijui ukweli upo wapi, ni kwamba nimeshaona vipindi vya cartoon vinatumia jina hilo, sio jirani, bali shirika kubwa la habari duniani, sijui wamepata kupitia mamlaka inayohusika ya TZ ama Jirani zetu???

    Kweli viongozi waamke ingawa wamechelewa! Mlima huo wenzetu walishajitangazia sana, Madini ya TANZANITE nayo yanaeleweka kwamba yanatoka kwao, na mengine mengi.
    Serikali ijitahidi kuboresha usafiri wa anga mf Kilimanjaro na Arusha, watalii wengi wanapitia kwa jirani zetu, na booking na malipo yote zinafanywa na mashirika ya huko, TZ tunaambulia leftover's!!
    Kwa ufupi: MFUMO WOTE WA UTALII NA BIASHARA , unatakiwa kurekebishwa, ili kutatua mttz yaliyopo.
    NCHI ITAFILISIWA NA WATU WA NJE, JAMANI TUAMKEEEEE!!!!

    ReplyDelete
  8. Wa tanzania kama kawaida yetu tunajua kulalamika tu ila kufanya kazi hatuwezi.
    Mimi sioni tatizo kwa wakenya kujitangazia mlima kilimanjaro, kwani watanzania tumeshindwa kuu tangaza.
    tatizo ni kwamba bado watanzania tuna kaasili ka ujamaa, wakati wenzetu wana akili ya kibepari hivyo wametuzidi ujanja katika kuwekeza.
    i wish waendelee hivyo hivyo kwani wanatuamsha usingizini.

    Mtanzania mwenye maarifa ila nisiye na uwezo wa kifedha.
    asante.

    ReplyDelete
  9. Jamani tuwe honest we una shati lako,umelianika nje bila ulinzi linaibiwa unaanza kulalamikia polisi? wasanii wa Tanzania hawajishghulishi kabisa kujua rights zao, I know, niliwahi kutayarisha semina na huyu ndugu Kitime kuwapa basics za copyright, tulitoa mialiko 59, walikuja wasanii 12, wawili walitoka kabla ya mwisho kwa udhuru mbalimbali, who is to blame. Familia ya Tingatinga wenyewe they have an infight, lets get ourselves organised kama wasanii wenye mali kwanza ndo tuanze kunyooshea vidole watu wengine baada ya kuibiwa. LAKINI NI KWELI SOCIETY NA SERIKALI YA TANZANIA HAITILII MAANANI UTAJIRI MKUBWA WA NCHI HII UTOKANAO NA UBUNIFU.

    ReplyDelete
  10. Nakubaliana moja kwa moja na Subi kuhusu ulalaji wetu waTanzania na hivi sasa tunakazana kuita wawekezaji njaa basi hao ndo watatufukia kabisa...!Wenzetu wana upendo na nchi zao na jamii yao sisi kazi yetu kuangalia nje na kuishia kawaachia wengine wanufaike na utajiri asilia wetu.Pole zetu!

    ReplyDelete
  11. He mambo gani tena haya!? Mi najua tinga tinga ni greda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...