Mgeni rasmi Ustaadh Suphian ( mwenye jacket la brown) akitoa zawadi kwa vijana. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa madrasa na Leeds Swahili Community Sheikh Amran Rashid (mwenye miwani) na kushoto kwa mwenyekiti ni mwalim mratibu wa madrasa Mufti Haji. pembeni kushoto kabisa ni Ustaadh Malik (Shati nyeupe) na Ustaadh Ridhiwan.
Mgeni rasmi Ustaadh Suphian (shoto) na Mwenyekiti Sheikh Amran Rashid (mwenye miwani) wakimfuatilia kwa makini mwanafunzi Shuena (hayupo pichani) akisoma surat Al imran

Kinadada wakisoma Quran Tukufu
Kinadada wengine wakisoma Quran Tukufu baadhi ya wanafunzi wakiwa na mwalimu wao Ustaadh Ridhiwan aliyeketi nyuma
Wanafunzi wa kiume
wanafunzi wengine

sehemu ya wanafunzi hao

Kaka Michuzi,

Asalaam Aleykum kwako na wasomaji wote wa globo hii ya jamii. Namshukuru Mwenyeezi Mungu (Allah) kwa kutujaalia kuwasiliana tena kupitia globo hii, Ahsante Michuzi.

Ama Allah atujaalie sote upendo, furaha, ushikiano na atuongeze kasi ya utekelezaji wa yanayompendeza kwa faida yetu ya hapa na kesho Akhera Inshaallah.

Kaka Michuzi na wasomaji wote wa globo hii, nawaomba tuungane na ndugu zetu wa Madrasat Mohamad ya LEEDS, U.K. Kufurahia sherehe ndogo ya kuwazawadia wanafunzi bora wa ngazi mbali mbali katika usomaji yakinifu wa Quraan Tukufu.

Sherehe hiyo iliyoandaliwa na uongozi wa madrasa ( Ustaadh Malik, Ustaaadh Ridhiwan, Mufti Haji na Ustaadhi Mundhihir) chini ya mwenyekiti Aran Rashid, iliyofanyika hapa Leeds siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Ebbo Garden, LS9 Hasle Wood drive saa 6.00 mchana, na kuhudhuliwa na wakazi mbali mbali wa maeneo ya Leeds na miji mingine ya hapa U.K. wakiongozwa na mgeni rasmi Ustaadh Suphian.

Kaka Michuzi na wengine wote ambao hamkubahatika kuwa katika sherehe hii, naomba radhi kwa kuwacheleweshea mualiko hata hivyo naamini nyoyo zenu ni kunjufu na kwa utukufu wa Allah nakuombeni tuwaombea dua njema hawa wanetu ili walichokisoma watuelimishe na sisi kwa wao kutafsili katika vitendo

Kaka Michuzi tafadhali tutolee picha hizi kama zawadi kwa wasomaji wote wa globo hii, Mwenyezi mungu atujaalie afya njema, furaha, ushirikiano kwa yenye kheri na upendo katika globo hii

Asalaam aleykum
Mwenyekiti Amran Rashid

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mashallah..

    ReplyDelete
  2. Salaam wanajumuiya,

    Hongera mwenyekiti na jumuiya kwa ujumla kwa harakati zenu za kuwapa vijana ilmu.

    Wapi katibu? Dr(Mahir) nae simuoni.

    Salaam,
    Othman

    ReplyDelete
  3. PETER NALITOLELAApril 04, 2010

    ACTUALLY I AM THINKING THIS THINGS IS VERY NICE BY THE WAY TO STARTED TO TEACH CHILDREN BY THE BUTTOM UP TO SPEAKING AND SAY HOLLY QURAN WHILE THEY ARE CHILDREN IAM VERY HUMBLE TO THIS KIDS BECAUSE IN THE FUTURE THEY CAN BE ABLE TO ANNOUNCE WHO IS PROFECY MUHAMAND WAS. AND HOWEVER TEACHING THEIR OWN KIDS AFTER GROWING UP. MICHUZI I AM HAPPY FOR YOU THAT THIS CHILDREN CAN ALSO SPEAKING ARABIC STRAIGHT FORWARD. BECAUSE IN THE 24TH CUNTURY TODAY KNOWINGLY 2 LANGUAGE ESPECIALLY NOT MOTHER TONGUE IS NOT SEREOUS JOKE MY FRIEND THUS GIVE HIM THIS CHILDREN HIGHER FIVE WELL DONE CHILDREN, GOD BLESS YOU ALL OF YOU. MICHUZI I SALUTE YOU FOR STANDING TALLEST AND LET INDIVIDUALS KNOW YOU ARE CARING THE SOCIETY. THANK YOU TOOOO.

    ReplyDelete
  4. Kila la kheri, very impressing, M/Mungu atawazidishia nyote walimu, wazazi na watoto.


    Mdau USA.

    ReplyDelete
  5. wewe mdau wa Sun Apr 04, 09:37:00 AM, kwa ni lazima uandike kwa kiengereza? kiingilishi chenyewe sijui hata umekisomea wapi? unaandikia kiingilishi kama vile unazungumza kwa kiswahili? hebu pata nafasi basi uende class za jioni ukajifunze hiyo lugha kwanza!!! wacha kututia aibu hapa.

    ReplyDelete
  6. mdau wa Sun Apr 04, 09:37:00 AM, kwani ni lazima uandike kiingilishi hapa? aibu tupu, ni utumbo gani huu umeandika hapa?

    ReplyDelete
  7. Mashekh Allah awape nguvu ya kuliendeleza hilo mnalolifanya...kwanza mnajiondolea dhima kwa Allah(sw)na pia hiyo ndio njia pekeee ya kunusurisha kizazi chetu na mabalaa ya ulimwengu huu tulionao.....Hususan huku tunapo ishi(ulaya)....kama hatukuwasomesha watoto basi tutakuja kulia baadae kwani wataburuzwa na kila linalokuja mbele yao
    BAARAK ALLAHU FII

    ReplyDelete
  8. Duhh jamaa aliposti kwa english hapo juu amenifurahisha sana. ni lazima huyu jamaa ni joker mkubwa sana, toba mbavu zangu weeeee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...