Stars United
Zambia

Na Ripota wetu Ughaibuni
Timu ya Stars inatarajiwa kupambana na Zambia hapo April 24 mwaka huu,mjini Cambridge,Massachusetts mpambano uliopaniwa na Wazambia.

Wazambia waishio Marekani huaa na siku maalumu ya kuwa mwangalifu na ukimwi kila mwaka shughuli hizi hufanyika state tofauti. Mwaka huu wanafanyia Massachusetts na huwa na shughuli za michezo kama vile mpira wa miguu ambapo mwaka huu wameialika Timu ya Tanzania(Stars United) kucheza na timu yao inayoundwa na golikipa aliyewahi kuichezea club ya Zamsure na timu ya taifa.
Wengine ni mabeki Aaron Simutowe aliyewahi kuchezea club ya Zanaco na timu ya taifa ya Zambia,atakuwa akisaidiwa na Peter Chitila na Emmanueli Chibale viungo wa timu hiyo ya Zambia ni Elton Kufa na Yonnah Banda mdogo wa mchezaji Cosmas Banda. Washambuliaji wataongozwa na School boy international Patrick Daka(Sacred Heart University) na Mambo Phiri(Worcester State University).

Stars itakuwa na magolikipa mahili Feisal Omar(mwana njenje)na Hakim Majaliwa(Mlandege),akisaidiwa na mabeki akili nyingi nguvu kidogo, Abdul-Latif Maalim,Muly Chomba,Lemy Mhando,Adam Jongo,Michael Mngodo,Adam Tenga,Libe Mwang'ombe(Germany Defense),Rashid(Beach Boy),Sultan na Evans Shangalai

Viungo ni Yahaya Kheri,Hadji,Helper,Elvis Dotto,Edgar Kisoka,Rahim Chomba,Francis Makala(Simba),Ally Hiral(Mpemba) na Juma Hadikubwa
Safu ya ushambuliaji itaongozwa na Gilles,Mudrick Majaliwa,Shabani Mwampambe,Hamfrey Owen,Inno Geofrey,Ebra Nyagaly,Denis Geofrey anechezea(Greensboro College,Nc),Vicent Ndusilo na Dullah Riyami

Mechi itachezewa stadium iliyopo
77Massachesetts Av,
Cambridge,
Ma.02139
"Stars itachukulia mechi hii kama sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo April 26 mwaka huu utakua umetimiza miaka 46. Kwa sababu hiyo basi tuna mipango ya kuuandikia ubalozi ituletee afisa balozi, Cambridge, Ma siku hiyo ya Mpambano. Tunaomba Wabongo Massachusetts wafike kwa wingi kuipa nguvu stars", amesema mratibu DJ Luke.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. mully unaweza kukumbia kweli kaka.jameel

    ReplyDelete
  2. Picha ya stars imeharibika mbona hamna mchezaji muhimu katika timu, Kipa!

    ReplyDelete
  3. kipa alikua captain anaongea na Refa...kamiss the shot.

    ReplyDelete
  4. Salaam kwa Adam Tenga nimefurahi kukuona kwenye picha. KIla kheir watanzania kwenye mechi hiyo. Hoya na sharifu watakua wanaifuatilia mechi hiyo. Bila kumsahau Yusufu Mkondolo. Swali Erick Baruti mbona hayupo kwenye timu??

    Japo najua kukimbia ishu lakini ndio hivyo.

    Ameir Sweet UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...