Shabiki wa Yanga,Saleh Mohammed, wa Dc akionyesha vidole vitatu kuwa ndio utakuwa ushindi wa Yanga dhidi ya mahasimu wao,Simba

Bw. Suleiman Saleh
Ule mpambano wa Simba na Yanga utakaofanyika jumapili hii April 4, 2010 homa imekua juu kwa kambi zote zaidi kwa Yanga inamuhofia mgeni rasmi wa mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wa DMV na vitongoji vyake. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa afisa ubalozi Bw.Suleiman Saleh.

Washabiki na viongozi wa Yanga wameingiwa na wasiwasi mkubwa wakikumbuka mechi ya April 26 mwaka jana wakati mgeni rasmi alikuwa afisa balozi Doc.Switebert Mkama kwa habari zisizokua rasmi inasemekana ni Shabiki wa Simba na mechi hiyo Yanga walikula kisago 3-2 dhidi ya mahasimu hao wa msimbazi.

Kambi ya msimbazi bado ipo kimya isipokua kocha Kenyata(Patrick Phiri) amehakikisha ushindi mnono kwa wanamsimbazi hao.Wakati huo huo kampuni ya Zion Home Care & Vizion one,inc,imetoa ahadi ya $100 kwa kila mchezaji na itawachomea nyama baada ya mechi wachezaji kama Simba itaibuka na ushindi.

Kocha wa Yanga Yasin Randi amesema vijana wake wapo gado tayari kukirudia kipigo kitakatifu cha september mwaka jana,tunamalizia mazoezi mepesi vijana wangu wamenihakikishia ushidi na wapo kwenye hali nzuri kimchezo.

Watabiri wanaipa nafasi kubwa Simba kuibuka na ushindi kwenye mapambano huo,kwa sababu ya wachezaji wengi wa Stars wanaokuja Dc akiwemo Francis Makala. Stars ina mechi ya kirafiki na Maryland United siku ya jumamosi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Tutawakilisha Simba Fans from Ohio..

    Ushindi msimbazi!!

    Malik.

    ReplyDelete
  2. Hizo timu haziwezi kuwa na majina yao mapaka zikopy majina ya timu nyingine?

    ReplyDelete
  3. Hapo ni beer na nyama tuu...hakuna kitu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...