KATIBU MKUU OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI. YA UTUMISHI WA UMMA, MH. GEORGE YAMBESI AKITOA TAMKO LA SERIKALI JUU YA MGOMO WA WAHADHIRI WA BAADHI YA VYUO VIKUU NCHINI USIKU WA KUAMKIA LEO OFISINI KWAKE JIJINI DAR. PAMOJA NAYE NI MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI BW. CLEMENT MSHANA.

VIDEO HII NA NYINGINE KIBAO
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Ninapenda kutoa dukudku langu kuhusiana na ndugu yetu kutoka ofisi ya rais sekta ya menejimenti. Ninaomba kumshauri huyu ndugu yetu ajifunze kujiandaa na kuisoma na kuikariri na kuielewa vizuri hiyo hoja anayopaswa kuzungumzia kwani haipendezi wakati wa speech kila wakati kuchungulia karatasi kwa kitu kama hiki ambacho hakina a lot technical data au informations za kumchanganya. Mambo yote hayo angeweza kuyasema bila hata hiyo nondo. haipendezi kwa mtu mwenye wadhifa kama wake kufanya hivyo kwani na matokeo yake kurudia rudia point zile zile. Nisamehe ndugu yangu kama nimekuudhi lakini ni vizuri kuelezana ukweli.

    ReplyDelete
  2. Huyu jamaa anapoteza muda mwingi kurudia rudia maneno.

    Aongee bila kurudia, kama waandishi hawajaelewa watauliza maswali.

    ReplyDelete
  3. Hilo tatizo mbona la muda mrefu. Serikali imelikalia tu kwa muda mrefu, sasa nashangaa huyu jamaa anazungumzia budget ya mwakani kwa ajili ya fedha. Utadhani issue hii ni ya jana.

    Walimu wa vyuo wametumia muda mwingi kusoma lakini hawaoni faida ya kusoma kwao.

    ReplyDelete
  4. Walimu wa vyuo wanapata shida licha ya elimu yao ya juu wakati kuna mafisadi hawajasoma wanakula nchi kwa mrija mpana.

    ReplyDelete
  5. Mwaka wa uchaguzi huu, kila mtu apeleke madai yake serikali na kutishia mgomo kama hakuna jibu la kuridhisha.

    JK una kazi safari hii.

    ReplyDelete
  6. Wadau mliozungumzia kuhusu huyu mtoa hoja mpo sahihi kabisa. Huu ni utamaduni tunaotakiwa kuufuta kabisa, iweje mtu mzito unakuja public bila ya kusoma na kuelewa ulichotumwa kuja kukisoma?. Yaani kila kitu ni defensive tu yaani mtu anasoma ili asikosee hata neno moja kwa hofu ya kuwajibishwa toka kwa aliyemtuma. Huu utamaduni wa defensive mmbaya kabisa unaua independent thinking capacity ya watu wengi sana Tanzania.

    ReplyDelete
  7. huyu jamaa na serikali yake vipi??!! mi bado naona kizunguzungu tu hapa, anaposema hili tatizo ni la wahadhiri 62 tu ana maana gani?? the thing is all the public university lecturers are automatically placed under PPF even if you are employed today you will be under that scrap pension fund and their claims are that they immediately be uprooted from PPF and placed under another fund with better terms and that the newly recruited lecturers be allowed to choose a fund of their preference that's the issue and it concerns all the lecturers so when this guy says the problem faces only 62 lecturers i'm surprised and i don't understand that statement, for those who have understood that particular statement please give hand!!! hii kitu ukisikiliza vema madai ya walimu hawa utaona yana ukweli ndani yake, wewe professor na elimu yake yote ambaye kazalisha marais, mawaziri wabunge wakurugenzi, anastaafu kazi analipwa milioni 12 na amefanya kazi miaka 35 UDSM wakati walimu wa shule za msingi ambao wako katika mfuko tofauti wanalipwa hadi milioni sitini haki iko wapi hapo. ndio maana maprofesa wengine wanaona bora waache kufundisha wakagommbee ubunge ili wapate uwaziri serikalini manake chuoni una elimu kubwa lakini ukistaafu unaishi maisha duni sana!! halafu profesa akifuga kuku na nguruwe ili kujenga maisha yake ya baadae mnapiga kelele!!profesa akiamua kula kona akafundishe botswana mnapiga kelele!!
    halafu suala la kuwahamisha kutoka PPF kwenda mfuko mwengine lina gharama gani?? wahamisheni na kuanzia hapo michango yao ya pension iwe inakwenda huko kwenye mifuko mipya wakati nyie mnashughulikia hizo siasa zenu mnazodai zina gharama zake. tanzania bwana!! too much blahblah too much politics little action!! hivi hii nchi inapelekwa wapi??

    ReplyDelete
  8. Ninamsupport mtona maoni wa kwanza apr 29 04:08pm na mdau WA 06:58PM ila inabidi tukumbuke kwamba huyu ni msemaji wa serikali na yeye ametumwa kutoa tamko rasmi na kwa taratibu za nchi hii inabidi asikosee hata neno moja ukizingatia ni ishu nyeti sana maana hapo akikosea neno tu itazua balaa,... Waziri wake ndio anapaswa kuongea lakini msimlaumu yeye ila ni mfumo mzima wa nchi hii tu,..mambo shagalabagala afadhali useme kitu kieleweke kuliko ukosee alafu watu wakushambulie.

    ReplyDelete
  9. sawa michuzi wewe ndiye mmiliki wa blogu.Udumu nayo

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 01, 2010

    SUCH A BORING INFORMATION, YOU CAN NOT EVEN UNDERSTAND WHAT IS HE TALKING ABOUT!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...