Uongozi wa muda wa Jumuiya ya watanzania London unawaomba watanzania wote waishio London kuhudhuria mkutano wa wana-London utakaofanyika ubalozini siku ya jumamosi tarehe 24-April-10 kuanzia saa 5 asubuhi. Mkutano huu unategemea kuongelea maswala ya chaguzi wa viongozi wapya na muundo mzima wa jumiya ya London.

Uchaguzi wa viongozi wa London unategemewa kufanyika tarehe 01-May-10. Mawazo yako ni mchango mkubwa kwa jumuiya na kama unazo sifa za uongozi na ari ya kuendeleza jumuiya mlango uko wazi kwa kila mmoja.

Mahali: TANZANIA HIGH COMMISSION,
3 Stratford Place W1C 1AS,
London.
Tel: +44 (0) 207 569 1470

Muda: kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Tunategemea ushirikiano wako wa dhati.
G. Mboya – TA Director of Communication

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...