mwasisi wa Tanzania Karate-Do.

Kwa mujibu wa kiongozi wa dojo hilo, Sensei Malekia, Jumatatu ijayo tarehe 19/04/2010 shule hiyo itafanya sherehe kubwa ya kutimiza miaka 35 toka izaliwe na siku itaitwa "Sensei Nantambu Camara Bomani Day" kumuenzi mwanzilishi wake. Sensei Malekia anaakaribisha wale wote waliowahi kupita hapo dojo kujumuika nao katika 'demonstration' maalumu ya kusherehekea siku hiyo hapo hapo Zanaki Primary School kuanzia saa 12 jioni.



habari za awali za dojo hili
Duuu....Mungu Mkuu amlinde ndugu Sensei Camara Bomani popote pale alipo. Huyu Mmarekani mweusi aliyekuwa mwalimu wetu miaka ile ya Sabini wakati shule ya Goju Ryu Karate Do Zanaki ikianza alileta mapinduzi makubwa ya kiafya hapa Bongo. Licha ya kujifunza kusema Kiswahili haraka, alikuwa akitembea kwa miguu, akipanda basi na kula ugali nasi. Alitufundisha kuipenda Tanzania na kuhusudu afya zetu. Kama kuna mgeni aliyesaidia kubadili tabia za vijana wa Kibongo kupitia michezo na mazoezi basi ni huyo kaka Bomani. Ni vizuri shule inaendelea kumtaja, na hongera Michuzi kwa kutuletea habari hizi; labda wangekupa pia picha zake? Lazima zitakuwa Daily News maana kuna wakati alifanya mahojiano pale mwaka 1975-83. Nilionana naye alipokuja akielekea Zimbabwe mwaka 1983. Tungependa kuelezwa je wanafunzi viongozi wa mwanzo akina "Sempai" Mabruki, mwenzake Sempai Daudi na Sempai Shoo ( yule Mchagga aliyeungua moto karibu afe lakini akaendelea kufanya na kufundisha Karate, YMCA Moshi) wako wapi siku hizi?
ReplyDeleteShughuli za namna hii ndiyo zinatakiwa Bongo, maana hujenga nidhamu, adabu, afya na akili hasa kwa vijana wanaokua na kupunguza uvivu na mawazo ya kimaskini. Kutokana na mafunzo katika shule ya Zanaki, shughuli hii imenisaidia mimi binafsi hadi leo...
Sensei Malekia bado una shine.
ReplyDeleteSafi sana.
(US Blogger)
Safi sana sensei nakumbuka enzi za miaka ya 80S wakati unatufundisha kama ningekuwepo dar ningeudhuria sherehe hii lakini tupo pamoja keep it up guys.
ReplyDeleteMOODY CHAM TX
Hivi Kuhitimisha na Kuadhimisha ni neno moja?
ReplyDelete