Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akikielezea kinywaji kipya cha Grand Malt ambacho hakina kilevi kilichozinduliwa leo katika Hoteli ya City Garden,Gerezani jijini Dar.
Meneja wa TBL anaeshughulikia Bidhaa za Kimataifa,Consolata Adam akielezea namna kinywaji kipya cha Grand Malt kitakavyofanya vizuri sokoni kwani ni kinywaji kinachoweza kunywewa na mtu yeyote kutokana na kutokuwa na kilevi cha aila yeyote ile.
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa TBL,Nicholaus Brooks kwa pamoja wakifungua mapazia ya jokofu lililosheheni vinjwaji vipya vya Grand Malt katika ujinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika jioni ya leo katika hoteli ya City Garden,Gerezani jijini Dar.
Jokofu likifunguliwa kwa uashirio wa uzinduziMkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja (kushoto) na Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa TBL,Nicholaus Brookes wote kwa pamoja wakinywa kinywaji cha Grand Malt wakati wakikizindia kinywaji hicho katika hoteli ya City Garden,jijini Dar jioni ya leo. cheeazzzz
vijana wakitoka burudani huku wakiwa wamenyanyua juu kinywaji kipya na kisicho na kilevi cha Grand Malt
Burudani ikiendelea
Wapendezesha Ukumbi
Wageni waalikwa
Wadau wa Executive Solutions,toka shoto ni Mike Mukunza,Tamika Zaun,Mgeni katika hafla hiyo pamoja na Carol Ndosi wakijiburudisha na kinywaji kipya na kisicho na kilevi cha Grand Malt katika uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika katika hoteli ya City Garden,Gerezani jijini Dar jioni ya leo. Wageni waalikwa pamoja na baadi ya wanahabari toka vyombo mbali mbali vya habari,wakiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kinywaji kipya na kisicho na kilevi cha Grand Malt uliofanyija jioni ya leo katika hoteli ya City Garden,Gerezani jijini Dar.


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imezindua kinywaji chake kipya cha Grand Malt ambacho hakina kilevi.

“Kinywaji hiki kipya kitaisaidia TBL kuwa na ushindani wa hali ya juu katika vinywaji vingine visivyo na kilevi kutokana na ubora na ladha yake,” alisema Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho katika Hoteli ya City Garden – Gerezani jijini Dar es Salaam.

Kinywaji hicho kimetengenezwa kwa maji,sukari,shayiri,lactose na vitamini huku kikiwa na ujazo wa mililita 330 katika kopo. Bei ya rejareja iliyopendekezwa na TBL ni Sh. 1,000 kwa kopo na Sh. 19,200 kwa katoni moja yenye makopo 24.

Minja alisema, Grand Malt ni kinywaji cha kipekee kutokana na ukweli kwamba kina vitamini pamoja na mchanganyiko wa maziwa.

Alisema kinywaji hicho kinawafaa wafanyakazi wenye shughuli nyingi lakini pia kinafaa kwa matumizi ya nyumbani, wafanyakazi wa usiku, wanafunzi, vikao vya kibiashara na sherehe nyinginezo.

Meneja wa TBL anayeshughulika na Bidhaa za Kimataifa,Consolata Adam alisema, “Kinywaji hiki lazima kizibe pengo la vinywaji visivyo na kilevi na bei yake inakwenda sambamba na vinywaji vingine vilivyopo sokoni.”

Alisema kinywaji hicho kimekuwa kikiuzwa katika sehemu nyingine Duniani na kutokana na hilo,TBL iliona haja ya kukizindua nchini Tanzania.

Consolata aliongeza kuwa Grand Malt ni kinywaji ambacho kinawafaa hata wanywaji wa pombe.

Kwa mujinbu wa meneja huyo, uzinduzi umeanzia Dar es Salaam na utaendelea katika mikoa mingine nchini hivi karibuni.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ni watengenezaji na wauzaji wa bia, vinywaji vya matunda vyenye asili ya kilevi (AFB’s) na visivyo na kilevi ndani ya Tanzania. TBL inazo hisa pia katika Tanzania Distilleries Limited na kampuni shirika, Mountainside Farms Limited.

Bia maarufu za TBL ni pamoja na Safari, Kilimanjaro, Ndovu Special Malt na Castle.
Vinywaji vingine vya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redds Premium Cold.

TBL imo pia katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na imeajiri watu kiasi cha 1,300 huku ikiwa na wawakilishi katika sehemu kubwa na Tanzania na viwanda vitatu vya bia na depot nane kwa ajili ya kusambazia bia na vinywaji vingine vya kampuni hiyo.

Kwa mawasiliano zaidi

Consolata Adam
TBL, Meneja Bidhaa za Kimataifa,
+255 767 266 766,
Consolata.Adam@tz.sabmiller.com

Michael Mukunza,
Executive Solutions Limited,
+255 784 978 302,
m.mukunza@executivesolutions.co.tz
mikemukunza@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Balozi hiyo kitu ina ladha ya asali? Inaelekea ni Bomba sana.
    Kuna wanyamwezi na wasukuma naona wanafurahia kweli kweli hapo Jamilla wa Changamoto na Kakake Victor Willy wa Radio Tumaini.

    Mdau

    ReplyDelete
  2. Ankal, ukipata mualiko mwengine unitumie na mimi nipate kuonja maana juzi ilikuwa HOLSTEN POMEGRANIT, HOLSTEN MANGO, HOLSTEN EPO NA HOLSTEN KOMAMANGA. sasa leo hii ni Ladha gani???? Lazima tushibe mwaka huu. me Harusi yangu karibuni, No alcohol hapa ni mwendo wa Holsten, Grand Malt na mengineyo. ahahahah

    ReplyDelete
  3. hizo ni kama kweli hazina kilevi basi zitakuwa zinadawa ambazo zinawakuza watu waje kuwa walevi baadae , kampuni za bia zinatafuta kila njia kupata wanywaji wengi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...