Timu za kuvuta Kamba Wanawake kutoka ikulu ya Zanzibar(kushoto) na timu kutoka Ikulu ya Tanzania Bara(kulia) wakichuana vikali wakati wa Bonanza maalumu la Pasaka lililofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kilichopo Changombe jijini Dar es Salam leo asubuhi.Katika shindalo hilo timu ya ikulu ya Dar es Salaam iliibuka mshindi. Timu kutoka ikulu ya Zanzibar wakichuana vikali na timu kutoka ikulu ya Dar es Salaam katika mchezo wa kufukuza jogoo.Katika mchuano huo mkali timu kutoka ikulu ya Zanzibar iliibuka kidedea
Wachezaji wa Timu ya kufukuza jogoo kutoka ikulu ya Zanzibar wakiwa wamembeba juu mshindi wa shindalo hilo Bwana Hashim Mohamed Omar wakati wa Bonanza maalumu la pasaka lililofanyika katika viwanja vya Chuo kikuu kishiriki cha elimu (DUCE) kilichopo Changombe jijini Dar es slaam leo asubuhi.
Mkurugenzi wa huduma za ikulu Dar es Salaam Bwana Frank Mganga akimkabidhi zawadi ya kuku mshindi wa mchezo wa kufukuza kuku bi Ziada kombo Hamad kutoka timu ya ikulu ya Zanzibar aliyeibuka kidedea katika shindano hilo wakati wa bonanza maalumu ililifanyika katika viwanja vya DUCE, chang'ombe jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katika bonanza hilo timu Mbili za Ikulu Dar es Salaam na Ikulu Zanzibar zilichuana vikali katika michezo mbalimbali.
Mshambuliaji machachari wa timu ya ikulu Zanzibar Saleh Hamad Mohamed"PATO" akimimina kombora kali kuelekea kwenye goli la ikulu ya Dar es Salaam wakati timu hizo zilipopambana leo asubuhi.Katika mchezo huo timu ya Zanzibar ikulu iliifunga timu ya ya Dar es Salam bao 3---1. Magoli mawili yalifungwa na PATO.
Mlinda mlango wa timu ya ikulu Dar es salaam George Mbilinyi akiokoa moja ya makombora makali yaliyokuwa yanaelekezwa golini kwake wakati wa pambano kali kati ya timu ya ikulu Zanzibar na ikulu ya Dar es Salama leo asubuhi.Pamoja na juhudi hizo timu ya ikulu ar es Salaam ililala bao 3--0 dhidi ya ikulu Zanzibar.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo la pasaka
lililoshirikisha timu kutoka ikulu ya Zanzibar na zile za Tanzania Bara,Mkurugenzi wa Huduma za ikulu Dar es salaam alisema lengo la michezo hiyo ni kukuza mahusiano mazuri kati ya wafanyakazi wa ikulu hizo mbiili, kuimarisha afya za washiriki na kuueanzi muungano wa Zanzibar na Tanganyika kwa njia ya michezo.Jana Timu ya ikulu Zanzibar ilitembelea ikulu ya Dar es Salaam na kupata fursa ya kukutana na Rais Jakaya kikwete na kupiga naye picha ya pamoja.
HAbari na picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu Dar






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Naona kuku wote wan'kwenda Unguja. Mbona nshindi wa Jogoo hawajambeba uzurii?? watam***nua mwenzao.
    Hongereni lakini.

    Mdau

    Ngazi mia
    Unguja.

    ReplyDelete
  2. heko zanzibar uzi huo huo.

    ReplyDelete
  3. its so fun 2read Bongo news, u kno oly in Our country u can find all of super stars.
    We have also Obama, Zinane, 50Cent, Drogba n alot au Mnabisha???
    Simmemuona PATO katiagoli,mbili tena.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...