kuna wadau wameomba kuona taswira hii ya mwaka 2004 wakati ankal na wenzie walipokwenda jimbo la chalinze na JK kukagua athari za mafuriko huko. Nyuma ya ankal ni Jimmy Elias ambaye sasa ni marehemu, Richard Mwaikenda na JK wakati huo akiwa Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. mdomoni mwa anko ni kizibo cha biki sio fegi kama alivyodai mmoja wa wadau walioomba kuona tena taswira hii. hapo ilikuwa kafia mtu...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Ndio Ankal hii picha ni kumbukumbu safi sana nikikumbuka nyumbani fikra napata fikra nyingi sana Mungu amrehem Mwaikenda amuondoshee adhabu ya kabuli
    Nn dau wa Iceland

    ReplyDelete
  2. KWELI MICHUZI UMETOKA MBALI SANA.JITAHIDI UWE MTU WA KUSADIA SANA JAMII/kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa kutoa sana sadaka, NATHAMINI MCHANGO WAKO ILA SEHEMU ULIZOPITA WEWE NI WATU WACHACHE SANA WAMEPITA,una expirience ya pekee kimaisha ilitakiwa uandike kitabu cha maisha yako kama changamoto kwa vijana wengine au watu wengine wajifunze.
    umetoka mbali una stahili kula kuku zako.

    ReplyDelete
  3. umetoka mbali kaka acha ule bata sasa

    ReplyDelete
  4. michuzi kiasi raisi jakaya asikusahau umetoka nae mbali.

    ReplyDelete
  5. ankal ni miaka sita tu ilopita mbona umebadilika sana au maisha tu hayo?

    ReplyDelete
  6. Ankal usitake kutuyeyusha mdomoni ni sigara kali ndo maana ulikuwa na nguvu nyingi za kuongoza libeneke!! hahahaaaaaaa this is funny!lol

    ReplyDelete
  7. Ankal,

    Na JK pia katoka mbali, from kupanda mitumbwi ya kimatumbi to kuingia White House kila mwezi.

    Mungu si Athumani.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  8. anko salute!
    Mi nilikua najua nimtu wa kubabaisha tu,
    kwali duniani hakuna mtu mwembamba.

    ReplyDelete
  9. ungeweza kuwafuta hao jamaa waliokuwa ndani ya maji aisee ni bonge la picha!yaani mngeonekana tu watu mliopanda mtumbwi.safi sanaaa.

    ReplyDelete
  10. Skip lunch siku hizi .....mweee umebadilika sana.....

    ReplyDelete
  11. duh ankal kumbe umetoka mbali na JK wacha akupe shavu tuhh si unajuwa mpende akupendae na kizuri kula na nduguyo? basi wewe kula bata tuh mkuu mmetoka mbali na JK

    ReplyDelete
  12. kaka ankal michuzi hapo nakulabali, JK shavu lamiza akupe tunaelewa mmetoka mbali sana nae usijali ankal mkuu wa nani lazima upe baada ya 2010.

    mdau kitoka holland mafichoni.

    ReplyDelete
  13. Picha nzuri sana!! wote mnatabasamu na wengine wanajivutia bange mnasingizia kifuniko cha kalamu!!! si mbaya...mko porini!!!

    ReplyDelete
  14. Duu niliwahi kuiona hii picha zamani lakini sikujua huyo hapo mbele ni ankal Michizi.

    ReplyDelete
  15. Ankal,
    kama wewe ulikuwa unapiga kasia, nani kapiga picha hii???

    ReplyDelete
  16. Kuuumbe!?nilikuwa najiuliza kwa nini tangu JK aingie madarakani michuzi mambo yake yanaenda mstari tu.Sasa nimepata jibu.Just kidding!ha ha ha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...