Haya, leo tumesikia kuwa tutatozwa hela kwa ajili ya 'carry on' bag kwenye Spirit Airlines. Mjue na airlines zingine zitaiga! Haya sasa nao Ryan Air wanasema utatozwa hela kutumia choo kwenye ndege! Jamani, sasa kama mtu kambanwa, ndo akae nayo mpaka ndege itue! Hii sasa ni uchu wa pesa!

Kwa habari zaidi:
http://www.cnn.com/2010/TRAVEL/04/07/
ryanair.lavatory.fee/index.html?hpt=T2

http://www.latimes.com/business/
la-fi-spirit7-2010apr07,0,5945292.story?track=rss

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Amerika tambarare.


    Hawa jamaa wanakusafirisha from Fort Lauderdale (Florida) mpaka Jamaica ama Peru kwa $30, bora wangeongeza nauli kuliko kuambiwa ulipe kwenda msalani.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  2. poa tu tutakuwa tunaingia na chupa za kukojolea..kasheshe iko kwenye number 2 ila tutapata ufumbuzi temporarily diaper might be an option

    ReplyDelete
  3. Tatito ni kuwa ndege hizi zabeba abiria wengi maskini kama ndio target customers (budget airline) ambao kwenda chooni kunatisha.

    Budget Airline yoyote ukiwauliza watakwambia tatizo liko chooni ikiwa ni pamoja na uchafunzi wa vyoo.Kila mtu akitoka inabidi mhudumu ukachungulie kama hajanya au kukojoa pembeni.

    Wakiingia tu ni chooni sasa ukiweka fee watajibana hadi itue.Maana hela hela za kulipia choo au wanabahilia.

    Ni strategy ya kudhibiti unyaji na ukojoaji ovyo unaotokana na ulaji ovyo na unywaji hovyo wa maskini kabla hawajapanda ndege hizo za dezo.

    ReplyDelete
  4. na hawa air canada nao wana visa ati wanauza microphone dola 3 wakati ndege nyingine wagawa bureeeee kama huna ndio utajiju utabaki kuangalia cinema kibubububu na miziki ndo holaa yani huku ni kukwibiana kimtimndo tu hamna lolote

    ReplyDelete
  5. hayondio matatizo ya ndege za bei rahisi pandeni ndege za uhakika mwishowe mtaambiwa mlipie hadi sehemu yakuweka mzigo

    ReplyDelete
  6. hello Michuzi
    Nimejaribu sana kukutumia email unitundikie Article yangu inayohusu Governance stytem In Tz need to be changed lakini u have been ignoring me i dont in what reason, may be naanza kuhisi kuna ufisadi au una ajenda na CCM.
    Naomba tena refers to your email box nitundikie hiyo Article.
    Tafadhali itundike
    Mdau USA

    ReplyDelete
  7. Usishangae, baadaye mwenye mimba akaambiwa alipe nauli ya watu wawili.

    Na wala si uchu wa fedha peke yake, hizi dizo zile dalili zilizosemwa za Mwana wa Adamu kuja. "Watu watapenda sana pesa, Upendo wa wengi utapoa, Vita na machafuko mahali mahali duniani. Na haya yote tunayashuhudia siku hizi; watu kujitoa mhanga ni kitu cha kawaida. Mauaji holela!!!
    Watu hawana hofu ya Mungu tena siku; ushahidi ni hapo mwanadamu anapomchaanga mwanadamu mwenzake vipande vipande kwa kisingizio cha kupata utajiri - tunashuhudia ndugu zetu walemavu wa ngozi jinsi wanavyouawa. Hakuna hofu tena ya Mungu.

    Ndugu zangu, tujirekebishe na kuwa tayari kumrudia Mungu. Tuokoke, japokuwa wapo wachache wanaotumia kinga ya wokovu huku wakifanya uharamia. Lakini, kama ukiokoka na kumaanisha moyoni kwa dhamiri na kunia, dhamira yako itakusuta, hutathubutu kufanya mambo mabaya, ambayo ni kinyume na WOKOVU.

    Bwana atusaidie sote, hasa wewe unayesoma ujumbe huu, Mungu akusaidie kutafakari haya na akupe neema ya kuona kiroho hizi dalili za kuja kwake Mtarajia, kuja kuchukuwa wateule wake.

    Fuatisha sala hii kwa kumaanisha: BWANA YESU, NATAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI. TENA NIMEKUKOSA MARA NYINGI. NATUBU MBELE YAKO NA KUACHA KUTENDA DHAMBI KWA KUMAANISHA KUZIACHA KABISA. BWANA YESU, NAOMBA UNISAMEHE MAKOSA YANGU YOTE. ASANTE YESU KWA KUNISAMEHE, NA KUNIOKOA, KATIKA JINA LA YESU. AMEN

    Bwana mwaminifu juu ya ahadi zake. ujue amekusamehe sawasawa na ahadi zake katika JINA LA YESU, Amen.

    ReplyDelete
  8. Na ukiwa na tumbo kubwa pia utaambiwa ulipe nauli ya watu wawili! Hivyo wenye vitambi angalieni itakuja kuwacost kama mkitaka kusafiri ma ndege za siku hizi....Tunakoelekea....mmmh...kubaya....

    ReplyDelete
  9. Mdau anon 07:47 AM umechangia vizuri ila usiwaite hao jamaa maskini sema watu wenye kipato kidogo. Kwa vile wanamudu kusafiri kwa kutumia ndege na wanalala kwenye hoteli za bei nafuu.

    Maskini ni mtu ambaye hana uhakika wa kupata mlo wake wa siku, malazi ya shida na hawezi kumudu gharama za matibabu. So you talk of someone ambaye hana pesa kabisa.

    ReplyDelete
  10. MLIFIKIRIA WENYE NJAA NI ATC TU.

    ReplyDelete
  11. well, Nadhani hakuna tatizo hapa kama mukifuatilia kwandani kwanini wanafanya hivyo tena mutakubali kwamba bora wafanye hivyo:-
    THINK. Air Line zote hucharge abiria wote bei sawa katika assumption kwamba utapakia mzigo kwenye boot na ndani, utajisaidia, utakula na kunya, pia utajisaidia.

    Ryan air wao: wanasema kwanini utozwe service ambazo hutozitaka? ndio maana wao kuna bei katika kila kitu na pale ambapo hutakula, or kunywa, or kubeba mzigo or ANY then bei yako lazima ipungue kwani wewe hujazitumia hizo service kwanini wakutoze?

    Ndio maana katika bei zao zinaonekana cheaper, na sio sawa kwa kila mtu.

    tufuatilie mambo kabla hatujashika mchawi kwani eleimu ni nafuu kuliko ujinga. JAZBA haijengi!

    G7
    Bongo

    ReplyDelete
  12. mdau wa Thu Apr 08, 07:47:00 AM, hizi airline hazibebi masikini peke yao. ni kweli ni budget airline lakini pia watu wengi wakifikwa na shida na hawawezi kupata ticket za airline nyengine huwa wanapanda hizi.

    Sitaki kufanya fahari lakini naweka point tu kuwa nishawahi kumuona Ian wright, shearer na lineker wakipanda easy jet luton mwaka jana katika nyakati tafauti wakati ule nikipiga boksi customer service pale uwanja wa ndege. Pia wafanya kazi wenzangu pale walishasema mara nyingi kuwa maselebrity wengi hutuma easy jet pale luton hasa kwa kwenda kucheza golf na kurudi siku hiyo hiyo.

    ReplyDelete
  13. well, Nadhani hakuna tatizo hapa kama mukifuatilia kwandani kwanini wanafanya hivyo tena mutakubali kwamba bora wafanye hivyo:-
    THINK. Air Line zote hucharge abiria wote bei sawa katika assumption kwamba utapakia mzigo kwenye boot na ndani, utajisaidia, utakula na kunya, pia utajisaidia.

    Ryan air wao: wanasema kwanini utozwe service ambazo hutozitaka? ndio maana wao kuna bei katika kila kitu na pale ambapo hutakula, or kunywa, or kubeba mzigo or ANY then bei yako lazima ipungue kwani wewe hujazitumia hizo service kwanini wakutoze?

    Ndio maana katika bei zao zinaonekana cheaper, na sio sawa kwa kila mtu.

    tufuatilie mambo kabla hatujashika mchawi kwani eleimu ni nafuu kuliko ujinga. JAZBA haijengi!

    G7
    Bongo

    ReplyDelete
  14. JAMANI SI MTEMBEEEE KAMA USA AU PARIS KARIBUU MNAPIGA KELELEEE WABONGO BWANAAA WE UNAENDA PANDA NDEGE AU UNAENDA KUNYA,MUDA SI MREFU MTACHAJIWA OXYGEN

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...