wachezaji wa simba wakifurahia kombe lao leo.
Picha zaidi nenda kwa Father Kidevu
Mfungaji bora Mussa Hassan Mgosi wa Simba akiwa
na jezi ya Yanga inayoonesha idadi ya magli aliyofunga ligi hii ya Vodacom

Mwenyekiti wa Simba Mzee Hassan Dalali gego nje na vidole vinne juu
Kipa wa Yanga akikubali
Wapenzi wa Simba meno nje leo

YANGA WAPATA PENATI BAADA YA KIPA WA SIMBA
JUMA KASEJA KUFANYA MADHAMBI LANGONI PAKE.
GERRY TEGETE ANAPIGA PENATI HIYO...
GOOOOOAAAAALLL!
BAO NI 3-3 SASA...
------------------------
GOOOOAAAAAALLL!
DAKIKA MBILI BAADAYE SIMBA WANAPATA BAO LA 4
NI ECHESA ANAPIGA BAO YANGA...

BAO SASA NI SIMBA 4 YANGA 3...
---------------
MCHEZO UNAANZA KUHARIBIKA DAKIKA HIZI ZA LALA SALAMA.
KIPA JUMA KASEJA KAPIGWA DALUGA NA ANAGALAGALA UWANJANI.
MPIRA UMESIMAMA KWA MUDA, WAKATI KASEJA AKIHUDUMIWA.
KIPA WA AKIBA DEO DIDA ANATROTI KULEEEE..
PIA KUNA MSHABIKI WA YANGA AMEZIRAI KWA PRESHA.
-----------------------------
MPIRA UMEKWISHA!!
SIMBA WASHINDI KWA BAO 4 DHIDI YA YANGA 3
SIMBA AMBAO NDIO MABINGWA WANAONDOKA UWANJANI WAKIWA NA FURAHA KWA KUHITIMISHA LIGI KUU WAKIWA NA KOMBE PAMOJA NA USHINDI DHIDI YA WATANI WAO WA JADI.
NA LEO LEO WANAKABIDHIWA KOMBE LAO UWANJANI
------------------------
SHABIKI WA YANGA ALIYEZIMIA KWA PRESHA ANAZINDUKA WAKATI KIPYENGA CHA MWISHO KINALIA. ANAPOAMBIWA YANGA KAPIGWA 4 ANAZIMIA TENA. MSHIKEMSHIKE WA KUMPEPEA UNAENDELEA WAKATI TUNAENDA HEWANI...




































Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mambo gani tena watani....

    ReplyDelete
  2. aksante michu kwa kutuhabarisha ongera mnyama kama kawaida yako

    ReplyDelete
  3. safi sana msimbazi,leo jumapili lkn itanibidi hata ninywe bia mbili kujipongeza

    ReplyDelete
  4. yanga kama arsenal vile jamaani timu yangu mtoeni Dalali haache kuwanga kwenye timu mambo ya znz hayo si manajua tene

    ReplyDelete
  5. David VillaApril 18, 2010

    Vibaka walikuwa wanawapora wazungu(watalii?) waliokuja kushuhudia mechi "vitu" vyao(hasa camera) live kweupeee baada ya mchezo kumalizika barabarani,polisi sijui walikuwa wapi.Watasha hao walikuwa wanatembea kwa miguu kuelekea keko karibu na chuo kikuu cha ualimu(DUCE)!!!Aibu hey?

    ReplyDelete
  6. HONGERA WANA LUNYASI, WANA SSC, KWA KUDUMISHA UTAMADUNI WA SOKA LA TANZANIA!!!
    KWA HALI ZOTE SSC NDILO CHAMA LA UHAKIKA LENYE SOKA LA HALI YA JUU KULIKO SIJUI NINI HAPO TZ.
    KANDAMBILI HUWA WANABAHATISHA BAHATISHA TU KUCHUKUA UBINGWA, HATA MIZENGWE HUWA MIIINGI ILI WAPEWE USHINDI.
    IWE IWAVYO, HATA KAMA TUKO HUKU MBAALI NA NYUMBANI, BADO WATANZANIA SOTE TUNAJUMUIKA NANYI KUSHEREHEKEA USHINDI WA MABINGWA WETU SSC, TUNASHUHUDIA WAKIWEKA HISTORIA NYINGINE MPYA YA KUTWAA UBINGWA BILA KUPOTEZA MCHEZO, ZURI ZAIDI KUPATA USHINDI WA BACK TO BACK DHIDI YA KANDAMBILI!!
    HIP HIP...HUREEEEEE!!!
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  7. HUU NI WAKATI AMBAO YANGA INA DEFENCE DHAIFU NADHANI KULIKO WAKATI WOWOTE. PIA NIDHAMU YA WACHEZAJI INA UTATA

    ReplyDelete
  8. hii inakuwa mbaya zaidi pale shabiki namba 1 wa arsenal na yanga damuni. sijui ni usiku ulioje leo..hlf upande wapili man utd 4eva na simba chama

    ReplyDelete
  9. Michuz yule jamaa hakutupwa jukwaani, bali alizi100 baada ya furaha ya yanga kusawazisha. Nilimwaonea huruma maana alipozinduka alikuta Simba wanakimbia huku na kule wakiwa na kombe mkononi alipouliza matokeo akaambiwa Simba 4-3 Yanga jamaa akazi100 tena!

    ReplyDelete
  10. Go Simba!!!!! Go Simba!!!!!

    Yanga should learn from their mistakes... Utapigaje kambi kwenye hotel mjini? LOL

    Go Simba!!!!! Go Simba!!!!!

    ReplyDelete
  11. Hongera Simba, yaani Yanga ndie amekutana na hasira ya Simba- wewe unamfwata Simba wakati ameshawinda anakula( eti nikatie kitoweo chake changa) hasira zake ameziona leo.
    2. Alafu hata Phiri, hakuona sababu ya kuwepo-alishamaliza kazi yake akawaambia vijana- nguruma, rarua , ngata ngata!
    Tunatoa pongezi kwa Wachezaji, Phiri na makocha wasaidizi, viongozi wote, sisi wanachama, friends of Simba na manazi wote wa Simba popote duniani, kwa kutupa raha mwaka huu.
    Mwaka ujao tunataka vikombe vya ndani na nje NAKUMBUKA, sasa tunataka uwanja wetu!
    Kampuni
    Norway

    ReplyDelete
  12. Werah werah! Aibu yao aibu ye2. Simba bingwa. Tena ubingwa umekua mtamu kwa kumfunga mtani. Mashaka Penza upo juu.

    ReplyDelete
  13. wakati sisi tunajifua znz wao walimualika mama karume aje kuwaombea dua! kama hiyo haitoshi wakacha kambi wakasafiri tena mpaka znz kwenda kuombewa tena dua!hili ndio tatizo la timu kuongozwa na mawakili wasio na rekodi za kushinda kesi! hata mbinu za soka hawajui. mpira kwao unachezwa magazetini na redioni tuu, sijui lini mtajifunza mbinu za soka nyinyi watu! kwa miaka kumi sasa mmeshinda mechi moja tuu kwenye ligi? p....f!

    mzaramo

    ReplyDelete
  14. angalia link hii hbr ya flaiviana matata


    http://bossip.com/238971/who-is-choppin-this-thang-down/#more-238971

    ReplyDelete
  15. Wadau mmeona rasmi tofauti ya timu inayocheza soka la kitabuni na timu inayocheza soka la magazetini.
    Kabla ya mechi kelele zilikuwa nyingi sana za timu iliyopania kuchafua hali ya hewa kwenye sherehe za mabingwa. Watu wakatamba sana kwamba toka awamu ya pili ya ligi ianze wameshinda mechi zote. Panapo kweli uongo hujitenga.
    Poleni watani. Wakati mnajiuliza sisi tutakuwa bize tukiwakilisha taifa la Tanzania kwenye soka la kimataifa.

    ReplyDelete
  16. Ha ha ha, ho ho ho..."mzaramu" wa 9:48 umenichekesha sana na umesema ukweli: kuombewa dua na mama Krume hakutainua kiwango chao cha kabumbu!!!! ha ha...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...