Kaka michuzi,
pole na mjukumu ya kutuletea habari. Usiweke email yangu tafadhali. Jana nilipanda DAR EXPRESS gari no T666AXL kutoka arusha kuja Dar. Ilipofika kibaha maili moja ikazima engine. Tukashuka chini mara tukamuona dreva kachukua ndoo anakwenda kutafuta mafuta. Sasa nikajiuliza mwenye gari huenda hayajui haya yanayotokea, ambayo ndio yanayofukuza wateja maana tulisubiri zaidi ya nusu saa.
Tunaacha magari mengine tunapanda yake sababu tunajua yanajali mteja lakini kumbe kuna uswahili ushaingia. Ushauri wangu wa bure; Wamiliki wanaojali huduma zao waweke namba zao za simu kwenye ticket ili tuwapigie tulalamike. Ndio maana mie nachelewa kukubali kuwa JK ni kiongozi mbovu. wenye matatizo siku zote ni watendaji huku chini. Mwenye gari wala hajui hili. -
Msafiri wa Dar Express

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2010

    JK ANAKUJAJE HAPA NA GARI ZA DAR EXPRESS, AU UNATAKA KUSEMA LINGINE TU JUU YA JK, IT IS UTTERLY AND ABSOLUTELY NON-SENSICAL TO INCLUDE JK HERE. KAMA CCM WAMEKULOGA USITULETEE HAPA, KUNYWA MAJI BENDERA UVIMBIWE

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2010

    ANON 24/MAY 08:27 PM PUNGUZA JAZBA, MWENZIO KATOA MFANO,SOMA VIZURI,ANASEMA HAWA WATU WA CHINI KAMA HUYU DEREVA WA DAR EXPRESS NDIO WAHARIBIFU SIO MKUU WAO/BOSS KAMA VILE WATU WANAVYOMLAUMU JK KUMBE WATU WA CHINI YAKE NDIO WAHARIBIFU,READ BETWEEN THE LINE NDG ACHA JAZBA

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2010

    Mwenye mabasi ni mzee Mremi. Nina uhakika kabisa hajui jambo hili; unfortunately, akijua tu, dereva hatakuwa na kazi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2010

    In fwact hizi jazba ni very interesting. Nashindwa kuelewa huyo bwana anayewaka hapo juu anahitaji msaada wa kisaikolojia ama vipi? Katika mazingira ya kawaida huwezi kukurupuka na kufoka tu namna hiyo, is it the economics or econometrix boiling you live again????

    Mdau mtoa mada, pole sana. Mimi na abiria wenzangu tulipatwa na kero ya ajabu ambayo sitakaa niisahau milele katika basi la TAWFIQ kutoka Dar kwenda mitaa ya Shinyanga. Sitakaa nisahau maisha yangu yooootteeee, yaani hayo mabasi kwangu ni FORGET.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2010

    "KWA BWANA YESU KILA GOTI LITAPIGWA"
    Mdau.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2010

    I second u mdau wa kwanza. Mimi sio ccm lakini kuna mambo mengine yakufikiria kabla hatujaweka viongozi wetu. Jk na private sectors inamuhusu nini? Kama ni uwajibikaji ianhitaji competition ukiona hakuna customer service nzuri achana na hilo shirika business yako ipeleke kwingine. Wewe unataka kuniambia dereva alikunya hiyo gas au mwajiri au meneja anawapa gari bila kuangalia gas inahitajika kiasi gani?

    Dereva hana kosa kwanza huyo ni dereva mzuri ni mwingine au wa huku angekaa chini na kuita wakubwa wake waje wailete hio gas kwa vile yeye sio kazi yake . kazi yake nikupeleka gari salama kutoka point a to point B.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 25, 2010

    SASA SIJUE UNA MAANA GANI ?
    KAMA DEREVA WAKO ANAFANYA VITU KAMA HIVYO KUNA SHERIA ZA MWAAJRI AU MKATABA WA KAZI KWA UNAMPA WARNING NA HAKIRUDIA TENA UNAMFUKUZA KAZI. KWA JK KAMA KUNA WATU WA CHINI YAKE NDIO WAHARIBIFU KUNA SHERIA SERIKALI AU JK MWENYEWE ANAWEZA KUWAFUKUZA SIO KUNYAMA KIMYA AU WATU WANAMDANYA KWA KUMPA DATA ZA UONGO.... MFANO KIONGOZI YOYOTE KAMA OFISI YAKE AU WATU WA CHINI YAKE HAWAFANYI KAMA UNAVYOTAKA HATA KAMA NI RAFIKI YAKO ...KWA FAIDA YAKO NI LAZIMA UWAFUKUZISHE AU WATAKUFUKUZISHA AUM KUUWA COMPANY YAKO KWA MASILIA YAO BINASFI...

    NDIO WAHARIBIFU SIO MKUU WAO/BOSS KAMA VILE WATU WANAVYOMLAUMU JK KUMBE ,READ BETWEEN THE LINE NDG ACHA JAZBA

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 25, 2010

    Yule aliyekuja na jazba masikini tumpe pole hajui kitu. Mwenzie alitoa mfano tu ili somo liingie vizuri. Bahati mbaya huyo kijazba hajaenda shule tumuache alivyo. Ila mabasi ya Dar Expess kwa kweli madereva wake wajiangalie. Mimi tarehe 19.4.2010 niliondoka na basi la Dar EXPRESS. kwenda arusha, kwa kweli dereva wake alitupeleka roho juu. Dreva mwenyewe alikuwa kama kijana mdogo mdogo, alifukuzana na basi la kilimanjaro express ambalo lilikuwa halina abiria mpaka moshi. Watu walipolalamika tukaambiwa kuwa tajiri anamwamini sana dereva yule na mkilalamika hatamfanya kitu. Ikabidi tuanze kuomba Mungu na tulisikilizwa tukafika salama. Ila wajitahidi kuwa makini mabasi yao tunayapenda.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 25, 2010

    He! Tumegee mwenzetu TAWFIQ ilikufanyaje? nasi tusijeingia kwenye mtego! Mabasi mengine bwana. Hawa matajiri wangekuwa kila safari ya basi wanawaweka watoto wao ajali zisingekuwapo. maana wasingependa wafe kwenye ajali. Sasa cha kushangaza tajiri anampangia dereva wake muda wa kufika, halafi si muda wa kuridhisha kusema labda ataenda na mwendo wa wastani.
    Hapa hata serikali ikiingilia itashindwa kwa vile mabasi mengi ni ya wakubwa

    ReplyDelete
  10. kaka hilo gari lenye hiyo namba lina matatizo sana...kuna siku huyo dereva aliovertake mara mbili nusura asababishe ajali....dada mmoja akamwambia dereva aendeshe gari vizuri...basi dereva akanuna halafu akazira hata kukiwa na lorry mbele yake haovertake akawa anaendesha 30km/hr....mimi nimeikariri na nikikuta ndio hiyo huwa sipandi....

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 25, 2010

    Kweli kabisa. Bora Mwenye basi la Dar Express ajue kuna mambo ya ajabu sana anayofanyiwa katika biashara yake hiyo. Mimi yalinipata siku hiyo nilikuwa nasafiri kwenda Moshi. Kabla hatujafika Segera mara Dereva aliyetutoa Dar kampa utingo wake gari. Utingo huyo karibu atumwage wote kwani yeye alijua kukanyaga mafuta tu lakini ku-control gari alikuwa hajaweza.Nao walitegea wakati watu wengi wamesinzia ndipo wakabadilishana. BORA RISITI ZIWEKWE current Tel no ili tuweze kumpigia mzee Mremi mwenye wakati wa tukio la ajabu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 25, 2010

    kwa kweli mabasi ya muda mrefu na kwa kiasi ni salama ni RAHA LEO. ni vema aanze na safari za Arusha.dar exp pia ndani wanaruhusu hata sio wasafiri kuingia ndani na kuibiwa ukilalamika wanakuwa wakali. mojawapo ya usafiri bora ni pamoja na usalama wa mizigo.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 25, 2010

    Wakuu, hawa wafanyakazi wa Dar express wanakiburi sio madereva tuu hata wakatisha tiketi..mimi nimeacha kupanda hayo magari toka mwaka juzi, baada ya kwenda kukata tiketi na kumkuta dada mkatisha tiketi akiongea na simu ya binafsi, nikasimama dirishani kama 20minutes bila yeye kunisemesha hadi alipomaliza kuzungumza na simu yake ndipo akaniambia mabasi yamejaa..sikurudi tena dar express na wala huwa simshauri mtu kupanda hayo mabasi unless hakuna altenative.

    ReplyDelete
  14. Jaymes BongMay 25, 2010

    Huyo dereva ambaye anon wa May 25th 7:43am anasema - jamaa mdogo mdogo hivi. Anajulikana sana. Yeye ndiye dereva wa T666 AXL. Dar Express nimepanda mara kadhaa na hio T666 AXL kwa bahati nzuri/mbaya nimeipanda mara 4.
    Yule dereva mdogo sio mchezo. Ni mzuri ila wakifika sehem za "kuchimba dawa" anatoa msokoto mkubwa wa bhangi na kuvuta.
    Nilishampiga picha mara kma tatu hivi.
    Dar Express wana service nzuri ila sometimes wafanyakazi wengine wanaagusha jina nzuri la Mzee Mremi.

    I will still take Dar Express because i like it lakini huyo dereva dah !!!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 25, 2010

    Dar express imekuwa ni tatizo lao la kawaida siku hizi, mimi ni mtumiaji mzuri wa mabasi yao na tatizo kama hilo limeshanikuta mara mbili, ya kwanza ilikuwa Chalinze na ya pili ilikuwa kwenye kona ya kuingia stendi ya Ubungo na kusababisha foleni kubwa, hivyo sishangai

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 25, 2010

    gari yenyewe ina namba za shetani 666

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 25, 2010

    SEMENI MTAKAYOYASEMA, LAKINI UKWELI NI KWAMBA DAR EXPRESS NDIO KAMPUNI PEKEE YA KUAMINIKA HAPA NCHINI KUHUSIANA NA MAMBO YA USAFIRI. GARI KUHARIBIKA NI KAWAIDA, NA WALA SISHANGAI. NIMESAFIRI SANA DAR ARUSHA DAR NA HUWEZI KUNIAMBIA NISAFIRI NA USAFIRI MWINGINE ZAIDI YA DAR EXPRESS. UDUMU MZEE MREMI NA POLE KWA KIFO CHA MKE WAKO HIVI KARIBUNI.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 25, 2010

    Mwe Mwe mwe!!!! Umenigusa MOYO wangu. Hilo basi la Dar Exp jamani madereva wake na utingo wao ni very hopeless!!. Nakumbuka siku moja nilipanda nikiwa natokea Dar kwenda Arusha na mtoto wangu mchanga nikapanda hilo basi lao "So Called Luxury". Kama kawa nikabeba kapu langu zuri la kupendeza nikaweaka vitu e.g chupa za chai na vitu mbali mbali kwa ajili ya kunisaidia mimi na mtoto safarini nikaweka pembeni mwa fridge kwani nilikaa just nyuma ya dereva. Tulipofika Mombo yaani baada ya watu kula Konda akaniambia hilo kapu weka miguuni kwako. Nikamwambia hivi nimempakata mtoto nitachoka sana naomba hilo kapu likae hapo. Akaniambia tena mbele ya abiria wenzangu nimekwambia toa "HIYO TAKA TAKA HAPO!!!!!" Sio siri niliumia sana moyoni, nikasikia kudhalilishwa na dereva aliskia hakutaka kununua ugonvi akatulia kimya. MIE TOKEA SIKU HIYO MABASI YA DAR EXP YAMENITUMBUKIA NYONGO kwa kauli zao na Customer Care yao MBOVU KABISA. "NI KWA NEEMA TU"

    dissapointed - Nanyori.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 25, 2010

    Pole sana mdau,lakini mimi ninalo moja la kuchangia,unajua sisi wabongo kama si wote basi ni asilimia nyingi,tunafanya vitu vyetu kwa mazoea kama si ushabiki,kwanini nasema hivi,yaliyowapata wewe na na wasafiri wenzako ndio yalikuwa yanatokea wakati wa enzi za Scandinavian, yametokea kwa Makampuni kama Mohamed Trans na kadhalika,lakini ukichunguza kwa makini nini sababu ya haya yote,ni mazoea au kwa lugha ya wazi un professional way of doing things,sidhani kama Mzee Mremi amewekeza vya kutosha katika utawala wa biashara yake kama ambavyo tunategemea kuwa,na simuombei mabaya,lakini naona mwanzo mbaya wa mabaya kuipata kampuni yake,kama kuna anayebisha awaulize watu nini kilitokea wakati ule Scandinavia inawika na kutamba si Tanzania tu,bali East Africa Yote.
    Sasa labda niseme tu waTz,tujipange na tubadilike,bila hivyo tutakuwa ni wa kufanya mambo yetu hovyo kila siku.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 25, 2010

    Wachangiaji wengi naona nyie si wasafiri wa mabasi ya Dar Express na mengineyo. Je kampuni hii unaweza kuilinganisha na ipi hapa Bongo? Msilaumu tuu, ila DAR EXPRESS IS THE DEVIL WE KNOW, AND NOT THE ANGELS WE DO NOT KNOW

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 25, 2010

    Nashukuru sana kwa maoni ya wadau.Mi nafikiri tukitafute chanzo cha huduma mbovu kwa wateja zinazotolewa na wahudumu wa vyombo vya usafiri pote nchini.Je ni mara ngapi walishapelekwa na matajiri zao kozi fupi za huduma kwa wateja?,tatizo liko kwa matajiri wanachojau wao ni kuwatuma pesa wafanyakazi wao,na si vinginevyo.Ndiyo maana utawakuta wanasema "Tumetumwa pesa bwana..."hivyo tuwashauri majiri wazingatie mafunzo ni mhimu sana,yote haya wataisha menyewe.

    ReplyDelete
  22. nimesoma mawazo ya wadau wote hapa,

    ukweli ni kwamba dar express ana jina zuri sana na usafiri wake ni wa hakika, ila sisi wateja wake tusiposema ukweli atapoteza wateja wake wote,

    mi ni abiria mzuri sana wa hili basi, ila nina kero moja kubwa sana, juzi jumapili(23/05/10) nilipanda dar express lile la 28000/= air condition class, i think hili basi lilikua T 663 ...,
    nikiwa natoka moshi kuja dar, ni nnilikaa siti i kwenye namba 40 something, hili basi lilikua linaharufu ya mkojo sana, na harufu hii ilitukera sana kwa kweli, naomba mwenye basi alifanyie usafi makini,
    kitu kingine, tuliomba tuwekewe walau CD ili tuangalie si wajua tena ukiwa unaangalia movie safari huwa inakua fupi, ila cha ajabu niliambiwa deki ni chafu, na hii sio mara ya kwanza kuambiwa kuwa deki safi( toen hizo screen kwenye magari yenu kama hazifanyi kazi),

    nimesema haya kwa kuwa napenda sana kuendelea kusafiri kwa kutumia dar express, na hii ndo njia pekee ya kumfikishia mkubwa taarifa.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 25, 2010

    I AM ABSOLUTELY WITH MDAU NAMBA ONE HAPO JUU. JK AMEKUJAJE HAPA? SI KAMA ALITAKA KUELEZA JINSI GANI ANAMFAGILIA JK, KIINI CHA MAADA HAKINA UHUSIANO WOWOTE NA JK. THAT IS A PRIVATE SECTOR, PRIVATE ENTITY IT HAS NOTHING TO DO WITH JK OR THE GOVERNMENT HE LEADS. HAMNA HATA SEHEMU MOJA JK INAMHUSU. HATA UKISOMAJE HIYO MAANA KIUNDANI, BETWEEN THE LINES, HAINA UHUSIANO WOWOTE NA JK. KUNA HAPO JUU MTU ANASEMA MDAU NAMBA ONE HAJUU HAJASOMA, KWA MAONI YANGU MTOWA MAADA NDO AMETUMBUKIZA KITU KISICHOHUSIKA HAPO. I WOULD AGREE WITH HIM IF IT WAS ABOUT SOMETHING TO DO WITH ROADS, TRAFFIC POLICE AND THE LIKE, ANYTHING TO DO WITH THE GOVERNMENT IN RELATION TO TRASPORTATION SYSTEM, BUT NOT OTHERWISE. AENDELEE KUNYWA MAJI YA BENDERA YA CCM AVIMBIWE, IT IS TIME NOW TO CALL BLUE BLUE, NOT BLUE RED

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 25, 2010

    mie nliyeleta mada nawashkuru kwa kuiona hii. wenzetu wakenya hawako hivi, watatushinda mpaka lini kwa customer care na kesho kutwa wanakuja kwa wingi. dreva wetu alikua anaendesha gari huku anaongea na brathamen wake anakunywa grants mwanzo mpaka mwisho wa safari. Ethics hakuna kabisa. mijitu mingine inacomment haina uzalendo kabisa, yaani khaa imenichosha. kama mmiliki haweki namba yake najua hajapata ujumbe huu na nitajipandia buffalo langu bas yaishe.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 25, 2010

    Jibu kwa mdau Tue May 25, 07:50:00AM na angalizo kwa wadau wengine wote kuhusu mabasi ya TAWFIQ:

    1. Waliniuzia tiketi hewa, hivyo nililazimika kukalia kagodoro kutoka Ubungo hadi Kahama.

    2. Nilipolalamika kuwa nimechoka sana na ninahitaji siti mtu anayefuatia akishuka wakanifokea wakisema zimeshauzwa na nisilete mdomo ama watanidunda.

    3. Tulipofika Dodoma basi ilijaza kuliko maelezo na trafiki akapewa chake na kututakia safari njema.

    4. Spidi ilikuwa ya kiama.
    Tulipofika karibu na Manyoni ikakata spring, jamaa wakaikokota taratibu taratibu na tukakesha Manyoni hadi mida ya saa 4 asubuhi kesho yake.

    5. Njia nzima walikuwa wanaongeza mafuta kwa vibaba (ya kununua kwenye ndoo).

    6. Ilituchukua siku nzima kusafiri kutoka Manyoni hadi Nzega (hivyo tukalala tena Nzega). Wakati wote huo wafanyakazi walikuwa wakitumia lugha chafu na vitisho kwa abiria waliohoji kuhusu mambo mbalimbali (ikiwemo kuwatishia kuwashusha watu waliokuwa wakisafiri na famila zao).

    7. Tulipofika Nzega nikaongoza jopo la abiria wenzangu kwenda kutoa tathmini ya safari yetu yote kituo cha polisi, ila cha ajabu tulikuta wafanyakazi wa basi wakiondoka polisi (walituwahi kwenda kuweka mambo sawa).

    8. Tulipotoa taarifa yetu tukaambiwa tutimue kwani hazina mantiki, eti ni basi la kuaminika na wao wanalijua vema.

    9. Mdau nikagoma na kuanzisha bonge la zogo hadi OCD akaamka na kuja kujua kuna nini. Tukamueleza hali halisi na akaongoza msafara kwenda stendi kuwapa mkwara wa nguvu hao wafanyakazi wa hilo basi. Cha kustaajabisha OCD akatunong'oneza kuwa mob justice sio mbaya sana (yaani tuwafanyizie kama vipi).

    10. Anyway, mkwara wa OCD haukusadia kitu, maana baada ya OCD kuondoka jamaa wakajitapa tapa sana na kesho yake wakatupelekesha vile vile hadi Kahama.

    11. Hivyo ilituchukua siku mbili kufika Kahama katika hali ngumu na inayokinaisha na kukasirisha sana.

    12. Abiria wengine waliendelea na safari kuelekea mitaa ya Bukoba (sijui safari yao ilikuwaje).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...