Ankal,
Maoni yangu ni kwamba naomba mfuatilie na Kutuletea taswira ya Kipande cha barabara ya Kilwa road maeneo kati ya Zakhem na kituni rangi tatu ambacho ni kero kero kero kubwa mpaka kinaleta foreni kubwa sana toka barabara kwisha na kukabiziwa kwa serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania. Kumekuwa na foreni ya usumbufu mkubwa sana na mpaka abiria wanabidi washukie zakhem na kutembea kwa miguu mpaka rangi tatu kituoni au mpaka kituo cha kilungule.

Kwa kumbukumbu zangu kama sikosei wakati ule wa mlipuko wa mabomu ya kule mbagala aliwaambia watu wajenzi wa barabara ile ya kilwa road na akaamulu mtu aliyekagua kurudia upya katika kuboresha ujenzi. Serikali wako wapi???????????

MAONI YA PILI
Hebu tuweke taswira na taarifa za watangazaji hawa wafuatao:
1. Julias Nyaisangah-Radio One
2. Rose Chitala-Radio One
3. Abdala Hussein- Radion One
4. Basil Mbakile- Sahara Communication
5. Swedi Mwinyi- TBC

Kazi njema na endelea kuendeleza lbene letu la kidunia
Mdau Chef Haruna

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2010

    Serikali wako wapi???????????
    We vipi wewe unataka serikali ya nini? Bila serikali huwezi kuishi? Jisaidie kabla ya kusidiwa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2010

    sasa ukishawekewa taswira za hao uliowataja ndio itakusaidia nini wewe katika maisha yako ya baadae? infact itatusaidia nini sote tunaotembelea blog hii?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2010

    Mmmh bado tu hujaelewa matumizi ya "r" na "l"?... Ni foreni au foleni? au na wewe umetoka kule kwa akina iwe?

    ReplyDelete
  4. ObserverMay 21, 2010

    Kesho kajiandikishe ili upate kitambulisho cha kupigia kura, halafu Oktoba ikifika nenda ukapige kura kuchagua viongozi watakaokufaa, anzia ngazi ya chini kabisa diwani wako na kuendelea mpaka juu. Mabadiliko yanaanzia kwa mtu binafsi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...