
NAOMBA UNISAIDAIE KUPELEKA HABARI HII KWA WANA JAMII KWAMBA NYUMBA ILIYOPO KWEMBE MPAKANI KILOMITA 2 KUTOKA BARABARA YA MORORGORO UKIPITIA PALE KITUO CHA MAFUATA CHA NATOIL KABLA YA KIBAMBA INAUZWA.
KIWANJA NA NYUMBA VIMEPIMWA NA WIZARA YA ARDHI NA KIPO KWENYE HATUA YA OFFER. KINAUKUMBWA WA SQUARE METTER 1518.
ASKING PRICING NI 80,000,000/=
SERIOUS PEOPLE WAWASILIANE NA MR. DENNIS NGASOMA 0719 173444 AU 0754 449932 FOR INSPECTION NA KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU NYUMBA HII
NATANGULIZA SHUKURANI MZEE MICHUZI.
ASANTENI


aiseee!!yani inauzwa?
ReplyDeletei hope haiko mambondeni maana gharika hapana,
Maji? Umeme? Miundombinu wakati wa mvua? Ni mambo muhimu ya kuweka wazi wakati wa kutangaza.
ReplyDeleteKaka usiwe unataka kuwatia watu changa la macho. Kwa ninavyofahamu eneo la kwembe ni eneo lenye mgogoro. Labda utuweke wazi ni Kwembe ipi hiyo kwani nami nimeipenda hiyo nyumba na ipo ndani ya uwezo wangu.
ReplyDeleteeeeee makubwa! siyo ya urithi kweli hii nyumba nisije nikatolewa nje na kundi la watu. Ila ni nzuri sema sasa kupata more details ni muhimu wadau.
ReplyDeleteMh barabani kabisaa ama vp... zile mita ishirni na tano zimekaeje?? pls help
ReplyDeleteDuh.... nzuri na yavutia macho... Imesisitizwa ipo barabarani kabisa!! hii imekaaje! manake magreda ya city yatailenga siku moja?? pls tuwekee hii sawa...
ReplyDeleteKwmbe ni eneo lenye mgogoro, unanihakikishiaje kwmba hiyo nyumba iko katika enao salama?
ReplyDeleteHuyu muuzaji bei yake ipo very reasonable. Nyumba hiyo inavyoonekana ipo kwenye maeneo mazuri wadau mwenye pesa achangamkie nyumba hii, kwa ilipofikia na kwa bei hiyo ni karibu na bure, kwani hiyo bei ni ya kununua kiwanja kwa Dar. Lakini jengo limesimama tayari ni finishing tu na ramani ya nyumba inavutia not bad. Kama kila kitu kinaenda kisheria wadau hakuna cha kuwa na wasiwasi changamkeni ningekuwa karibu ningeichangamkia kwani ni bei ya nyanya hiyo.
ReplyDeleteMdau wa Damu USA
unfinished house in Kwembe for 80m, Government house in Oyster Bay 35m!!
ReplyDelete...Usije mjini.......!
ReplyDeleteUshaambiwa ipo jirani na barabara...nunua afu siku kawambwa akohoe ndo utajua road reserve ni kitu gani
ReplyDeleteMchangiaji hapo juu wa Thu May 13, 04:35:00 PM wewe ndo muuzaji nini? Au we ndo dalali? maana duh!!!!!
ReplyDeleteGofu hilo mil 80, tena Kwembe huko !! Makaratasi hayajatulia,offer zipo kibao tunataka hati, road reserve hakuna. Changa hilo !!
ReplyDeleteAkuna mnunuaji humu !!80m unazani kokoto hizo?? humu mnaishia kutoa comment tu hila sizani kama kuna mnunuzi!! jiulize upo ulaya mwaka wa ngapi hata pikipiki hujatuma kwenu !! ndo uje nunua nyumba!! nyie mnachekesha sana!!
ReplyDelete80m hapa nilipo nipo kwenye nyumba ya kupanga uswazi!! unazani napenda !! shekeli akuna.
ReplyDeletewewe muuzaji utakuwa umefulia. kwa nini usimalizie tu kujenga!! kwani ulivyo kuwa unajenga ulikuwa unafikiria ujenge nusu then huuze. Mimi sipendi shinda kabisa bongo wajanja wengi !uje kulizwa 80m hivi kudadeki lazima kuchimbike
ReplyDeletehaiwezekani ukauza nyumba hivi hivi!1 Nasikia bongo ndo deal hizo.ukisha nunua unasaau kama umenunua nyumba. nilisha sikia tukio kama hilo mzee mmoja kila akimuuzia mtu nyumba nunuzi akishalipa tu anasaau. wamelizwa wengi adi hule mzee alipo kufa !!
ReplyDeletewewe utajengaje nyumba then unafika kati unataka kuuza lazima kuna kitu!!! nyumba za urithi hizo
ReplyDeleteumefulia wewe!!
ReplyDeleteBongo kazi...kwanza ujue hiyo ni ramani yako kwa hiyo unatakiwa kubembeleza mnunuzi.
ReplyDeletePili mimi nauliza ni kuwa watu hawafanyi appraizal kabosa au ni markup kubwa sana bongo...Mimi najua finishing ya nyumba ndio inacost sana kuliko kusimamisha jengo na kuweka vigae tu..Unataka kuniambia hicho kiwanja ni ghali sana au ? manake ukiangalia hivyo vigae na hayo matofali yaliyojenga hiyo nyumba hayacost that much...Nasema hivyo kwa vile nimejenga mimi bongo.....
OT hamna kitu nachukia kama mijitu inayosemaga wewe uko ulaya hata hujapeleka pikipiki kwenu...wewe uko bongo mbona huwapelekei wanao huko nje hiyo pikipiki...Kwanini nyie mnangojea tu kuletewa ...Kwanini nyie msiwapelekee watu huko nje hivyo vitu unavyovisema...Mmezidi kuwekesha mabakuli tu...Mnaandika sana huku lakini kila tukija ni asubuhi asubuhi mnaanza kugonga milango....Na kuanza kujieleza na matatizo as if sisi tunaoishi nje ya nchi hatuna matatizo. mimi nina mtoto hivi, mtoto wangu vile...na wengine wanakupa mtoto wakati huna...Unajua mwanao anamaliza shule sijui unaweza kumtafutia huko uliko.....Muache tabia hizo za kufikiri watu walioko nje ya nchi ni easy rider.
mdau wa 10:15:00
ReplyDeleteumewapasha wamezidi kukinga mabakuli kama vile walioko ughaibuni wanafanya kazi benki ya dunia huwa mnatuboaaaa basi tu ati mtafutie fulani shule aje huko nyoo kirahisiiii?! mara ooh huku hali ngumu lo kivipi jamani si kila siku mnasema nyumbani ni kuzuri?? na nyie ndugu zetu wa huko nyumbani muwe mnapeleka misaada kwa wazee sio mnyooshe mikono yenu mirefu hadi huku tulipo hata na sie tuna majukumu yetu nyeti kama ulizaa mwanao usitegemee mtu akusaidie kulea kimpango wenu na perfume nguo viatu marufuku si mnasemaga bongo new york??
Ninachojua. Kiwanja cha Ardhi cha sq.m 1500 ni shs 4 milioni. Gharama ya kujenga hadi kufikia kuezeka ni kama shs 30 milioni. Kwa hio unapotaka kulipwa 80 milioni ina maana faida unayotengeneza ni shs 50 milioni.Ili mimi nimalizie iwe nyumba iliyokamilika itabidi nilipe kama shs 40 milioni juu.At the end of the day nitakuwa nimeinunua hiyo nyumba kwa shs 120 milioni!! Sina ugomvi na hilo. Ila nina hofu. Kwembe siku za karibuni lilitengwa kwa ajili ya kujenga chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbili. Halafu kama uko karibu na barabara kuu iendayo Morogoro inatakiwa uwepo mita 50 kutoka katikati ya barabara. Hilo haliizuii serikali kukichukua hicho kiwanja halafu ukalipwa fidia. Swali. Hiyo fidia utakayolipwa itazidi 120 milioni? Na kwa utalipwa kiasi gani na lini?
ReplyDeleteIn conclusion. Sitaki kununua nyumba hiyo.
Duh, ukitaka kuuza nyumba usiiweke humu watu wanaichambua kama karanga !!!
ReplyDeleteumasikini shida sana. KAMA WEWE UNAYO HIYO HELA NUNUA AU MNUNULIE NDUGUYO. kisa cha kuanza kutukana walio ulaya nini ?
ReplyDeleteAu unajua comment ipi imtoka mzenga, na ipi NY ?