
Serikali mpya ya Uingereza inayoongozwa na Mh. David Cameron imejipunguzia mishahara kwa asilimia 5% kwaajili ya kupunguza bajeti ya rekodi ya madeni.
Vyama vya Conservatives na Liberal Democrats Vimekubaliana siku ya Jumanne kuweza kushirikiana katika kupunguza madeni yanayoikabili nchi na pia kupambana na hali ngumu ya uchumi wa nchi.
Baraza zima la Mawaziri limekutana siku ya Alhamisi kwa mara ya kwanza kujadiliana mikakati ya kuendesha nchi na kujipunguzia mishahara.
Waziri Mkuu David Cameron mshahara wake utapungua toka Paundi £150,000 mpaka kufikia Paundi £142,000 na viongozi wa chini yake watapokea Paundi zisizozidi £135,000 kwa mwaka.
Mawaziri wote watapunguziwa mishahara yao kwa muda wa miaka 5. Kitendo hicho kitasaidia kuokoa kiasi cha Paundi millioni tatu za Kiingereza.
Habari na Ally Muhdin
http://www.tz-one.blogspot.com/
Dah!! Natamani na serikali zetu ziige, viongozi wakubwa kama mawaziri na wengine mishahara yao na matumizi mengine yakipunguzwa kwa asilimia 10, twaweza ongeza idadi ya hospitali na shule za kutosha kabisa!
ReplyDeleteJK vs TUCTA Wanaihua hii habari!!teh teh teh Tafakarii!
ReplyDeletehaya koloni letu hilooo limeanza kwa vitendo tunatakana mawaziri na wabunge wa TANZANIA wafanye namna hii manake wmezidi kujilimbikizia mihela hukoo geneva halafu wanasema ni vicent wakati wenzao wanalilia laki tatu wao wanaita bilioni vicent kufuru hizi zinatoka wapi?? oneni wenzeenu ndo mana haki ya Yesu huko ni ngumu saana kurudi acha iwe mbaya!!
ReplyDeleteWenzetu ako kwenye ligi tofauti na sisi. Viongozo wao wanatumikia nchi na wana uzalendo. Kuhusu viongozi wetu mgogoro wa TCTA unatosha...
ReplyDeleteWabunge wetu mara nyingi sana wanasema wafanye hivi au vile kwa vile 'wenzetu' wanafanya hivyo.
ReplyDeleteHaya sasa, mfano mwingine wa wanayofanya wenzetu huo hapo. Igeni sasa kudaaadeki!
Ama hakika hawa jamaa wana mapenzi na nchi yao. Wabunge na Mawaziri mnangoja nini? Kutangaza mmejipunguzia mishahara japo kwa asilimia 5% tu. Ni matumaini ya Watanzania wote kuwa mtaiga mfano wa hawa jamaa na tutasikia kuwa nanyi mmejipunguzia mishahara, ha ha ha ha ha ha labda jua litoke Magharibi na kutua Mashariki.
ReplyDeletekiongozi wangu hapa kwa jina simtaji anasema hawa jamaa ni sawa wapunguze mishahara kwa kuwa majimboni kwao barabara ni nzuri magari yao hayatumii mafuta mengi kuwafikia wananchi, hivyo basi hata mishahara ya sasa ya viongozi haitoshi inatakiwa kuongeza kwa asilimia 23 ili kukidhi mahitaji na kumfikia kila mwananchi ila wameamua kukaa kimya kwa kuwa wanapenda kutumikia taifa kuliko mapato ya kutosha
ReplyDeleteSERIKALI IJAYO TA TZ NAYO ITAFANYA HIVI, KUPUNGUZA MISHAHARA.LOL!
ReplyDeleteSasa wabune wetu wataiga vipi haya wakati wengi wao wanaomba ubunge ili wapate utajiri? Wenzetu wanaanza kuwa matajiri ndio wanaomba kutumikia wananchi. Kwa sababu hii wakina Freeman, Wakina Ndesamburo wanafaa kuongoza nchi kwa sababu wameutafuta utajiri wao kwa jasho LAO! Au mnasemaje watanzania wenzangu?
ReplyDeletewadau wenzangu,
ReplyDeletekwa ubinafsi uliopo kwa viongozi wetu serikalini na kwenye taasisi mbalimbali hilo la kujipunguzia mishahara ni gumu kutekelezeka. Mpaka tufike huko kwa wenzetu ni lazima mabadiliko yaanze kwenye mioyo ya viongozi wetu. Moyo wa kupenda na kuhurumia taifa letu kwetu haupo, badala ya kutafuta solutions za matatizo yetu kama wenzetu wanavyofanya, wananchi tunatishwa kwa kupigwa na virungu kama tutagoma/tutaandamana kutetea maslahi yetu. Lakini wao kucha kukicha wanajiongezea maslahi na kutembelea magari ya kifahari kwa kodi zetu. Wadau wenzangu tuamke, zile zama za ujinga zimeshapita!!!!
kila afanyalomzungu zuru enhe? maana naona comments nyingi hapa watu wanataka na tanzania waige mfano huu. nchi nyingi zimefanya mseto na watu hapa walikuwa kimya, mpaka mzungu kafanya sasa watu wooooote wanapendekeza haya yafanyike tanzania.
ReplyDeleteKinachotakiwa kufanyika tanzania ni uchaguzi usio na dosari na chama kinachoshinda kipewe madaraka, na sio chama tawala kuendelea kutawala kimaguvu guvu.
eee mwenyezi muumba wa mbingu na nchi
ReplyDeletetufikishe hapa na huu uongozi wetu wa tanzania ili nchi iweke vipaumbele katika mambo ya msingi na maendeleo ya nchii hii yenye utajiri lukuki
amen
Jibu maswali yote kwa kumalizia methali zifuatazo hapa chini:
ReplyDeleteUKIONA MWENZAKO ANANYOLEWA, ....,
ASIYEJUA KUFA............,
ASIYEJUA MAANA,...........,
UKIONA KWA MWENZAKO UNAWAKA,....,
GODON BLUE (BROWN) MIGUU..... KAMA MENDE MFU.
Tafakari, Chukuwa hatua.
Ngo, Ngo, Ngooo....HAKI ELIMU!!!
Jamani mbona mnawasifu sana hawa jamaa, na zile kashfa za wabunge wao mmezisahau? wananunua hata condom na ku claim kutoka serikalini na wao tuwaige? Ama kwakuwa wao ni wazungu?
ReplyDeletealikuwa analipwa hela nyingi lol Paundi £150,000 hivi ni Tshs ngapi vile ni 150,000 x 2000? = 300,000,000/= ambayo ni Tshs 25,000,000/= mshahara pekee. sijui hawa mawazili wetu wanalipwa Tshs ngapi, zitakuwa hazifiki huko na huku kwetu kupunguza ni ndoto. labda kupunguza posho
ReplyDeleteSerikali MSETO itaanza Zanzibar October 2010. Hii ni kwa mujibu wa Mtabiri wetu wa nyota a.k.a ........... Yetu macho, let's wait n c.
ReplyDeleteHapa kwetu kupunguziwa viongozi mishahara hakutasaidia maana wanajua jinsi ya kuzirudisha na zaidi ya hizo watakazopunguziwa. Kwani nani anataka kuniambia viongozi wetu wanaishi kwa mishahara? Wangekuwa na vitu walivyonavyo, magari, majumba, watoto nje ya nchi, nyumba ndogo Nk. Nk.?
ReplyDeleteInafurahisha kwamba wakati wengi waliloliona ni mfano mzuri wa kuweka maslahi ya taifa mbele katika suala la uwezo wa serikali kifedha. Lakini kuna wachache hilo wala halikuwagusa. Wao wameona suala la kuiga kwa wazungu kuwa na serikali ya mseto ndilo la maana, bila kujali kama watawianisha uwiano wa mishahara yao na hali ya uchumi wa nchi au la.
ReplyDeleteBila kuwa na watu wenye nia njema na nchi, mtaunda serikali za mseto, mchanyato na mabumunda lakini zote zitaendelea kuwa mzigo kwa wananchi tu.