Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, na ujumbe wa Bunge kutoka Tanzania wakiwa wamesimama kwa heshima wakati wimbo wa Taifa la Uturuki ukipigwa mara baada ya kufika katika jengo la Historia ya kumbukumbu za kupigania Uhuru wa Uturuki leo jijini Ankara. Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akijiandaa kupokea maua kwa ajili ya kuweka shada la maua kama ishara ya kumkumbuka mpigania uhuru na Rais wa kwanza wa Uturuki hayati Mustafa kemal Pasha katika jengo la Historia ya kumbukumbu za kupigania Uhuru wa Uturuki jijini Ankara, Uturuki leo Spika akisindikizwa kuweka shada
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kama ishara ya kumkumbuka mpigania uhuru na rais wa kwanza wa Uturuki hayati Mustafa kemal Pasha katika jengo la Historia ya kumbukumbu za kupigania Uhuru wa Uturuki jijini Ankara
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mhe. Spika ukitoa heshima za Mwisho
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akijsaini kitabu cha kumbukumbu mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la mpigania uhuru na Rais wa kwanza wa Uturuki hayati Mustafa kemal Pasha katika jengo la Historia ya kumbukumbu za kupigania Uhuru wa Uturuki.
Spika sitta akipata maelezo ya vita vya ukombozi wa nchi ya Uturuki katika jengo la Historia ya vita ya kumbukumbu za kupigania Uhuru wa Uturuki. Kulia ni Mbunge wa Nyang’wale Mhe. James Musalika na Kushoto ni Mbunge wa Muleba kusini Mhe. Wilson Masilingi.
Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2010

    HONGERA MH.SITTA KWA ZIARA YENYE MAFANIKIO.UDUMU UHUSIANO MWEMA WA MABUNGE YETU HAYA MAWILI,IKIWEZEKANA NA WAO WAALIKWE KUJA KUITEMBELEA NCHI YETU

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2010

    Hivi, mbona hawa Waturuki wametokea kuizimia sana Bongo?

    Wachina naelewa wanahitaji mali ghafi, Wamagharibi najua ni mambo yao ya Ubeberu wa kawaida, Wakenya naelewa pia kuwa ni masoko, lakini hawa waturuki nashindwa kuwa-place.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 13, 2010

    mdau umesahau kama mturuki naye ni ulaya,na anamalengo sawa a nchi za ulaya,hujui kama mturuki uchumi wake ni imara kuliko nchi nyingi za ulaya,kama ugiriki na spain hawawezi kuufikia hata nusu uchumi wa jamaa hao,,pia ni moja ya nchi inayoheshimiwa sana kijeshi,ndo maana wanaogopa kuingiza EU,cha muhimu waje kuwekeza kwetu na tufaidike kwa pande zote.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2010

    Kwa anony wa tatu.

    Ni kwamba inaeleweka kuwa uturuki iko ulaya, lakini utaonekana mrahisishaji wa mambo ukisimama mbele ya watu na kusema agenda ya uturuki juu bongoz inashadidiana na ile ya zile nchi za magharibi (yaani, uingereza, ujerumani, japani, marekani, uspaniola, ureno n.k.)

    Ajenda ya nchi za magharibi ni kuendeleza uhusiano wa adult-child (characterised as Ubeberu). Hii inawafaa kwani malengo yao yako long term zaidi.

    Kwa upande mwingine Uturuki imejionesha kutaka uhusiano wa adult-adult kama wanavyofanya wachina.

    By the way, siyo kwamba ni vibaya, kwani hakuna nchi inayotaka kujitenga na mahusiano na nchi zingine

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 13, 2010

    Mh adult adult ndiyo nini sasa! Mi najua huko uturuki kuna galz wazuri kufamtu...

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2010

    Uturuki ni nchi ya 17 duniani kwa utajiri, pia ni ya 3 kwa textile industries duniani, ina lots of big manufacturing industries kwenye nyanja za construction industries, military equipment kama ndege za kivita, vifaru n.k.
    Bila predujice ni nchi ambayo ina waislamu 99% lakini inaendeshwa kimangaribi. Utauliza kwa nini raisi wa kwanza na mpiganiaji wa uhuru marehemu Kamel Pasha aturk anaenziwa hadi sasa ni kwa sababu alikataa kuendekeza utawala wa kidini hususani ya waislam na akawa ni raisi wa kwanza katika nchi za zenye waislamu wengi kuruhusu na kupigania wanawake enzi hizo kuwa na viti bungeni.
    Sikatai kuwa alikuwa na mahusiano ya karibu na watawala wengi mashuhuri wa ulaya enzi hizo.

    Kwa maelezo zaidi ingia: Kamel Aturk biography kwenye google.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2010

    uturuki ni nchiambayo kasi yake ya maendeleo ni kali sanaa ukifananisha na nchizi zingine hapa ulaya miaka ya nyuma ilikuwamkiani leo ni ya saba7 hapa europ nawenyewe wanadai baada ya miaka 15 ijayo watashika 1 au 2,hivyo viongozi wetu wajifunze mengi sanaaa kwa hwa jamaa..

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2010

    Jamani hili jambo la ku-bow down (Kusujudu) kama nionavyo hapo pichani au nionavyo watu wengi wakifanya wakati wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu linanitatiza sana. Zamani nilikuwa nikiona si jambo kubwa lakini sasa baada ya kusoma maandiko matakatifu nikagundua si vema hata kidogo. Mungu hapendezwi kabisa na kiumbe wake yoyote kusujudia chochote isipokuwa yeye mwenyewe. Mungu peke yake ndio wakusujudiwa (Kupigiwa magoti au kuinamiwa). Kwani heshima haiwezi kuonekana kwa njia mbadala isipokuwa kwa ku-bow au kusujudu? Nawakilisha tu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2010

    kwa wenzenu tambarare sio enhheee sio ile dodoma yenu vumbiiiiiii ukameeeeee kwa nini hampafanyi pawe tambarare kama huko mlikotembelea??? aibuuuuuuuuu ati capital loooo!!!! ni capital ya kwanza kwa ubaya duniani pako ovyoooooooooooo!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2010

    Ku-bow down (kuinama) si lazima imaanishe kusujudu. Ninavyoelewa mimi ni ishara tu ya kuthamini jambo (appreciation). Mimi niki-bow down wakati wa kuaga mwili wa marehemu yeyote si kwamba nausujudu, bali nathamini kuwa tulikuwa pamoja na huyo ambaye sasa amefariki na pia natoa sala yangu wakati huo.

    Pengine maana inatofautiana kati ya mtu na mtu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 14, 2010

    sasa wewe anoy 08:03:00 PM umesema ukimsujudia mtu maanake ni kwamba mlikuwa pamoja , sasa hao walikuwa pamoja ???/

    THINK !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...