Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Uturuki Mhe.. Abdullah Gul mara baada ya Spika na Ujumber wa Wabunge wa Tanzania ambao wapo katika ziara ya nchini humokumtembelea Ofisi kwake leo. kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. wilson Masilingi. Spika na Ujumbe wa Wabunge saba upo ziarani Uturuki kwa Mwaliko wa Spika wanchi hiyo.kwa lengo la kuhamasisha wawekezaji katika sekata mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa nchi hizi mbili.
Ujumbe wa wabunge toka Tanzania ukiongozwa na Spika wa Bunge wa Tanzania Mhe. Samuel Sitta, ukiwa katika mkutano wa pamoja na Rais wa Uturuki Mhe.. Abdullah Gul kujadili namna ya nchi hiyo inavyoweza kusaidia maendeleo mbalimbali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wawekezaji toka Uturuki kuja kuwekeza nchini. Spika na Ujumbe wa Wabunge saba upo ziarani Uturuki kwa Mwaliko wa Spika wa Nchi hiyo.
Picha na mdau Owen Mwadumbya wa Bunge


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...