Mshindi wa Vodacom Tuzo milionea Bernard John(27) akifurahia baada ya kukabidhiwa kitita cha Milioni 100 na Mkuu wa uendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Corriea hayupo pichani mwishoni mwa wiki mjini Morogoro Mshindi wa Vodacom Tuzo milionea Bernard John (kulia)akikabidhiwa fedha taslimu shilingi milioni 100 kutoka kwa Mkuu wa uendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Correia katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.Mshindi wa Vodacom Tuzo milionea Bernard John (katikati) akipokea sanduku lenye shilingi milioni 100 kutoka kwa Mkuu wa uendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Correia (kulia )na kushoto ni Meneja wa kanda ya nyanja za juu NBC Ramadhani Lesso Mshindi wa Vodacom Tuzo milionea Bernard John (kushoto) akipokea sanduku lenye shilingi milioni 100 kutoka kwa Mkuu wa uendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Correia,kulia ni Mkuu wa kitengo cha utawala cha mahusiano kwa wateja wa Vodacom Aika Makinda.

========================

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Leo imemkabidhi hundi ya shilingi milioni 100 mshindi wa Promosheni ya Tuzo milionea Bw. Bernard John (27) mkazi wa mjini hapa katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwake na kuhudhuriwa na maofisa wa Vodacom ndugu jamaa na marafiki.

Ujumbe wa Vodacom Tanzania uliongozwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Correia ambaye pamoja na mambo mengine alimpongeza mshindi huyo na kumshauri azitumie fedha hizo kuboresha maisha yake.

“Kwa niaba ya Vodacom Tanzania, ninapenda kuchukua fursa hii kukupongeza sana ni furaha iliyoje kuona mwenzetu katika familia kubwa ya Vodacom Tanzania yenye wateja zaidi ya milioni saba anabadilisha maisha yake kwa kuyaboresha,” alisema.

John alipatikana alipatikana kupitia droo kubwa iliyochezeshwa na kampuni hiyo na kuonyeshwa moja kwa moja kupitia kituo cha televisheni cha ITV chini ya usimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini.

Naye mshindi huyo, aliishukuru Vodacom kwa kuanzisha promoesheni hiyo ambayo alisema inaboresha maisha ya wateja wa Vodacom.

“Kwakweli ninaipongeza Vodacom Tanzania kwa kuanzisha promosheni hii ambayo imebadilisha kabisa maisha yangu na kuwa yenye matumaini, nitazitumia fedha hizi kwa kujiendeleza zaidi kielimu na manufaa ya familia yangu na jamii yangu inayonizunguka,”alisema

Promosheni ya Tuzo Milionea kwa mwaka huu, ilianza mapema mwezi Februari lengo likiwa ni kuwarejeshea wateja wa Vodacom sehemu ya kile Vodacom inachokipata na pia kuboresha maisha ya wateja wake.

Correia alifafanua kuwa tangu kuanza kwa promosheni hiyo ambayo imedumu kwa miezi mitatu sasa, wateja wa wameweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwa ni pamoja na muda wa maongezi.

Correia alisema kuwa kupitia Promosheni ya Tuzo wateja Saba wa Vodacom walijishindia muda wa maongezi wenye thamani ya sh. 100,000 kupitia droo za kila wiki na hadi mwisho wa promosheni hiyo wateja wetu walishindia muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni tisa.

Aidha aliongeza kuwa Promosheni hii ni mwendelezo wa promosheni ya Tuzo milionea iliyoendeshwa na Vodacom Tanzania kwa mwaka jana.

“Kama mtakumbuka mshindi wa droo kubwa ya mwaka jana alikuwa ni Renatus Mkinga, Mkazi wa Mombasa, Ukonga Jijini Dar es Salaam, ambaye alishinda shilingi milioni 100 na kuboresha maisha yake”.

Akitoa wito kwa wateja wengine kushiriki mara nyingi katika promosheni mbalimbali zinazochezeshwa na kampuni hiyo kwa siku za usoni Bw Correia aliwahakikishia kuwa zitawawezesha kuibuka kidedea na kuboresha maisha yao.

“Tutaendelea kuwekeza ili kuboresha huduma zetu mbalimbali kwa kuwa tunaamini kwamba huduma bora na za uhakika za mawasiliano ni sehemu ya maendeleo, kwani maendeleo ya nchi yoyote yanachangiwa na huduma za mawasiliano zenye uhakika” Alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2010

    Michuzi inabidi muelezee kabisa kuwa hizo pesa hakuenda nazo nyumbani la sivyo mtasababisha jamaa avamiwe bure jamani. Kuna watu wana mawazo madogo watasema kaenda nazo nyumbani wakamvamia.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2010

    Afu kesho wakimkaba mnasema vibaka wamezidi bongo,kumbe wenyewe ndo mnawatamanisha.Kwa nini watu wasipewe hizi zawadi kimya kimya kila mtu afe kivyake?Utadhani ni sherehe za ma-gangs in Harlem miaka ileeeeee.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 16, 2010

    Mbona naona hizo bundle za 10mil zipo sita tu..alishindwa kubeba zingine au ni ta imekatwa?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2010

    Halafu kuandika tu check haitoshi mpaka mdhalilishe hela yetu hivi....Kwani kuyaonyesha hayo mahela ndio nini jamani???

    Nilikua namwonyesha mwenzangu hapa aone jinsi million 100 tshs inavyobebwa kwetu akacheka kweli.....

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 16, 2010

    haya kaka jitafutie tu finance adviser ili mambo yako yazidi kuwa mswano usije ukaishia kutapanya ovyoo enjoy mshiko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...