Baadhi ya viongozi wa dini wakichangia masuala mbalimbali leo wakati wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea jijini Dar. Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na serikali kwa lengo kutoa fursa kwa viongozi wa madhehebu kujadili, kutoa maoni na ushauri kuhusu masuala mbalimbali yanayolikabili Taifa.
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akichangua wakati wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea jijini Dar leo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Sera, Uratibu na Bunge Philip Marmo akiongea na viongozi wa Madhehebu ya dini kutoka maeneo mbalimbali nchini wanaohudhuria mkutano wa siku mbili kujadili masuala mbalimbali yakiwemo Sheria za Uchaguzi, Uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010 na Mapambano dhidi ya Rushwa nchini leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wa Madhehebu ya dini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Sera, Uratibu na Bunge Philip Marmo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa siku mbili wa Viongozi wa Dini leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2010

    Kaka michuzi naomba uwasilishe hoja hii ijadiliwe, mdau kanitumia kwenye email anaomba ushauri, nikaona ni vyema nikufowadie jamii ijadili.
    "Hoja"
    anasema boyfriend wake bahili,anasema sio kwamba anataka mwanaume huyo ampe fedha, au kumnunulia kitu, lakini tabia yake ya kudai hana fedha kila siku ndo inamboa.
    ukweli ni kwamba anadai mwanaume anauwezo anataka kutumia fedha za mwanamke tuu, na hata kama hana mwanamke hukopa ili kutatua tatizo linalomkabili boyfriend wake. Lakini tangu wafahamiane na kujuana hajawahi hata kununuliwa zawadi au chochote hata (handikachifu)sasa anasema mapenzi gani ya upande mmoja?mbaya zaidi ni kwamba mwanamke akiwa na tatizo mwanaume haimgusi anadai hana jinsi!
    nawasilisha!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2010

    Ankal mbona ni Vibaraghashia tu ndivyo vilivyokuwa vinachangia mada tu?au ni hizi picha mbili tu?

    Mchambuzi

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 13, 2010

    WIZI MTUPU...WHY NOW?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2010

    Wakianzisha wanasiasa inakuwa sio kuchanganya dini na siasa. Wakianzisha viongozi wa dini inakuwa kuchanganya wizi na siasa.
    Mambo ya aibu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 14, 2010

    Wizi na siasa, duh?? upside down 250 degrees! Achana na hilo, mi sijafurahia hata kidogo kwa viongozi wetu wa dini kukubali kuwekwa sawa. Kwani walikuwa wakitudanganya all this time??? Sasa wakiongea tutajua ni CCM ndio wanaongea kupitia midomo yao. Ninyi viongozi wa dini ndio mlipaswa kuwaita CCM na vyama vingine katika kikao cha KUWAONYA KATIKA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, ninyi ni watu wazito sana (endapo mna-behave correctly). Mmetuangusha sana, sasa hata hatuelewi tumsikilize nani, Kaizari au Mungu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 14, 2010

    Quran "Allah does not like the corrupt'

    BIble "They promise them freedom, but they themselves are slaves of corruption. For whatever overcomes a person, to that he is enslaved."

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 14, 2010

    Mimi naomba wajadili na udini ulioibuka kwa kasi miaka ya hivi karibuni. Maana ukiomba kazi baadhi ya sehemu tena taasisi za umma hupati mpaka uwe wa dini fulani. Madhara yake hiyo ni bab-kubwa wanafikiri watu hawaoni.
    Inaboa ile mbaaaaaya.

    Hata ukiibania sijali.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 14, 2010

    Ankal.....hivi ni nani haswa anahitajika kufahamu sheria za OFFSIDE KTK mpira wa Miguu?! Nadhani ni mchezaji, refa, na Kocha, sie Washabiki tutakubaliana na maamuzi kadiri ya wahusika wanavyotafsiri sheria! Sasa Sheikh au Padri/Askofu, ufahamu wake washeria utasaidia nini kwenye uchaguzi?! HOSEA (refa) amelalamika rafu zimeanza mapema kabisa mbele yake na firimbi anayo mkononi badala ya kuweka mdomoni! Mtazamo wangu hapa ni usanii mtupu na wahusika wanawekwa sawa waache madongo watu "watanue" Wenye "AKILI" zao wataelewa! vinginevyo wajinga ndio waliwao.
    KALAGA BAHOO!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...