Dear Bro Michuzi
Nimefikishiwa maulizo mengi kutoka kwa wadau na wapiganaji wengi wakisema
wamesikia kuwa nimetangaza nia ya kugombea ubunge mwaka huu kupitia CCM
kwenye jimbo la Njombe Magharibi. Napenda kuwajulisha kuwa ni kweli ingawa
ukiacha gazeti moja na habari chache tu ndio vilivyoandika habari hizo. Kwa
sababu mtandao wako unafuatiliwa na wapiganaji wengi ambao wameniulizia juu
ya habari hizo nimeona kuwa niwajulishe rasmi kuwa kweli nagombea kwenye
kinyang'anyiro hicho. Kwa wale ambao hawanijui kwa undani wanaweza kupata
maelezo yote kwenye libeneke langu:
Nimefikishiwa maulizo mengi kutoka kwa wadau na wapiganaji wengi wakisema
wamesikia kuwa nimetangaza nia ya kugombea ubunge mwaka huu kupitia CCM
kwenye jimbo la Njombe Magharibi. Napenda kuwajulisha kuwa ni kweli ingawa
ukiacha gazeti moja na habari chache tu ndio vilivyoandika habari hizo. Kwa
sababu mtandao wako unafuatiliwa na wapiganaji wengi ambao wameniulizia juu
ya habari hizo nimeona kuwa niwajulishe rasmi kuwa kweli nagombea kwenye
kinyang'anyiro hicho. Kwa wale ambao hawanijui kwa undani wanaweza kupata
maelezo yote kwenye libeneke langu:
www.mpumilwa.com
Ahsante!
Ahsante!
Nimejaribu kuweka commenti kule nikashindwa. Ninashukuru kwa kazi nzuri lakini jaribu kufanya / kuweka tafsiri ya kazi zako ni nzuri sana mzee ili wengine waliosoma st. Madenge PS waelewe na wapiga kura wako wengi wako ktk kundi hili
ReplyDeleteSwahiba wangu, kaka yangu Dan Lutte..mimi nadhani ni busara ukaanzisha taasisi kubwa tu ya habari ya kimataifa ambayo walau itakuweka kwenye chati ya media zaidi kuliko huo uvuvuzela ambao ndugu yangu ukiwatoka wananchi japo kwa siku kadhaa kwenda a-town kula ndafu watakushikia bango..njombe magharibi muachie mzee wa majembe..bado majembe yake makali na yanalima kisawasawa...we haya tu
ReplyDeleteMIMI BINAFSI ANAEGOMBEA KWA TIKETI YA SISIEMU NAONA NI WALEWALE
ReplyDeleteNi nini kimekuvutia hasa mpaka ukaamua kujitosa kugombea ubunge hali ukijua ni kazi nzito na ya wito, kwani Njombe ninayoijua mimi watu wanashindia mlo mmoja kwa siku. Utaleta mabadiliko gani na kwa njia zipi na fedha utazitoa wapi?
ReplyDeleteNilimfahamu Danford miaka 40 iliyopita nilpokwenda kusoma Form 5 Mkwawa High School, Iringa. Yeye alikuwa "O" level, (nadhani form 3). Hata hivyo, nilimzoea zaidi kwa kuwa yeye alikuwa katika jazz band ya shule iliyokuwa ikiitwa Orchestra Mkwawa na alikuwa mwigizaji na "crooner". Baadaye, tukakutana UDSM. Najua kuwa alikuwa Daily News, TTC na kisha AICC, Arusha. Nilipokuja Arusha nikamkuta mahakama ya UN ya Rwanda akiheshimika kwa utendaji wake wa kazi (professionalism) katika Tribunal. Lakini watu wengi wa Arusha wanamjua kwa kujihusisha kwake na utamaduni (muziki na michezo {Wazee Club}). Kama ataitumia ari, uzoefu na 'energy'yake kuwawakilisha watu wa jimbo lake kama anavyotoa mchango wake hapa Arusha kwa njia mbalimbali, basi litakuwa jambo la manufaa kwa watu wa jimbo lake. Aidha, naamini kuwa mara nyingi ni vizuri kumchagua mtu ambaye kwa zaidi ya miaka 30 amefanikiwa katika kazi alizozifanya kuliko mtu anayetaka kufanya uwakilishi kuwa "mradi". A. Inkishafi.
ReplyDeleteNakubaliana na Inkishafi. Ni bora kuwa na mbunge ambaye walau ana afueni kimaisha.
ReplyDeletemmmmh wazee wetu nao hawako nyuma kwa kupenda kuuza sura...you look like FISADI!!STAY home n help yo wife care the family.TUNAHITAJI VIJANA.Alaaah..huna hata hayaaa.
ReplyDeleteHIVI TANZANIA HAKUNA NJIA NYINGINE YA KUSHIRIKI KWENYE HARAKATI ZA KULETA MAENDELEO KAMA KWELI WATU WANA NIA YA KULETA MAENDELEO KWA WANANCHI? SASA KILA MTU ANATAKA KUWA MBUNGE.
ReplyDeleteMalafyale Danford Mpumilwa hongera kwa kuweka wazi nia.
ReplyDeleteKura uangu na kula vile vile unayo,
Nduguyo wa siku nyingi-lawerence
Mzee Mpumilwa kwa sasa sioni kama unaye mpinzani,utapita kwa kishindo bila ya upinzani.
ReplyDeleteMaendeleo ya jimbo la Njombe baada ya uchaguzi ndilo litakuwa tatizo la upinzani mkubwa kwako.
jimbo hilo aidha limesahauliwa kwa muda mrefu au huyo utakayemridhi hakupewa nafasi ya kumalizia maswala na matatizo ya kilio cha wakazi wa jimbo,elimu ya msingi bado inayumba yahitajika marekebisho,kilimo cha vijijini hakijapata mipangilio ya mafunzo ya kilimo cha kisasa na mikopo kwa wakulima, mazahanati na usafiri wa wagonjwa katika jimbo hilo yanahitaji marekebisho ya teknologia za kisasa kina mama wengi bado wanazalia watoto majumbani,vijana wengi baada ya masomo ya kati wanakosa kupata ajira na hakuna mipangilio ya mikopo kwa kujituma ibinafsi,wengi hufuatilia njia fupi za kukimbilia miji mikubwa kutafuta ajira.
Hata hivyo nina imani mafanikio yako ya kupita uchaguzi,utafanya mabadiliko makubwa jimbo la Njombe.
KILA LA KHERI
Mickey "MIKIDADI" Jones
GLOBAL ADVANCE TANZANIA NETWORK
Hahaaa ankal bwana eti vuvuzela dahhh inachekelesha
ReplyDeleteKila la heri, tutaonana Bungeni.
ReplyDelete(US Blogger)
Inkishafi, Mimi pia nilikuwa Mkwawa High "A" levels 1970. I'm sure ukitumia jina lako ambalo si nickname nitakufahamu. Mimi pia namfahamu Dan, na ijapokuwa mimi si MwanaNjombe, najua atawasaidia sana watu wa jimbo lake kwa kuwa, kama ulivyosema, yeye mwenyewe ni mtu ambaye kila alikofanya kazi amefanikiwa including hapa UN (Nalijua hili kwa kuwa mimi pia niko hapa UN Arusha). Inatia moyo kuona kuwa kuna watu ambao wamefaulu kimaisha wako tayari "to give back to their communities" badala ya kukaa tu na kutumbua.
ReplyDeleteWe S. Ibrahim, usiite watu ambao huwajui mafisadi. Huyu Uncle Dan huko UN anapata mshahara ambao ni mara kumi au zaidi kuliko wabunge wa wetu. Sasa wacha akatoe mchango wake kwao. J. Gombanile.
ReplyDeleteMjomba Lutengano, sisi huku Njombe tunasamini mchnngo wako na kukuombea Mungu akulinde. Amen. mimi Atanasi.
ReplyDeleteankal Dan, kila la heri...ndugu zetu kule nyumbani wanahitaji viongozi, overseers, ili mawazo yao yatekelezwe..tunachokosea wengi ni kudhani wale wote wa kule ni 'hamnazo'. Na tunaodhani hivi, kwa bahati mbaya sana, tumezaliwa kule, kukulia kule na kupata kijibahati cha kuja mijini!Wametufikishaje tumefikaje hapa tulipo kama hamnazo! Go, Dan, go...wasikilize na uwaongoze. Lusungu
ReplyDelete