Habari wa ndugu wapendwa.

Chama cha waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni Tanzania (CAJAtz) kimeshtushwa na kusikitishwa na uamuzi wa Bodi ya Biashara ya Nje (BET) wa kupiga marufuku maonyesho ya Muziki na Ngoma za Utamaduni katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kupitia waraka wake uliotolewa na UTAWALA, BET imepiga marufuku maonyesho yote ya sanaa za Kitanzania ikiwemo ngoma, muziki na maigizo eti kwa madai kwamba yanaleta kelele. wakati huohuo muziki unasikika ni ule wa wasanii kutoka nje ya nchi kwenye maspika makubwa. CAJAtz inatambua thamani ya sanaa na Utamaduni wa Taifa hili na inaamini kwamba sehemu kama hizo ndiyo muafaka hasa katika kutangaza shughuli za sanaa na Utamaduni wetu.

Tunaamini pia kwamba katika maonyesho hayo ya biashara makampuni na asasi mbalimbali huwatumia wasanii katika kufikisha ujumbe wao kwa watu mbalimbali hasa kwa kuamini katika nguvu ya sanaa. lakini tunashangaa leo hii kuona BET inawataza wasanii kutumia fani zao kutoa ujumbe kwa watu licha ya kuwa makampuni na asasi hizo zimetumia pesa kuwakodi wasanii hao. CAJAtz inaamini kwamba sanaa ni biashara hivyo kwanza ilipaswa kuachwa ili ijitangaze kupitia maonyesho hayo. Pia BET inapaswa kufahamu kwamba kwa miaka yote ambayo wameilezeza kuwa na Mafanikio makubwa katika maonyesho hayo, sanaa na hizo ngoma zilikuwa zinatumika sana katika kusherehesha, kutoa ujumbe na kuelimisha wananchi juu ya mambo mbalimbali ya washiriki. Kwa kitendo cha kupiga marufuku maonyesho ya sanaa BET imekosa UZALENDO na utamaduni wetu na pia imebana ajira ya wasanii wengi walikuwa wameajiriwa na makampuni kwa ajili ya kufanya shughuli za maonyesho kwenye mabanda yao.

Kwa Msingi huo kama wadau wa masuala ya sanaa na Utamaduni hapa nchini, CAJAtz tunalaani vikali zuio hilo ambalo halina tija na limeegemea zaidi ulimbukeni na Kasumba ya watu wa kuthamini sanaa za nje na kuwatukuza wageni wachache kwa visingizio visivyo na maana. Iweje sanaa za Kitanzania iwe kelele na hizo za magharibi iwe burudani? Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kulishughulikia suala hili haraka iwezekanavyo. Pia tunomba BET kutafakari upya zuio hilo.

Hassan Bumbuli
Katibu Mkuu CAJAtz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hili ni jambo la kushangaza sana....Kwa mtazamo wangu binafsi, kelele kwenye maonyesho ya Saba Saba yanatokana na miziki pamoja utangazaji wa biashara na sio ngoma...
    BET inabidi itafakari upya uamuzi huu.....Maana "Mkataa kwao ni mtumwa"....

    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2010

    hii serikali haiwezi kuwa siriaz akija mgeni hapa ndio wanaithamini sanaa wanashinda wamewaanika wasanii uwanja wa ndege tangu sa moja hata kama mgeni atfika saa saba ikiwa wana kampeni wao ndo wa kwanza kuita wasanii washereheshe leo hii eti wanapiga kelele kama baraza la sanaa litakaa kimya kwa hili mimi sitawaelewa! sasa kama wasanii wanapiga kelele kwa nini mnatumia kodi za watanzania kujenga chuo cha sanaa bagamoyo sasa hao wasanii nwataenda kutumbuiza na kuelimisha wapi kama nchini kwao wanaambiwa wanapiga kelele! nataka na waziri wote wawili wa habari na michezo na yule wa biashara kama kweli wana busara wajibu tuhuma hizi wasikae kimya nashindwa hata kuendelea nimeghafirika !

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2010

    Ume wasaidia kuelezea ni jinsi gani sanaa imewasaidia kufika hapo walipo. Pia kuwakumbusha kuwa cha kwao ni bora kuliko vya kigeni. Kwa maoni yangu, katika hali kama hii wasanii hawana nguvu za kuwafanya wabadilishe msimamo wao. Napenda kuwaomba nyinyi kama waandishi wa habari wote na wapiga picha muwasaidie wasanii kwa kususia maonyesho hayo hadi hapo waheshimiwa hao watakapo zinduka usingizini na kuwaruhusu wasanii wajitangaze na kujipatia riziki.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2010

    Mzee Hassan Bumbuli, kwanza nikupongeze tu kwa chombo hiki kutoa msimamo. Lakini si jambo la kushangaza sana kwa nini sanaa ya kitanzania inapigwa marufuku. Sishangai hili kwasababu hata serikali iliwahi kufuta sanaa na michezo mashuleni, na sasa inahangaika kuirudisha. Ninachoweza kutabiri tu ni kuwa maonyesho ya mwaka huu yatakosa msisimko kwa sababu sanaa ilikuwa ni kivutio kikubwa kwa watu wa kipato cha chini. Na ninajua mwakani BET itahaha kurudisha sanaa kwenye viwanja hivi. Watanzania inabidi tujiulize kwa nini tunadharau utamaduni wetu? Kwanza kelele ni nini? Je muziki unaopigwa kwenye redio siyo kelele? Je tutaendelea kudhamini mziki wa kizungu mpanka lini?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2010

    Wewe kama katibu-Mkuu CAJATZ(CAJAtz)waombe wananchi wenye uchungu wa sanaa na utamaduni wa kitanzania wasiende kwenye maonyesho hayo kwa siku tatu au siku zote ili hao Punda(BET)wajue humhimu wa sanaa na utamaduni nasio kulalamika kwenye Blogger

    ReplyDelete
  6. Maudhi mengine ni makubwa, katika maonyesho ya biashara ya nchi nyingine, inatambuliwa kuwa sanaa za maonyesho ni kielelezo muhimu cha utamaduni wa nchi, kwetu wako watu wanapiga marufuku, hivi hawa wakuu hawajawahi kuhudhuria maonyesho ya biashara ya nchi nyingine? kweli Mtanzania unaweza ukafungua mdomo na kupiga marufuku muziki wa nchi yako na kutoa nafasi kwa muziki wa nchi nyingine. Hebu tuwasake kwa majina waliotoa wazo hilo tuwatangaze hadharani

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 30, 2010

    ETI MUNAIOMBA SERIKALI NA WIZARA HUSIKA!!!!!! MNACHOTAKIWA NI KWENDA MAHAKAMANI KUOMBA PINGAMIZI JUU YA HILO, NI MAHAKAMA TU NDIYO INATOWA HAKI NA KUTAFSIRI SHERIA ZA NCHI. GO AND GET COUNRT INJUCTION MAN. KAMA HAMJUWI HAPO WALENGWA NI WANAMUZIKI HASA WA KIZAZI KIPYA WANAPIGWA VITA NA MADONGO, BET WANACHOONA HAPO NI KAMA HIZO NYIMBO ZIKIPIGWA ZINAFANYIWA MARKETING Y BURE BILA YA KULIPIA, NI GREEDY NA UCHOYO, WANAONA WATOTO WATAPATA. MAMBO NI COURT TU.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 30, 2010

    na bado,na huo mkataba wa east africa ukishasainiwa watanzania tutabakia kuwa ma house girls na boys

    ReplyDelete
  9. ni upumbavu wa hali ya juu kwa watawala wetu(sio viongozi maana hawajui uongozi)kwa kuona mila na utamaduni wa kitanzania kuwa ni kelele na badala yake kuruhusu na kushabikia mila na tamaduni za kigeni..Ni watawala wa Tanzania tu ndio wanaoweza kufanya ujinga huu ktk dunia ya leo.wenyewe wanafikiri wakiruhusu tamaduni za kizungu basi kuna nafasi nzuri ya kupata rushwa au "chochote"tokwa kwa hao wazungu.(Ankal najua huwezo toa hizi comments zangu)

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 01, 2010

    Kwa vile wabongo waoga. Huku tuliko watu wakikususia biashara huna...Waulize BP sas hvi wanakiona cha mtema kuni. Kumwaga mafuta yao baharini na kuact like coward sasa watu wamesusia kujaza gas kwa station zao. Leo wanaanza kushusha bei ya mafuta kwnye gas station zao.

    na nyie wabongo amkeni. Mtu akiletea jeuri lala na njaa siku mbili haufi...Msiende kwenye hayo maonyesho for just two days ....

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 01, 2010

    Kwahiyo tunaanzaje kuwaambia wabongo wengine!!?? NDUGU WATANZANIA MNAOMBWA SANA MSITEMBELEE MAONYESHO YA SABASABA MWAA HUU KWABABABU HAKUTAKUWA NA NGOMA ZA KIENYEJI!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 01, 2010

    Maonyesho ya biashara ya kimataifa - kama jina linavyojieleza ni mahala pa kuonyesha biashara zetu, yaani ikiwemo pia na sanaa za ngoma na muziki wa asili! Maonyesho na Matamasha makubwa kote duniani ni FURSA NADRA kwa wafanya biashara na hasa wasanii wa ndani kuonyesha kazi zao, kujulikana na hatimaye kupata mikataba mipya!! Sasa kama mtanzania hawezi kuonyesha bidhaa yake ya sanaa katika maonyesho yanayofanyika nyumbani kwake,tena bidhaa inayoonyesha asili yake, ataonyesha wapi????? Huyu mkurugenzi wa shirika angekuwa kaburu tungeelewa, lakini ni mbongo mwenzetu halisi anawaua wabongo wenzake hivi hivi! yaani muziki wa R. Kelly uwe poa sabasaba, lakini sindimba na gobogobo iwe ni kelele????!!!! Makhilikhili kutoka Botswana wakija hapo hawatazuiliwa lakini sie tunaonekana tunapiga kelele!!!! Tafsiri ya kitendo hiki sio tu inaonyesha jinsi gani watendaji wetu walivyojawa na kasumba za kuabudu mambo ya nje lakini pia WANAUA AJIRA ZA WASANII - Hawajui watendalo sio kosa lao, wanapaswa waelimishwe na baadaye walaaniwe kwa nguvu zote, wanadidimiza utamaduni wetu na pia wanatuua sisi wasanii!!! Jambo la kusikitisha watendaji wengine wa utamaduni mko wapi ili hali anafanya madudu kama haya??? kurugenzi ya Utamaduni iko wapi?? maafisa wa utamaduni mkoa na wilaya mnasubiri nini??? Au mnsubiri Miss Temeke mkapate posho - hii ndio kazi yenu, mtu anapochezea sanaa/utamaduni kama wajinga hawa muwe wakali!!!! mnaponyamaza na sie tunawaona akili za huyo mtu na zetu ni kama ziko sawa!!! JK WATU KAMA HAWA NDIO WANAUONGEZEA MZIGO - ONDOA UCHAFU KAMA HUU, FUKUZILIA MBALI!!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 01, 2010

    BET hovyo kweli, ugonjwa gani unawala hawa viongozi wetu jamani mnanake wamezidi maaaumuzi ya kijinga, mara hakuna muziki , mara tamsha la mashoga ruksa Mafia ilimradi wanalikoroga tu. Kazi imewashinda tokeni wenye uwezo waifanye.

    ReplyDelete
  14. projestus evarist rwegarulilaJuly 03, 2010

    Jamani mimi nilipokuwa huko niliwai kutetea wasanii kwa kusema kuwa WASANII WANATUMIWA KILA SEHEMU lakini wakishatumika wanadharahuliwa sasa ona jinsi wanavyoonewa na BET.Hapa ndo namkumbuka baba wataifa katika kutetea utanzania.Sasa mimi nahisi kwamba wenye vitumbo na wala rushwa wanataka wasanii wahifadhi sauti zao waje wawaimbie wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka huu mhmmmm....muunganiko wa wasanii unahitajika na kama BASATA haina nguvu basi kiteuliwe chombo kingine ambacho ningekuwa kiongozi wake ninge itisha mkutano wa wasanii wote nchini na kuamua kutoa burudani bure kwa wakaaji wa dar katika viwanja vingine na kwa siku zote ambazo maonyesho yanafanyika na hii ingeleta attention kwa wasanii.Kama wasinge sikia,tafuta wasanii wenye akili nzuri wazushe kuhusu kutegwa kwa mabomu viwanja vya SABASABA kitu ambacho kingewaogofya watu kuudhuria maonyesho hayo na hapo BET wangepata hasara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...