Mh. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akikaribishwa makao makuu ya Commonwealth Parliamentary Association (CPA) jijini London leo kwa lengo la kumuaga rasmi Katibu Mkuu wa CPA, Mheshimiwa Dk. William Shija.
Mheshimiwa Balozi Mwanaidi Sinare Maajar leo alitembelea Makao Makuu ya Jumuiya ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Parliamentary Association, CPA) hapa London kwa lengo la kumuaga rasmi Katibu Mkuu wa CPA, Mheshimiwa Dk. William Shija.
Balozi Maajar amepata uhamisho wa kikazi kwenda Washington, Marekani kuwa Balozi wetu mpya nchini humoi.

Dk. Shija ni mwanasiasa mkongwe wa Tanzania aliyechaguliwa kusimamia sekretariati ya CPA kwa miaka mitano toka mwaka 2006. Mwaka huu anatarajiwa kuongezwa muda mwingine wa miaka mitano kukamilisha utaratibu rasmi wa CPA. Jumuiya ya CPA ilifanya Mkutano wake Mkuu wa Kimataifa Mjini Arusha mwishoni mwa mwaka jana (2009).

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Balozi Maajar alisindikizwa na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania London, Bw. Amos Msanjila.


Mh. Balozi akioneshwa sehemu ya kutia saini kwenye kitabu cha wageni na Katibu Mkuu wa CPA Mheshimiwa Dk. William Shija huku Afisa ubalozi Bw. Amos Msanjila akiangalia
Katibu Mkuu wa CPA Mheshimiwa Dk. William Shija akimkabidhi zawadi Mh. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar
Mh. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa CPA





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2010

    Hello Ankal tunaomba fully story ya huyo mbunge aliyewafananisha wanzake "vuvuzela" leo asubuhi bungeni...!!

    ReplyDelete
  2. Hadj Drogba "mwana chelsea"June 18, 2010

    hee!huyu mama bado anaaga tu kazi ataanza lini sasa?naona aliipnda sana uingereza,mama nenda kazini sasa oooh!ingekuwa enzi za LYATONGA MREMA kiti chako cha kukalia pale ofisini ungekifuata ofisini kwake na kupewa siku saba kueleza kwa nini hukuwapo eneo lako la kazi muda wa kazi,hao wenzio wanaokusainisha vitabu wako kazini ohooo!

    ReplyDelete
  3. KELAND N&P SCHOOLJune 18, 2010

    Hongera sana Mama tutakumiss sana. Mungu akabariki huko uendako

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2010

    SAMAHANI WADAU KUULIZA SIO UJINGA NA HUYU BALOZI AMOS MSANJILA AMEOA? NAOMBA JIBU TAFADHALI

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2010

    mwenzio kwenye zile picha za juzi alivyokuwa na full white nilizoom picha nikachunguza vidole vya amos naona havina pete, kaka tunaomba utupe jibu tafwadhali im a sigle lady
    mdau canada

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...