Mojawapo ya mabasi kwa ajili ya wanafunzi yaliyotolewa na Benki ya CRDB. Jumla ya mabasi matano yenye uwezo wa kubeba wanafunzi mia moja yametengwa rasmi kwa shughuli hiyo ya kupakia Wanafunzi tu katika sehemu mbalimbali za Jiji la Dar.
Mgeni rasmi,Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa mabasi ya Wanafunzi,uliozinduliwa na benki ya CRDB katika viwanja vya Karimjee jijini Dar leo

Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh.Jumanne Maghembe pamoja na Mkurugenzi wa bodi ya UDA,Mh Idd Simba wakizungumza katika uziduzi huo mapema leo asubuhi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Kutoka kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh Jumane Maghembe,Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB,Bw. Charles Kimei,Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda,Mkurugenzi wa bodi ya CRDB Bw.Martin Mmali,Mkuu wa Mkoa wa Dar, Mh William Lukuvi pamoja na Mkurugenzi wa bodi ya UDA,Mh Idd Simba wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2010

    inatia moyo, tukipata na mabasi ya abiria y auhakika itakua vizuri sana
    mdau DC

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2010

    Kwa nini hayo mabasi yasiandikwe kwa Kiswahili tu.

    Usafiri kwa Wanafunzi kuliko Scholar Account!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2010

    Tuombe Dua haya mabasi yawe kweli ya wanafunzi!Nakumbuka miaka ya tisini tulichangishwa kwa fimbo pesa za mabasi ya wanafunzi tukitegemea tutakomboka na tenda wakapewa Umoja wa Vijana wa SISIYEMU nyakati za wanafunzi kutoka skuli eti hayo magari yakawa ndio yanapumzika!!!Na nyakati wanafunzi tuko darasani ndio yanapiga mzigo baadae yakapotea kabisaa!!Mpaka Mzee Mwinyi akaagiza mabus ya mashirika ya Umma yawe yanachukua wanafunzi wakitoka maskulini nyakati za Jioni
    Wadau wa Jangwani, Tambaza, Zanaki, Azania , Forodhani wa miaka ya Tisini mtakumbuka mambo haya!!Michu usiibanie hii...Leo asubuhi umentia homa blogu yako ilikuwa ina quiqui(qwiqwi eti ilisema hujalipia)
    Mdau Ugaibuni Magaribi mwa Dunya

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2010

    JAMANI MUWE WAKWELI/BE OPEN AND FRANK JAMANI NANI ALICHANGSHWA MAUS YA WANAFUNZI HIYO MIAKA YA 90 MIMI NILIKUWEPO WAKATI HUO NA AKILI ZANGU HAKUNA MTU ALICHANGISHWA MABUS HIYO SI KWELI NI UONGO MTUPU WENYEWE HASIRA NA KUWAPAKA WATU MATOPE, MABUS YALINUNULIWA KWA PESA YA MSAADA WA BURE ULIOTOLOEWA KWA CHAMA TAWALA NA KUYANUNUWA MABUS HAYO NA KUPEWA UMOJA WA VIJANA KUYANDESHA

    ReplyDelete
  5. Mpalang'ombeJune 08, 2010

    Tatizo la kuwa na viongozi wafanyabiashara litatu-cost sana Tanzania. Hivi mradi wa DART umeishia wapi?, hawa viongozi wetu wanamiliki madaladala kibao matokeo yake wanauwekea kauzibe mradi wa DART ili wasitolewe nje ya biashara.

    Kama DART ingekuwa implemented huu mradi wa wanafunzi ulikuwa hauna haja. Kwani ukiwa na kampuni moja kubwa inapewa tender ya usafiri Dar nzima, haitapata hasara kusafirisha wanafunzi kwani still abiria wote ni wao.

    Nchi za wenzetu unakuwa kuna kampuni mbili au Tatu zinafanya biashara kwenye majiji na still nobody denied a ride. Hawa jamaa kabla ya kuanza propaganda za uchaguzi 2010 kwa kutudanganya na picha za mabasi watueleze mradi wa DART umefikia wapi kwanza?

    ReplyDelete
  6. Nayapa miezi 13 hayatukuwepo barabarani.Wajanja watayanywa kama yale ya mwanzoni.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2010

    Africa tunaitaji viongozi vijana na wasomi, viongozi wetu wote ni wazee uki-compare na nchi za nje. compare kikwete na wengine au rais wa kenya na wengine..wamezeeka akili ya kufikiri si sana ..
    mdau,
    USA

    ReplyDelete
  8. Marangu One.June 08, 2010

    Kama huu mradi hauendeshwi kwa kufuata misingi thabiti ya kibiashara, basi huu mradi hauko endelevu.

    Kama hakuna taasisi inayopata faida kutokana na hiyo service, huu mradi ni kwishnehi kabla haujaanza.

    Yale mabasi ya UVCCM yalikufa kwa sababu hiyo hiyo. Ukweli ndiyo huo na asemayo vingine haelewi dunia inavyoenda.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 08, 2010

    Tunaishukuru CRDB Bank. Lakini hulka za viongozi wa TZ si tunazijua? Hebu subirini mradi huu utakaoishia. Ni mifukoni mwa wenye meno. Wanafunzi hapo hawana lao.Hili ni changa la macho

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 08, 2010

    hivi serikali haioni aibu kwa hili suala mpaka benki ije kusaidia ina maana wizara husika na wanafunzi imelala wapi...! kazi kuomba posho za vikao na utekelezaji wa masuala muhimu kwa manufaa ya jamii hakuna eti unaita dar es salaam jiji no way. huyu pinda naye bila aibu kaenda ningekuwa mimi ningegoma kabisa. viongozi wa hii nchi wananiudhi kabisaaaaa

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 08, 2010

    Mdau benki wanaandika lugha wanayoipenda.
    Wewe wa Kiswahili anzisha yako uandike kiswahili ama kisukuma chako.
    Mnakosoa kila kitu
    Kesho utauliza kwanini mabasi yana mataili.
    Thats being BICHWA

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 08, 2010

    mfano mzuri wa kuigwa watu kama wakina YUSUPH MANJI wakiomba kuchangia mabasi haya sidhani kama watakataa ni watu wa kujitoa kama aliweza kutoa tiketi za mechi ya stars na brasil ambapo sijui zaidi ya milioni mia mbili zimemtoka sidhani kama atakuwa mzito kuchangi japo tubasi kama huto 20 na ikiwa ni sehemu ya kuboresha elimu nchini tanzania

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 08, 2010

    HUYO ANONYMOUS WA PILI HAPO JUU ANASEMA ETI"KWANINI MABASI YASIANDIKWE KISWAHILI".YAANI WEWE UNATAFUTA PROBLEM NYINGINE BADALA YA KUIONA FAIDA YA MABASI.TAFADHALI TUACHE UJINGA!WENGINE WOTE WAMEANDIKA MAONI YA MANUFAA:

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 08, 2010

    Joni Guninita akae mbali kabisa na haya mabasi. Na wewe uanayedai sisisemu ilitoa mabasi elewa kuwa hata sisi ambao hatujawahi kuwa sisiemu tulichangia kama vile ambavyo tulichangia viwanja vya michezo

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 08, 2010

    kwa kweli kimei unastahili heko umelenga watu muhimu sana hope mabenki mengine nayo yatafuata nyayo za crdb

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 08, 2010

    Ninyi wawili, anonymous wa Tue Jun 08, 09:04:00 AM na wa Tue Jun 08, 09:41:00 AM (na wengineo wenye mawazo kama hayo), nitarudia: Mabasi hayo ingefaa yaandikwe kwa Kiswahili sio Kiingereza!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 08, 2010

    Kwa kweli kitu naweza sema kwa Bank ya CRDB, Mungu wangu awazidishie pale mlipotoa , hakuna shida nilikuwa napata kama issue ya wanafunzi, mpaka ilifika mahali nilitamani sana kuleta mabasi kuwasaidia wanafunzi, ingawa bado mawazo haya ninayo. naomba niombe wengine wenye mapenzi mema waige mfano ukitaka kitu kifanyike fanya mwenyewe usisubiri kiongozi wako. Kimei Udumu milele. I envy you! whatever the name these buses will be given , to me it doesn't matter,so long as for students. Wanafunzi mabasi ni yenu tafadhali yatumieni kwa uangalifu msianze kuchorachora, na kugombeagombea ni yenu. Mungu ibariki CRDB.

    ReplyDelete
  18. CRDB, great! Nafikiri Mmekuwa na manejimenti nzuri ndo maana mkafikia hatua ya kuwasaidia wanafunzi. Mdumu milele, Kimei kazi nzuri wewe na wafanyakazi wako wote mbarikiwe. Tanzania inaweza kubadilika haraka kama kila mtu binafsi atabadilika. tupunguze maneno tufanye kwa vitendo. sijawahi sikia CRDB wakipiga kelele oh! hili liko hivi lile vile, ila wameonyesha kwa vitendo, haya wengine mko wapi!!!!!!!! jitokezeni. Asanteni sana wanaCRDB kwa niaba ya wanafunzi na wazazi, tumeguswa na kufurahishwa sana na huduma hii.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 09, 2010

    jambo la maana hili,miaka ya 90 tulihangaika wanafunzi na usafiri lakini wa miaka hii wanakipata cha mtemakuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...