Jamal Zuberi na Mwirabi Sise
MAELEZO Dodoma
19/6/2010.

ASILIMIA 36.22 YA FOMU ZA TAMKO LA
MALI NA MADENI BADO HAZIJAREJESHWA

Jumla ya fomu 20,861 za Tamko la Mali na Madeni zilirejeshwa kutoka kwa Viongozi mbali mbali wa umma. Idadi hiyo ni sawa na asilimia 63.78 ya fomu 32,704 zilizotarajiwa kuwasilishwa na viongozi wahusika.

Hayo yalisemawa leo Bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia wakati akiwasilisha makadirio ya matumizi ya fedha kwa mwaka 2010/2011 mjini dodoma.

Mhe. Ghasia alisema kiasi cha fomu zipatazo 11,843 za Tamko la Mali na Madeni sawa na asilimia 36.22 hazikurejeshwa hadi sasa.

Alisisitiza kuwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inaeendelea kuwafuatilia viongozi ambalo wamekiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 2005 ili wachukuliwe hatua.

Alisema kuwa jumla ya malalmiko 757 dhidi ya viongozi wa umma yalipokelewa na kuchunguzwa ambayo malalamiko 197 yalihusu Sheria ya Maadili ya Viongozi na Umma

Aidha malalamiko 560 hayakuhususiana
na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Alisema kuwa malalamiko kuhusu viongozi hao kwa sasa yapo katika hatua mbali mbali za uchunguzi na malalamiko mengine yamepelekwa kwenye taasisi husika.

Hivi karibuni kumekuwepo malalamiko ya baadhi wananchi kwamba kuna watu wengi wanaolimbikiza mali nyingi kama vile majumba, mashamba kuliko uwezo wa mapato halali wanayopata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2010

    Hizo swiss bank account zao zote wazitaje, na yale majumba waliyoandika majina ya wandugu zao pia yaonyeshwe.

    hao ambao hawataki kurudisha form mkishawachukulia hatua pia majina tuyajue ili tusiwape kura mwakani. mafisadi wakubwa shame on them na mungu atawalaani...Inasikitish unapoona mtumishi wa umma anakua kiongozi within a year anakua na billions. JE HII NI HALALI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...