Kesho Tarehe 26 mwezi Juni kila mwaka Tanzania hujumuika na mataifa yote duniani kuadhimisha Siku ya Kupiga Vita Biashara Haramu na Matumizi ya Dawa za Kulevya . Mkoa wa Dar es salaam umepata bahati ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo yanayobeba ujumbe wa “ Jali Afya yako, usitumie Dawa za kulevya.”Maadhimisho hayo yatafanyika katika viwaja vya mnazi mmoja kuanzia 3.00 kamili na Mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Maadhimisho haya yataanza kwa maandamano yatakayoanzia Kidongo Chekundu na kupokelewa mhe. Rais katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Hatuwezi kuukataa ukweli kuwa dawa za kulevya ni hatari kwa taifa hasa vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa letu , hivyo basi, maadhimisho haya ni changamoto kwa wananchi wa mkoa wetu, kwani Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na tatizo kubwa la wauzaji na watumiaji wa dawa hizi za kulevya, ambazo zimezagaa sana katika maeneo yaliyo mengi kwenye mkoa wetu sambamba na kuongezeka kwa watumiaji wa dawa hizi ambao pia huwa katika hatari ya kupata maambuzi ya VVU na Ukimwi, homa ya Ini ikiwa nikatika kutumia dawa hizi hatari kwa njia zisizo salama ikiwemo kushirikiana vifaa vya kutua dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga
Wananchi wanaombwa kuja kwa wingi na kushiriki katika maandamano yatakayo ongozwa na Police Brass Band kuanzia saa 3.00 asubuhi kwenye viwanja vya Kidongo Chekundu na kupokelewa na mgeni rasmi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia atahutubia kwenye maadhimishio haya.
Wananchi wanaombwa kushiriki kwa wingi katika maadhimisho haya hii ni fursa pekee kwao kupata mafunzo yanayohusu athari za matumizi ana biashara ya dawa za kulevya.
Kutakuwa na maonyesho ya Taasisi, Idara na Asasi za Serikali na zisizo za kiserikali ambazo zipo kwenye mapambano dhidi ya biashara haramu na matumizi ya dawa za kulevya, shughuli mbalimbali zitakuwa zikiendelea kwenye mabanda zikiwemo ushauri nasaha na tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya.
Katika siku hiyo pia kutakuwa na maonyesho na burudani mbalimbali, ushuhuda kwa waliowahi kutumia dawa za kulevya, ngoma , kwaya na wasanii wa Kizazi Kipya Prof J, na bendi ya msondo ngoma watatumbuiza.


duh kumbe hili jani linapendeza kishenzi
ReplyDeleteKwani bangi ni madawa ya kulevya....it's not a drug bwana...."It's a plant that grow like that, but if you happen to put it on fire, there are some effects"...you need this especially if you don't have a job...it will help you see the world different and know what's important in your life....cause you don't think about bills or anything else...if you don't believe follow this link:
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=gWhUqo9Aivs
Mdau-NYC, USA
ifike mahala tuache kufuata mkumbo wa mataifa makubwa kwanza wao wenyewe ndo wauzaji wakubwa refer album ya immortal technique utajua marekani kuhusu madawa ya kulevya. lkn mbona uchumi wa afghanistan unategemea madawa ya kulevya acheni watu waingize hela jamani
ReplyDeleteKWAKWELI NIMESIKITIKA SAANA HII MADA SIKUIONA! WELL, NDIO MAANA WAAFRIKA TUMEKUWA WAJINGA MPAKA LEO NA UMASIKINI JUU KWASABABU YA KUZUIA BANGI, SINA HAJA YA KUORODHESHA SABABU HAPA LAKINI TUANGALIE MFANO HOLLAND HAPO AMBAPO IMEACHIWA HURU KAMA INAVYOTAKIWA KUWA.HAPA KWETU WANAACHIA POMBE, SIGARA HUKU WAKIJUA TUNAZIKA KILA LEO NA MAGONJWA YANAYOSABABISHWA NA MIPOMBE NA SIGARA, LAKINI MPAKA LEO HAKUNA MTU KAFA KWA BANGI, WANABAKI KUSEMA OOH KACHANGANYIKIWA NA BANGI! KAJICHANGANYA MWENYEWE JAMANI
ReplyDeleteAnonym hao wawili wa kwanza wamesema yote ambayo nilitaka kusema.Cocaine na madawa mengine yanayofanywa na chemicals ni hatari,lakini Bangi inachemsha ubongo inakupa fikira ya kujua what to do next!hata babu zetu walizitumia,acheni ujinga nyie wote mnaojifanya eti wasomi.Kwanza hapo Tanzania mikoa kama Mara(ika) na Musoma(ika) ndio kama Jamaika yetu,huko zinatoka Bangi tamu ile mbaya.High Grade,Ganja,Chalwa,Chalice,Lambsbread,Kaya,Herb,Collie,Weed!yote haya ni majina ya jani hili takatifu!
ReplyDeleteCOCAINE NI MMEA PIA UNALIMWA SANA AMERIKA YA KUSINI NA PIA HUTUMIKA KATIKA COCA-COLA KAMA HAMNA HABARI, KWENYE FORMULA YA COCA-COLA COCAINE IPO. NA HILI SWALA LA MADAWA YA KULEVYA NI LA WAKUBWA VIGOGO WANASHIRIKI KATIKA BIASHARA HIYO KWA VILE INA PESA ZA HARAKA WASITUDANGANYE HAPA, WATU WOTE WANAJULIKANA WANAOFANYA BIASHARA HII
ReplyDelete