Huyu dogo asubuhi hii yuko Clouds FM katika kipindi cha Power Breakfast akiongea na Gerald Hando na wenzie baada ya video hii kupata watazamaji wengi duniani ambao walimpenda kwa vituko alivyoonesha akiwa na wachezaji nyota wa Brazil pamoja na JK neshno
Home
Unlabelled
dogo aliyetia fora gemu la stars na brazil atembelea clouds FM asubuhi hii
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
hivi huyu dogo ni mtoto wanani babaka atakuwa mtu maarufu au la ???
ReplyDeleteMnashangilia ugonjwa wa ADHD - Attention Deficit Hyper Disorder!
ReplyDeleteSasa huyu dogo inabidi aachwe. Tusisahau kwamba na madogo wanahaki zao sasa hapa kuna watu wazima huenda wanataka kunufaika kwa mgongo wa dogo... hiyo ni biashara haramu. Natumaini wazazi wake wanafahamu kwamba anahitaji uhuru wake kama mtoto na siyo kutumiwa kama mtaji. Awe mtoto wa mtu maarufu au asiyefahamika hilo siyo hoja. Watoto wote wana haki yakuwa watoto na kutotumiwa kiuchumi.
ReplyDeleteNaungana na Mdau wa pili hapo juu. Inawezekana kweli ni ADHD, wazazi wake kama wanamjali chalii inabidi wajaribu kufuatilia kwa wataalamu wamasuala ya akili. Nimekutana na maelezo mazuri ya ADHD kwenye tovuti hii http://en.wikipedia.org/wiki/Attention-deficit_hyperactivity_disorder
ReplyDeleteSio mnashabikia tu kila kitu, kawa maarufu, sijui ninini, wakati inawezekana kabisa kua dogo ni mgonjwa. Nimefuatilia vizuri hiyo video, na bahati nzuri nimesikiliza clouds fm na dogo kweli attention yake ni 'F'. Ushauri wangu kwa wazazi wake, kama wanasoma hii blogu, au kama michuzi unawajua, waambie kuna ugonjwa uko hivi, then wajaribu kuona wanamsaidiaje dogo, ili kama itabainika kweli ni mgonjwa wajue mapema wanadeal vipi na situation kabla haijawa mbaya.
Cute kid!Mtoto kalelewa vizur huyo..hana nidhamu ya uoga kama wabongo wengine..
ReplyDeleteUnajua wabongo wengi..they don grow..they just learn how to act in public..wako very artificial in short..
Thanks G.Hando..its all about creativity bro..achana nao hao hawajui what is parenthood..na wala hawajakaa na bright kids..
We unaesema ADHD...you lost your mind dude..fani za watu hizo..see this link uone ulivyo huna upeo..
http://en.wikipedia.org/wiki/Attention-deficit_hyperactivity_disorder
Mdau Babati
Sio kwamba anatumiwa kiuchumi, ni vile wengi wameona kuwa yuko entertaining bwana. Sasa kama mtu ana 'kipaji' kwa nini kisiendelezwe? Toka lini mtu akawasha mshumaa halafu akauweka chini ya uvungu? Inabidi ukae sehemu wazi ili umulike.
ReplyDeleteMbona akina Wacko Jacko (R.I.P) walianza shughuli za mziki angali wadogo? Vivyo hivyo yule dogo Zena, na wengine kadha wa kadha.
Kinachokatazwa ni child labour - yaani kumtumikisha mtoto katika mazingira duni na kwa 'kumlalia/kumdhulumu', kwa manufaa ya anayefanyiwa kazi; na pia child prostitution, trafficking na vitu kama hivyo.
Mtoto hakatazwi kujihusisha na shughuli fulani fulani ambazo zitapelekea yeye kujipatia kipato, yaani zenye manufaa kwake, cha msingi awe na wasimamizi (Ma-Manager, mawakala n.k) ambao watahakikisha kuwa hizo shughuli zinamsaidia mtoto.
Biashara Matangazo.
Dodo alitaja jina la baba yek kuwa ni Nesto, sasa sijui.... kwa mdau anayeulizia umaarufu.
ReplyDeleteTatizo si huyu dogo kusumbua bali kuwaminyia vijana wa kila siku wanaookota mipira uwanjani mwishowe wakapachika na huyu anayesumbuliwa na radhi la kukosa utulivu.
ReplyDeleteHuyu Mtoto ameonyesha tabia mbaya lakini sisi kama kawaida yetu tulivyo kuwa tayari kushangilia mambo kinyume, tunaona yeye ndiye aliyetia fora.
ReplyDeleteYaani wale watoto wengine wote walio nyesha adabu pale na kutulia, sasa wao tunawaona walikosea ila huyu ambaye alifanya mambo kinyume kabisa na alivyoelekezwa dniye alitia fora!!!
Hivi hivi ndivyo tunavyowaona majambazi, wala rushwa, waiba kura, wahuni wanaosambaza ukimwi, walevi wa kupindukia, wakwepa kodi n.k. tunawaona wao ni wajanja katika nchi yetu.
Kweli sisi Watanzania tunaishi dunia ya pekee sana.
Only in Tanzania.
Mdau,
Reading, UK.
Four letters ADHD
ReplyDeletedogo mpumbavu tu huyo,sijui hata kama anawezakukontrol mihemko ya mwili wake.upuuzi mtupu,kwanza mi ningekuwa askari ningemtandika viboko skuile mpaka akimbie kichaa.analeta sifa za kijinga tena mbele ya rais! malezi gani alopewwa huyoo?????
ReplyDeleteAsante sana mdau na.3 kwa kudadavua mada hii kwa kiwango cha kimataifa.Mtoto huyu ana haki na uhuru wake utotoni na hapa hakuna la kushangaza umati.Pale uwanjani aliitibitishia duni kuwa yeye ni mtoto na kamwe kwa watoto hakuna msamiati wa ubaguzi wa rangi.Watoto wanatofautiana katika maamuzi na mshikamano na jamii kulingana na mazingira ya malezi yao katika familia husika.Kwa kuwa Clouds FM kituo cha habari za burudani wana kila sababu ya kumhoji huyo mtoto ikiwa ni sehemu ya kazi yao.Angalizo muhimu kwa wazazi na walezi wa mtoto huyu ni kuwa makini na watu wenye nia mbaya.
ReplyDeleteHuyu mtoto ni 100% ADHD. Ushauri wa bure kwa wazazi mtoto apelekwe kwa wataalam na apewe huduma/ushauri wa jinsi ya kuishi na mtoto mwenye ADHD.
ReplyDeleteDogo hana tatizo lolote nyie mnao dhani ni mgonjwa nyie ndio wagonjwa tena mna ugonjwa mbaya "uwezo zero wa kufikiri akili zenu hazina akili". Angalieni vizuri hiyo Video,
ReplyDelete1.Fabiano anaonekana akimfinya dogo kila akitulia.
2.Huyo ni mtoto mdogo, usifikiri anafikiria kama wewe.
3. Na kwa mujibu wa radio mbao hakuwa ball boy wa siku zote alipachikwa tu kwenye hiyo game, so u all haters shut fuck up, ain't no a big deal here. Ass matter of fact, he was heck of funny.Thy fabiano and robinho were chilling wit him
Sijui mnamfaglia nini kupata hits nyingi kwa mambo aliyoyafanya wala sio kitu cha kumshabikia. Tabia mbaya au alikua mdogo kuliko kazi aliyopewa alikua haelewi kwanini yupo pale.
ReplyDeleteIna maana wale waliobehave vizuri wao ndio walikosea.????.kesho kila mtu akiamua kuact up ili apelekwe kwenye radio mtamlaumu nani?
ndio watanzania tuna uoga fulani lakini huyu hapa wala haonyeshi kuwa jasiri bali ni tabia mbaya. na wazazi wake wasipomuongoza na kumfundisha limitations hebu tumpe miaka 12....
AIseee!! watu wanajikokotea dhambi ya bure kabisa,yani nimehudhunishwa sana na huyu aliyetoa maoni ya 15 juni 03;37;00,,na hapo unaweza kukuta ni mtu mzima au hata mzazi kabisaaa!! yani unaongea eti ungemtandika mpaka kichaa......? hivi umeringana hivo bila kujua kwamba mtoto hata apewe malezi ya aina gani haki yake inabaki palepale ,neno la Mungu linasema waacheni watoto waje kwangu kwasababu mbingu ni za kila anayejishusha kama mtoto,,mimi huyu mtoto nadhani hata hao wachezaji au rais mwenyewe hawajakasilishwa vitendo vyake,na hata polisi hawezi kuwa na roho yakuadhibu mtoto kama huyo kwakosa hilo bali yeye ndo anaweza kuadhibiwa,kwasababu wanajua mtoto ni mtoto popote alipo.wadau wanaosema eti anaugonjwa sio kweli,,mtoto nimzima kabisaaa ila hayo yalisababishwa na umri wake,lazima kwa umri wake huo popote alipo lazima aendereza utundu.Na huku ulaya mtoto kama huyo wazungu wanampenda sana kwasababu wao hawapendi mtoto wakuzubaa zubaa.
ReplyDeletehamna lolote huu ni ufisadi tu wa nafasi wale watoto wanaaokota mpira uwanjani mliwakatili kwa vile ilikuwa ni timu maarufu duniani wakampeleka mtoto wao ili auze sura wakati hajui kitu mbona huko south hatujaona haya madudu halafu mnadhani sifa aibu tupu huyu dogo sio mgonjwa bali ni mtundu sana sijui walimpeleka wa nini uwanjani wakati madogo kibao walikuwepo kwani we ankali huna dogo jamani?
ReplyDeleteJAMANI... JAMANI... MAVUVUZELA NI TOO MUCH HADI YANAKERA UTADHANI MKUTANO WA NYUKI DUH!! SIJUI WACHEZAJI HUMO UWANJANI INAKUWAJE YANAVYOKERA WANGERUHUSU MACHACHE MANAKE YANADATISHA MUKICHWA!!
ReplyDeleteJamani mtoto huyu kwanza ni mdogo sana ukilinganisha na hao wenzake...ana miaka kati ya 3 na nusu na minne na nusu...anafanya tunayotegemea mtoto wa umri huo afanye...!!! haumwi wala nini...!!! kiburudisho tosha
ReplyDeleteHuyu dogo ni taahira,hana lolote
ReplyDeleteanko, dogo ana umri gani na ni mara ya ngapi kuja uwanjani kama kijana msindikizaji? maana naona wadau wanabweka kweli utadhani dogo ni mtu mzima vile.
ReplyDeletepili inawezekana kipaji chake ni ucomedy so wadau wajaribu tu kumwendeleza anaweza kuwa mchekeshaji wa kimataifa baadaye.
We hapo uliekywa juu yangu umenikosha kwa moyo gadi nimefurahiiiii mavuvuzela yanakera haaaaha nimeona leo waxungu wanalalama yana boreee.minaona kuhusu huyo mtoto ni utoto pili wanafanta vitu bila kuangalia kuns watoto hiyo ndo mambo yao sasa wao wanafanya kundika tu watoto ilimradi ndo matokeo yake yake kwa ufupi ni aibu sana.ijapokuwa kafurahiiisha au sio ankaaaal!!!!!!! Ybintyyyyyy aka honeypie
ReplyDeleteHakuna ADHD ila kuna fake psychologists mnaodhani kuwa mnajua. Nina master ya Psych kutoka TSU na sipendi wanao misuse psychology.
ReplyDeleteHuyu mtoto amepata umaarufu wa hits like laki 1 kwenye youtube na kwa lugha ya kichikano ambayo hamuijui amepata positive comments duniani.
Huyo mtoto anatakiwa aendelezwe kwakuwa ameshaonesha kipaji cha kutoogopa public and he can be a star na sio kumfanya mzazi aanze dozi ya dawa na woga kuwa mtoto wake ni mgonjwa.
Msiharibu maisha ya huyo mtoto
Please acheni negative comments
ADHD mnayo nyie mnaotaka kujionesha kuwa mnajua. Pia ni ya mwanadamu ni ugonjwa kisaikolojia-wrooooong
Huyo mtoto ni mdogo sana kwa hiyo kazi, anaonekana tu. Umbo tu ndio kubwa. Kosa ni kwa watu wazima waliompeleka hapo lakini ni dhambi kumsemea vibaya huyo mtoto hana kosa ni umri wake tu. Kuna watoto wa aina tofauti wengine huwa ni watundu hadi wakue ndio wanaacha.
ReplyDeleteFundisho watu wasiwe wanaangalia maumbo ya watoto waangalie umri kila jambo lina umri wake.
Nani aliyewaambieni kuwa dogo alipelekwa uwanjani kuokota mipira??? huyu dogo alikuwa miongoni mwa watazamaji,aliruka uzio mmoja baada ya mwingine akazama ground.
ReplyDeleteWabeba maboksi mnaleta mambo ya ADHD.. Case ya huyu mtoto ni tofauti in a way that huyu mtoto ni mdogo kwanza, umbo lake linaonyesha ni mkubwa lakini sio, huwezi kusema mtoto wa miaka minne akawa ana attention ya mtoto wa miaka 7 na kuendelea, na hii haihusiani na malezi. Mnaoona ni adabu mtoto kulelewa kwa kuchapwa haisaidii bali inazidisha ukaidi. Huyu mtoto anatokea mazingira yanayomruhusu kuwa huru kufanya anachotaka ili aadapt mazingira yake na haihusiani chochote na ADHD..!! Nimekaa Marekani miaka 19 na huyu mtoto hayupo anywhere close to ADHD because i have encountered kids and adults with ADHD cases
ReplyDeleteHuyu mtoto inawezekana alikuwa tu hyper au ni mtoto ambaye ana uchangamfu na wala haihusiani na ADHD..!! Nyie mliokaa miaka yenu mitano Marekani mnaojifanya hiyo ni ADHD wala hata sio, nyie mmekariri sijui. Huyu mtoto umri wako unaonyesha ni mdogo sana na nina uhakika kuwa he's under 5 years old kwa hiyo attention deficit kwake haipo sababu ukiona mtoto wa umri huo anakuwa na attention mnayoitaka nyie ya kiutu uzima basi na wenyewe ni ugonjwa na mara nyingi huwa inafanya watu kama hao kuja kuwa na an isolative life. The kid is having fun and that is all so acheni kuandika pumba.
ReplyDeleteKama si ADHD basi ni ADD full stop.
ReplyDeleteAnkal hebu tutolee huu upuuzi. Na wazazi kama wana enjoy ADHD na au ADD basi ni wao. Please dont share it with us. Mi huyu mtoto namjua personally. He is abnormal.