miongoni mwa waliojaza na kurejesha fomu leo leo kugombea nafasi mbalimbali
Muda wa kurejesha fomu za kugombe uongozi kwenye klabu ya YANGA ambao uchaguzi umepangwa kufanyika Julai 18 umemalizika robo saa iliyopita na takriban wagombea watarajiwa 40 wamechukua fomu kuwania nafasi mbali mbali .
Hadi Globu ya Jamii inapaa hewani jumla ya w
agombea watarajiwa watano wamesharejesha fomu kuwania nafasi ya Uenyekiti, na wengine wanne wawania umakamu mwenyekiti.
Wanaowania Uenyekiti ni Francis Kifukwe,
Mbaraka Igangula, Edgar Chibula, Ally Mwanakatwe na Constatine Maligo
Kwenye kinyang'anyiro cha Umakamu wa Mwenyekiti kuna Ayoub Nyenzi, Davis Mosha, Abeid Mohamed Abeid na mwenyekiti wa kamati ya Miss TZ ankal Hashim Lundenga
Kwa upande wa mwenyekiti sijaona,makamu mwenyekiti anayeweza kuifaa Yanga ya sasa ni MPIGANAJI DAVIS MOSHA,uncle HASHIM LUNDENGA ANAFAA PIA,HE IS A GOOD ORGANIZER Lakini angegombea ujumbe ungemfaa zaidi yeye na MAJID KABURU wanafaa zaidi kwenye ujumbe.wengine Kina MALIGO,KIFUKWE,IGANGULA hawawezi kuwa jipya,bahati mbaya sana YANGA ina watu wengi wenye uwezo na ushawishi lakini hawajitokezi kugombea nafasi tofauti na wenzetu simba,YANGA kwa muda sasa tumekua na tatizo sana katika nafasi ya mwenyekiti,ilikua chance nzuri ya kupata mwenyekiti asiye mtu wa makundi,bahati mbaya sana zitarudi sura zilezile,watu kama nyie kina uncle michuzi hiyo YANGA yenu sijui hata mnaifanyia wapi maana hamjitokezi kugombea kuiongoza timu yenu wakati mna vision.Tafadhali msiibane comment hii,nimetumia muda wngu wa thamani sana kuiandika tena kwa uchungu na masikitiko makubwa.
ReplyDeleteNi kipindi muhimu sana kwa club ya yanga. Nashangaa sana wako wapi watu wanaojua mambo yanga? hawajitokezi jamani! Viongozi wababaishaji wenye mawazo ya uadui badala ya ushindani dhidi ya washindani wetu Simba ndiyo huchukua form. Mpira siyo uadui! Viongozi wa aina hii hupoteza muda mwingi kufikiria namna ya kumufunga simba badala ya kuitengeneza club kisayansi ili automatically iweza kuzifunga timu mbalimbali pamoja na simba mwenyewe. Club haina hata website halafu tunajidanganya ni club kubwa. Kumejaa mawazo ya kipuuzipuuzi tu, hili nililiona pale Tegete aliporudishwa kutoka majaribioni eti kwa ajili ya mechi moja. Eti watu wanajivunia uanasheria! kama wanasheria wanauwezo huo wa uongozi ni ajabu sana.
ReplyDeleteIli soka la Tanzania liweze kukua lazima watu wenye akili waingie katika vilabu hivi Yanga na Simba hata katika vilabu vingine au vilabu hivi viwili vifutwe kabisa visiwepo ndiyo maendeleo ya soka yatapatikana.
Maana viongozi wa mpira hapa Tanzania hadi wale wa TFF huonyesha 'unazi' wao katika maamuzi mbalimbali kwa kuangalia masirahi ya klabu anachohusudi. Hata akija kocha yupi kuifundisha stars ataondolewa na Yanga na Simba tu. Maximo anaondoka kwa sababu ya 'unazi mbumbumbu'.
YANGA OYEE!HII MADA TUNAOMBA KWA BLOGGER ASIIONDOE,AIACHE KWA MUDA ILI WATU WATOE MAONI YA KUTOSHA,AKIITOA HARAKA WENGINE WENYE MAWAZO MAZURI TU WANAWEZA WASIIONE,YANGA NI CLUB KUBWA YENYE MASLAHI YA JAMII KUBWA YA WATANZANIA KAMA ILIVYO SIMBA,NA SASA INAPITIA KATIKA KIPINDI KIGUMU SANA CHA UCHAGUZI UTAKAOWASIMIKA VIONGOZI WATAKAODUMU KWA MIAKA MINNE MADARAKANI,HIVYO BASI WAKIPATIKANA WAZURI MAANAKE NI AMANI - MAENDELEO KLABUNI-TAIFA AND VICE VERSA.HIVYO UMAKINI UNATAKIWA KATIKA KIPINDI HIKI NDIO MAANA TUNAOMBA TUPEWE NAFASI YA KUTOSHA HUMU ILI TUWEZE KUWATAMBUA SAWASAWA WATU WALIOCHUKUA FOMU NA KUZIREJESHA KUPITIA MAONI YA WATU MBALIMBALI WANAOWAFAHAMU WATUPE UWEZO WAO NA UDHAIFU WAO ILI MWISHO WA SIKU TUPATE KILICHO BORA,SIO BAADAE TUNAKUJA KUSIKIA AAHH!YULE KUMBE MNYAMA N.K.SASA YANGA KUJA KUONGOZWA NA MNYAMA TENA KWA MIAKA MINNE NI UNYONGE SO MR. MICHUZI LIFANYIE KAZI OMBI HILI
ReplyDeleteheee!KIFUKWE tena?!!!!!!Yale .....yaleeeee!
ReplyDelete