DA' SHERRY KAJEMBE
BAADA YA KUAMRIWA NA WADAU, GLOBU YA JAMII IMEFANYA JUU CHINI NA HATIMAYE KUFANIKIWA KUPATA UHAKIKA KWAMBA DADA YETU SHERRY KAJEMBE, AMBAYE ALIKUWA ANATAFUTWA NA MAMA YAKE BAADA YA UKIMYA WA TAKRIBAN MIAKA MITANO AKIWA HUKO UJERUMANI, AMEONGEA NASI NA KUTUHAKIKISHIA KWA MDOMO WAKE KWAMBA YEYE NI MZIMA NA YU BUHERI WA AFYA NA ANAENDELEA NA MAISHA YAKE HUKO UJERUMANI.
DA'SHERRY ANATOA SHUKURANI KWA WADAU WOTE WALIOONESHA UPENDO NA UVUMILIVU KWA KUMUULIZIA KILA MARA TOKA TANGAZO LAKE LITOKE KATIKA GLOBU YA JAMII. ANASEMA HANA CHA KUWAPA ILA KUWAOMBESA KWA MOLA AWAONGEZEE MOYO WA IMANI NA UPENDO WALIOONESHA KWAKE NA WOTE WALIOPATWA NA MASWAHIBA KAMA YEYE. NA KATIKA KUTHIBITISHA YU SALAMA SALIMINI DA'SHERYY AMETOA NAMBA YAKE HII +491 51223 907146 ILI MDAU YEYOTE ANAYETAKA KUONGEA NAYE WAWASILIANE.
DA'SHERRY AMESEMA UKIMYA WAKE ULITOKANA NA MATATIZO YA KAWAIDA KWA BINADAMU AMBAYO SASA AMEWEZA KURUKA VIUNZI VYAKE NA KWAMBA SASA MAMBO NI MSWANO. ANASEMA AMESHAONGEA NA MAMA YAKE KITAMBO NA KUMTAKA RADHI KWA KUWAWEKA ROHO JUU MUDA WOTE HUO.
WAKATI TUKISHEREHEKEA KUPATIKANA NA PIA KUONGEA NA DA'SHERRY, GLOBU YA JAMII INAUNGANA NA WADAU KUTOA MKONO WA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU CAROLINE NJAU AMBAYE ALITOWEKA NYUMBANI KWAKE HUKO CALIFORNIA NA KISHA KUKUTA AMEZIKWA NYUMA YA NYUMBA YAO.
MOLA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI NA AWEZESHE ALIYEMFANYIA UNYAMA HUO APATIKANE NA KUPEWA ADHABU STAHILI
- AMINA
HABARI YA AWALI YA DA'SHERRY BOFYA HAPA
Mkuu hii namba ya simu ya sister si sahihi nimejarigu mara kadhaa nikitaka kuongea nae ana kwa ana simu hii inajibu kuwa na hii haipo
ReplyDeleteASANTE
Nbr za Ujerumani huwa +49 then followed by ten digits. Hii nbr ziko digits 12 baada ya +49, something isn't right here.
ReplyDeleteAnyway unamtafutia nini? Nugu yake au unatafuta umbeya zaidi tu??
hhahaaah!!!!
kaka Michu,naona hii namba ina mgogoro nimejaribu inaingia voice mail.
ReplyDeleteASANTIII
Michuzi bado siamini hii habari.
ReplyDelete1.Mama yake hajathibitisha kama ameongea nae au aliyeongea nae kweli ni da sherry.
2.Je Globu ya jamii iliongea nae na inathibitisha kweli ni yeye?
3.Hii namba uliyotoa haifanyi kazi hii inaleta mashaka.
4.kuna watanzania wengi German hata wewe michu unaendaga sana huko
kwa nini usimtafute watanzania na sio mmoja watuthibitishie kwamba wamemuona kwa macho yao?
Ni mawazo yangu tu.
Mdau wa Kijito nyama.
kaka michuzi angalia tena kama hiyo namba ni sahihi.hata mimi nimejaribu kuipigia na haiendi.
ReplyDeleteswali lingine kwako kaka michuzi.hivi si ulikua Ujerumani hivi karibuni? hukufanikiwa kupata konozzzz na da'Sherry. hiyo ingekuwa mwake sana..hahahha....ukienda tena ulikumbuke hilo.
Safi sana ankal!! Nimependa sana jinsi ulivyo sensitive na mambo ya jamii haya. hasa juhudi zako mpaka tumemsikia sista weyuhuyu na concerns zako kwa mpendwa wetu marehemu carol. Endelea kuonyesha ushirikiano mjomba ankal!! Ushirikiano daima mjomba wangu ankal!!! Mdau wa Pajazzzzzzzzzzzz na Titizzzzzzzzzzzz!
ReplyDeleteSASA ULIKUWA UMEMNUNIA MAMA YAKO??KUMKALIA KIMYA HIVYO NDIO NINI???
ReplyDeleteNamba ya Kisanii hiyo....au ulikupigia kwa kadi Bwana Michuzi ukafikiri ndio namba yenyewe??Nafikiri ni namba ya calling card, haipo namba hii
ReplyDeleteMdau
Khamis Hassan Batanyaga
Ugaibuni
Lile libeneke la Michuzi Youth Social Initiative vipi kaka?Naendelea kusisitiza mpaka urespond!!!
Michuzi,
ReplyDeleteHao wanaompigia wote na kulalamika kwamba hapatikani kwa namba hiyo ni ndugu zake wenye nia nzuri kweli au ni WAKWARE tu hao?
Chunga sana!
Mlevi ama wewe kweli ni mlevi kikweli kweli, sasa unamuuliza michuzi yeye atajuaje? unadhani michuzi anawajua kila anaeleta comments hapa?
ReplyDeleteHuoni kama labda baadhi yao niwasamaria wema na wanataka kumjulisha tu kuwa kama wapo watanzania wenzake na kama ana matatizo asishindwe kuwasiliana nao.
Hata hivyo huenda wengine pia wanataka wampate na kuanza kumshambulia.
YOU VEVER KNOW, lakini suali lako ungeliwauliza wanaolalamika kuwa wamepiga simu na number ni wrong, hao ndio wanaojua madhumuni yao moyoni.
Ingawa huenda ndugu zetu wengi mliojaribu kumpigia simu mna nia nzuri lakini jee mumefikiria ni kiasi gani itakavyokuwa kero kwake ikiwa kila aliekuwepo hapo ujerumani atakuwa anampigia simu?
ReplyDeleteNadhani kama kuna jumuia ya watanzania basi ni bora mumchague mtu mmoja na ampigie simu na kumkaribisha katika jumuia.
Wengine labda muweke number zeni za simu hapa pamoja na maeneo mliopo, sherry ataziona hapa na atawapigia wale walio karibu nae.
Sahihisho: SI Caroline Njau NI Caroline Mmari. Tuendelee kumuombea.
ReplyDeletemimi simpigii simu mtu kama huyu sherry, hana utu ana roho ya unyama kwenda ulaya ndio kajiona kawa mzungu na yeye anaacha kuongea na mzazi wake, hata kama hujatunzwa nae bado ni mama yako. Najua atasoma hii msg yangu kama nikimtafuta au kumpigia simu nitampa vipande vyake haswa kumpa ukweli asijione leo kapata. Kwa sasa niko ujerumani kikazi nina muda mwingi sana wa kuzurua manake nishamaliza kilichonileta ila sababu ya hali nzuri nimeona nitembee kidogo. ila sheri tafadhali ukiniona kaa mbali manake nitakuchapa kibao.
ReplyDeletendimi twanga pepeta
mdau wa Sun Jun 13, 07:24:00 AM unasema kuwa mwenzio hana utu na ana roho ya unyama, jee unajua sababu hasa zilizomfanya asiwasiliane na mzazi wake? labda alifikwa na mabaya au alifikwa na magonjwa au hata kuwa jela you never know. Si juu yako wala juu yangu kumjudge, ni juu yake kumueleza mzazi wake kilichomsibu na kama mzazi ameridhika na sababu alizopewa who are you to critise?
ReplyDeleteAcha kulaumu watu na acha chuki binafsi kwa walio nje ya nchi.
By the way ni nani alokwambia kama umpigie simu any way?
Mungu ni mkubwa kama amepatikana na yu mzima! Huyu Dada nilikuwa nae Oljoro JKT miaka ya 1991/92. Toka tulipomaliza sikuwaki kupata habari zake. Nimefurahi sana kusikia anaendelea vizuri. Ila alichokifanya si kizuri.
ReplyDeleteBAURAWISE
SAMAHANI KAKA MICHUZI, KUNA WATU WANAKUCHEZEA AKILI YAKO.
ReplyDeleteHIYO HABARI NI FEKI!!
1. ANGALIENI WANATOA PICHA ZAKE ZA ZAMANI TU ZA ENZI YA UHAI WAKE.
2. NUMBER YA SIMU FEKI.
3. HUYO MZUNGU WAKE ANASHIRIKIANA NA WANAWAKE WENGINE WAKIBONGO KUTOA HIZO HABARI NA PICHA FEKI!
4. KAMA NI KWELI AKAREPORT UBALOZINI.....