Hi all
Wateja wa Tigo wapewe taarifa hii kutoka Tigo kuhusu swala la usajili kwamba
Ikiwa hawajasajili hadi leo waende wakasajili kwenye vituo vya karibu mapema iwezekanavyo kwa kuwa siku zimekwisha!!!

Ikiwa watapata mesaji hii hapo chini pia wanatakiwa wafuate maelekezo yaliyopo kwenye meseji hiyo ili namba zao zisije zikasimamishwa kwa madai ya kwamba hazijasajiliwa.
Meseji hii inatumwa kwa wale wateja ambao hadi sasa namba zao hazijaingia katika orodha ya waliosajili namba zao hadi leo.

Ndugu mteja wa Tigo bado hujasajili namba hii, tafadhali jisajili leo. Kama ulijisajili zamani tuma neno JINA kisha jina lako kamili na namba ya fomu kwenda 106.

Tigo tunawashukuru sana watanzania kwa
ushirikiano wao mkubwa katika zoezi hili la kusajili namba zao za simu
Asanteni sana
Meneja uhusiano wa Tigo
Jackson Mmbando

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2010

    Tigo tumewapata ila kwanini makampuni mengine ya simu yasitupatie namba za kucheki kama simu yangu imesajiliwa? Kwa mfano " *106Reli".

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2010

    This an open comment. Ninaipenda Tigo ndio maana I dare to tell you that WATU mliowapa kazi ya kusajili they were not serious.

    How comes for a person who registered to a vendor since July 2009 is TODAY informed that his/her number is not registered? Halafu when we send to you the details through the 106 as you guided us, still YOU SEEM TO pick up the snails response. Kwa hili hamjanifurahisha. Be quick and act fast. Ulimwengu wa ushindani huu isije ikawa mlifanyiwa kazi na MAMLUKI.
    MDAU WA THUMNI

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2010

    Bwana Jackson Mmbando nasikitika kusema kwamba Tigo ni kampuni ambayo haiko serious kabisa. Mimi nilisajili namba yangu mwezi Desemba tena ktk ofisi za tigo pale mlimani city nimekaa siku zote nikijua line yangu imesajiliwa leo nacheki kupitia namba 106 naambiwa eti haijasajiliwa!!!!this is lack of seriousness na ni ujinga kabisa. On the same day nilisajili line yangu ya Zain na Voda palepale Mlimani city na nimecheki wamenitumia sms kwamba line yangu imesajiliwa. Uzembe wenu Tigo utawatia hasara wateja wenu tutapofungiwa na huku tulishajisajili na nyie vitabu na mkavikalia. Kwetu sie wateja hatuna shida kwa sababu tunazo line za Voda na Zain ambao wamekuwa serious na zote ni sh.1 tu siku hizi. by Deo Johnson.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2010

    Tigo hamko serious watu tulishajisajili tena ofisini kwenu leo mnatutumia msg eti hatujasajiliwa, ujinga huo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2010

    Anon wa Pili - Thumni

    What?

    Au unatukumbusha ule wimbo uliovuma hapo kitambo?

    ' ... sitishiki mimi sibabaiki, niko freshi na niko fitii, nilie nae hachukulikii, hata mkiwa na mamlukii ... Ni rahisi kubeba maji kwa pakacha kuliko yeye kuniachaa ...'?

    Kwa hiyo, tiGO ndio inayosababisha hiyo 'snail response'?

    Mdau,
    Wichita, Kensas,
    USA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...